
SIKU ILE NI SIKU YA FUJO
Ezekieli 7:5 “Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, jambo baya la namna ya peke yake; angalia, linakuja.
[6]Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.
[7]Ajali yako imekujia, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; SIKU YA FUJO, wala si ya shangwe milimani.
[12]Majira yamewadia, siku ile inakaribia; huyo anunuaye asifurahi, wala asihuzunike auzaye; maana ghadhabu imewapata wote jamii.
[13]Kwa maana auzaye hatakirudia kilichouzwa, wajapokuwa wangali hai; kwa sababu maono haya yawahusu wote jamii; hapana mmoja atakayerudi; wala hapana mtu atakayejitia nguvu katika uovu wa maisha yake.
Ndugu, kila tunapopiga hatua moja kuingia siku nyingine, ndiyo tunazidi kusogelea ile siku ya Bwana.
Ninaposema siku ya Bwana simaanishi siku ya jumamosi au siku ya jumapili, hapana; siku ya Bwana tunayozungumzia hapa ni ile siku ya ghadhabu ya Bwana kwa wanadamu watendao maovu.
Ndugu, usiombe uwepo katika siku hiyo, maana ni siku ya kutisha sana!! Hapa biblia inasema ni siku ya FUJO, na sehemu nyingine anasema ni siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa!.
Isaya 22:5 “Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.
Hiyo siku kuu ya Bwana kulipisa kisasi kwa wouvu imekaribia sana.
Sefania 1:14 Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!
[15]Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,
[16]Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.
[17]Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.
[18]Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.
Siku hizo ndizo za mapatilizo!! Ni siku ya Bwana kupatiliza waovu maovu yao.
Luka 21:22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.
Katika siku hizo waovu wote wataangamizwa na kuharibiwa vibaya na kisha kutupwa katika ziwa la moto.
Isaya 13:6 Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
[7]Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
[8]Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
[9]Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
[10]Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
[11]Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
[12]nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.
Umeona ndugu, ni mambo ya kutisha sana yanakuja, biblia inazidi kutuonya juu ya siku ya Bwana, kwamba sio ya kutamani kabisa.
Amosi 5:18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwani kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.
[19]Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
[20]Je! Siku ya BWANA haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.
Ndugu siku ya Bwana inatisha sana, huwezi kufikiri kwamba utakuwepo au hata yule adui yako atakuwepo. Kumbuka hatuzungumzii jehanumu ya moto, hapana hiyo ni habari nyingine!! hapa tunazungumzia SIKU YA BWANA.
Siku ya ya Bwana inahusisha yale mapigo ya vile vitasa saba kwenye Ufunuo 16. Hebu kwa taratibu soma we mwenyewe uone mambo yanayokuja kuikumba hii dunia.
Biblia imeandika milima na viziwa vitakimbia siku hiyo..
Ufunuo wa Yohana 6:12 Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
[13]na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
[14]Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
[15]Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
[16]wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
[17]Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?
Kumbuka biblia inaposema siku ya Bwana haimaanishi siku kama siku moja!! Hapana, inamaanisha kipindi fulani ambacho Bwana amekitenga kumwaga ghadhabu na hasira yake kwa waovu wote kabla hawajaenda kuhukumiwa ziwa la moto.
Ndugu, chunguza maisha yako angali neema ipo, mambo hayatakuwa hivi siku zote, pale mlango wa neema utakapofungwa kutakuwa hakuna kurudi nyuma itakuwa ni vilio na maombolezo.
Naam, hiyo siku i karibu sana!!
Yoeli 1:15 Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
Yoeli 2:1 Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;
[2]siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.
Ndugu, kimbilia kalvari sasa, tubu dhambi zako, uoshwe kwa damu ya Yesu na upokee Roho Mtakatifu kabla ya hii siku ya kuogovywa haijafika.
Kumbuka adhabu ya hii SIKU YA BWANA, sio jehanamu ya moto, baada ya mapigo hayo ndipo ziwa la moto ziwa la moto litafuata.
Kimbia injili ambazo zinakufanya usifikiri hatma ya maisha yako ya milele badala yake inakupeleka kutazama mambo ya ulimwengu huu. Hii ni roho ya shetani inawapumbaza wengi wafikiri mambo hayo yatakuja kutokea baada ya miaka 2000 mbele, usidanganyike ni uongo wa shetani, ndugu dalili zote zinaonyesha, unabii wote umetimia kwamba tunaishi katika kizazi cha hatari sana.
Ikiwa unataka kumpa Bwana Yesu maisha yako na kugeuka leo tubu mwenyewe moyoni mwako na dhihirisha toba yako kwa kuacha dhambi zote kwa vitendo, maana yake kama ulikuwa ni mlevi UNAACHA ulevi kwa vitendo, kama ni muasherati hivyo hivyo unaacha kampani za waasherati..unafuta namba zao, unafuta na picha zile za ngono unazozitazama, unafuta na miziki yote ya kidunia na yale mavazi yote ya kikahaba kama vimini, suruali, makaptula, nguo za kubana, na mapambo yote (rasta, wigi, mekaups, kucha bandia, lipusticks, wanja, hereni, n.k) unazichoma zote bila kusita sita. Na mambo yote mabaya UNAACHA kwa vitendo kisha unapiga magoti na kusali sala hii..
Sema..
“Bwana Yesu, Leo hii nasogea mbele zako nikiwa mwenye dhambi, natubu makosa yangu yote niliyokukosea, naomba unisamehe, nimeamua kugeuka leo, nisaidie Bwana Yesu, neema yako iwe juu yangu, nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu, asante Bwana Yesu kwa kunisikia na kunisamehe. AMEN! “.
Baada ya kutubu unahitaji kubatizwa, Hivyo basi tafuta kanisa linalobatiza ubatizo sahihi nao ni kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na ni kwa jina la YESU KRISTO, Kwa kufanya hivyo Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu na utakuwa umekamilisha wokovu wako na hivyo hakutakuwepo miongoni mwa waovu watakaoangamizwa katika siku ile.
MUNGU AKUBARIKI.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.