PITA KATIKA NJIA KUU.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafari maneno ya uzima wetu.

 

Maandiko yanasema Neno la Mungu ni taa na mwangaza wa njia zetu

 

Zaburi 199:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu”

 

Sasa katika ulimwengu wetu huu tunaoishi zipo njia za aina mbili tu na kati ya hizi ni lazima mwanadamu apite moja. Haiwezekani kuzipita zote kwa wakati mmoja katika maisha yake.

Na njia hizo ni njia ya UZIMA  na njia ya MAUTI. Hizi zote ni njia na zina utaratibu/kanuni zake za kupita.

 

Mungu anamwambia Yeremia ameweka njia ya mauti na njia ya uzima..

 

Yeremia 21:8 “Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya UZIMA, na njia ya MAUTI.  ”

 

Unaona hapo! Sasa hizi njia zikoje?

Njia ya uzima inampeleka/kumuongoza mtu uzimani na njia ya mauti inamuongoza/kumpeleka mtu kuzimu(katika ziwa la moto).

 

Njia ya uzima ni moja tu wala haina mikatomikato au kujikunja kunja na haijagawanyika mara nyingi kama maandiko yanavyosema..

 

Yohana 14:6” Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

 

Hivyo njia pekee ya kumfikia Baba/Mungu mwenyewe si nyingine bali ni Yesu kristo peke yake. Hakuna njia mbadala au mtakatifu Fulani au mtu awaye yoyote ila Yesu Kristo Bwana wetu.

 

Lakini njia ya mauti ni moja pia lakini haijanyooka imegawanyika mara nyingi nyingi sana kiasi kwamba mtu ni ngumu sana kuelewa kama yuko katika njia ya mauti.

Maandiko yanasema..

 

Mithali 14:12” Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.”

 

Unaona hapo anasema “iko njia ionekanayo….” unaona kumbe njia hiyo inaonekana kuwa ni moja kwa macho ya nje na kwa udanganyifu wa mioyo yetu na shetani.

Lakini anamalizia kwa kusema… “…lakini mwisho wakwe ni NJIA ZA MAUTI.”

Ni njia moja lakini imegawanyika gawanyika mara nyingi nyingi sana. Hii ni hatari sana. Hii njia ya mauti ni ibilisi/Shetani.

Na watu wengi sana wanamuabudu shetani kupitia mambo mbali mbali au vitu mbali mbali kama vile Sanamu,miti,mawe,waganga wa kienyeji,wachawi,fedha,dini/madhebehu,nk hivyo unaona maandiko yanavyotwambia kuwa ni noja lakini inamatawi mengi mno na zaidi ya hayo.

 

Na maandiko yanasema kuwa kuzimu hakuna lango moja bali imesema kuna malango mengi sana kule tofauti na mbinguni ambako lango ni moja tu nalo ndio Yesu wetu Kristo mwokozi wa roho zetu.

 

Sasa maandiko yanasema kuwa “….hapo patakuwa na njia kuu…..”

Isaya 35:8” Na hapo patakuwa na NJIA KUU, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.”

 

Unaona hapo njia kuu ni njia ya uzima na njia pekee ni njia ya mauti.

 

Akimaanisha kuwa wote wanaotembea katika njia ya uzima ambae ni Yesu Kristo ni lazima utakatifu ndani yao. Sasa na maandiko yanavyisema katika kitabu kile cha Waebrania(12:4)

 

Na pia ni lazima wawe ni wasafiri. Ambapo tunajua msafiri ili aweze kudumu katika safari yake ni lazima akae katika chombo ili aweze kufika katika safari yake anakokwenda na awe makini hata anapotoka nje gari lisimuache…

 

Na tunapokuwa kwenye safari hi njia kuu ya Yesu Kristo mambo ya kidunia ni lazima mambo ya ulimwengu huu hatupaswi kushikamana nayo kabisa.

 

1 Petro 2:11 “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.”

Unaona sisi ni kama wapitaji tu hivyo tusishikamane na mambo ya dunia hii kabisa. Maana yatatufanya tuwe wakaaji na walasio wapitaji.

 

Maaandiko yanasema kuwa “ijapokuwa ni wajinga” lakini kamwe hatapotea katika njia hiyo dunia hii itkakuona kama kuwa ni mjinga,umerukwa nakaili,hujitambui lakini kaa katika njia hiyo hiyo kuu kamwe hautapotea amesema Mungu mwenyewe.

 

Usiuangalie ulimwenu unasema nini ama unakutazaje ndugu, ikiwa umeamua kukaa katika njia hiyo ya utakatifu asikuyumbushe Mtu, mwamwagalie Mungu.

 

Ufunuo 7:15-17” Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.

16  Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.

17  Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.”

 

Swali la kujiuliza wewe ndugu yangu uko katika njia ipi? Ya UZIMA au ya MAUTI.

 

Maandiko yanatuonya na kutwambia

 

Kumbukumbu la Torati 30:14-15 “Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.  [15] Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya”

 

Shalom!

 

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *