Ufahamu udanganyifu wa shetani,

Siku za Mwisho No Comments

Jina la Bwana Yesu Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana libarikiwe daima.

Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Siku ya leo kwa Neema za Mungu tutazidi kuongeza maarifa ya Neno la Mungu tusije tukachukuliwa na udanganyifu wa yule mwovu katika siku hizi za mwisho ambayo udanganyifu umekuwa mwingi sana.

Ukisoma kile kitabu cha ufunuo sura ya 12 na mstari wa 7 utaona kulikuwa na vita mbinguni ambayo Mikaeli kama malaika wa vita pamoja na malaika wengine  walipigana na shetani ambayo ndiye yule joka, yaani malaika aliyeasi, na mwisho tunaona baada ya kushindwa vita alitupwa huku duniani,

Sasa kumbuka wakati huo mwanadamu bado alikuwa hajaumbwa, hivyo shetani alipotupwa huku duniani, tuseme kazi yake kubwa ilikuwa ni kuzunguka zunguka tu, na hiyo ndio kazi yake kama kipindi kile cha Ayubu.. kwasababu duniani kulikuwa hakuna kitu..

Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Umeona hapo! Biblia inasema HAPO MWANZO.. maana yake dunia iliumbwa miaka kadhaa nyuma kabla ya huu uumbaji ambao tunaona sasahivi, biblia haisemi moja kwa moja muda au miaka ambayo ile dunia ya kwanza ilidumu hadi hii ya pili tuliyopo sasa kuumbwa, labda ni miaka 1000 au maelfu ya miaka hatujui, tunachojua kulingana na biblia ni kwamba Mungu alipoanza kuiumba hii dunia kwa upya..

dunia ilikuwa hali ya UKIWA (usiyokuwa na kitu ila maji tu), kuonyeshwa dunia ya kwanza ilikuwa imeharibiwa na Mungu..Mungu alifuta kila kitu  maji tu ndio ysliyobaki. Sasa kuna uwezekano kabisa kuwa shetani ndiye chanzo cha dunia ya kwanza kufutwa na Mungu kwasababu ya uharibifu alioufanya, maana biblia inatuonyesha kuwa kazi ya shetani ni kuua pamoja na kuharibu (Yohana 10:10),

Sasa tukirudi katika hii dunia ambayo sisi tupo, tunaona mwanzo wa uumbaji wa Mungu shetani alianza tena kufanya uharibifu pale alipomdanganya Hawa kula lile tunda ambalo ni kinyume na maagizo ya Mungu, na ndipo hapo tunakuja kuona dunia imeharibika tangu hapo mwanzo mpaka sasa inalewa-lewa kama mlevi kwasababu ya maovu yanayoletwa na ibilisi kupitia wanadamu.

Isaya 24:20 Dunia inalewa -lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala HAITAINUKA TENA.

Umeona hapo! Dunia imechafuka, dhambi imelemea dunia na Mungu anaenda kufuta kama hapo mwanzo na kama tunavyosoma hapo baada hii dunia kuanguka haitainuka tena maana yake hakutakuwepo tena na dunia nyingine kama hii, kwani shetani ambaye ndiye anayeharibu dunia hatakuwepo tena maana baada ya hii dunia shetani atatupwa kwenye ziwa la moto milele pamoja na wafuasi wake wote, baada ya hapo kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya ambayo watu wa Mungu wataishi na Mungu daima.

Swali je utakuwepo huko? au utakuwa umeungana na shetani kule kwenye ziwa la moto!.. kumbuka mambo hayo yapo mbioni kutokea..hivi karibuni tukio kubwa la unyakuo litapita, ambayo watakatifu wote waliolala watasikia sauti ya parapanda na wote watafufuliwa na wataungana na wale walio hai wote kwa pamoja watamlaki Bwana Yesu mawinguni..soma 1Wathesalonike 4:13-17,

Wataenda kwenye karamu ya Mwana-kondoo kwa miaka 7 ambayo huku duniani kutakuwepo na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea toka dunia hii kuumbwa, na baada ya hizo miaka saba watakatifu watakuja na YESU KRISTO akiwa kama MFALME MKUU kuja kuleta utawala wa miaka elfu hapa duniani na baada ya hapo hukumu ya kiti cheupe kwa watu wote itafuata ambayo bahari na kuzimu itawatoa wafu wakubwa kwa wadogo na wote watahukumiwa sawa sawa na matendo yao (Ufunuo 20:11-15),

kumbuka ukifa sasa hivi kwenye dhambi au baada ya unyakuo.. moja kwa moja utapokelewa kuzimu ambapo kuna mateso yasiyoelezeka ambapo huko utasubiria hukumu ya kiti cheupe ambayo itakuja baada ya ile miaka elfu, na baada ya hapo utahukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto.

Ni nini kinakupa kiburi usiache dhambi na kumpokea Bwana Yesu sasa kipindi hiki cha Neema, je! Ni uzima au mali, elimu ya hii dunia iliyoharibika, au nini kinakupa kiburi usimpokee Bwana Yesu sasa, kumbuka utakuja kujutia maisha yako yote pale ambapo hii neema imeondoka au pale ambapo umekufa kwenye dhambi.

Kazi anayoifanya shetani kwasasa ni kudanganya ulimwengu kuwa unyakuo bado sana, hakuna Kuzimu, akizidi kuwadanganya watu waendelee kufurahia maisha ya anasa,  ameenda mbali zaidi akiwadanganya Wanawake waendelee kujifurahisha kwenye mambo maovu ya kujichubua, wanavaa mawigi, hereni, wanaume wanasuka nywele, jambo ambalo ni la ajabu sana, huu ni udanganyifu mkubwa sana wa shetani..

Ndiye aliyemdanganya Hawa!. na siku hizi za mwisho ameongeza udanganyifu, kila siku anakuja na mbinu mpya ili awapate wengi, yupo kila mahali, kanisani anajibadilisha kuwa malaika wa nuru kama maandiko yanavyosemavyo(2Wakorintho 11:14),

kuwa makini sana usimpe ibilisi nafasi, usikubali kudanganywa na mambo au vitu anavyoviachilia kila siku ambavyo vinaonekana vizuri na kutamaanisha macho, wewe kama mwamini sio kila fashion inayotoka ukimbilie, sio kila kitu ukifanye, sio kila kitu ukiamini fuata Neno la Mungu, Wala usiangailie ulimwengu wanafanyaje, usiangailie kanisa lako wanachokiamini.. angalia Neno la Mungu, epuka uongo wa shetani unaofanana na ukweli,

tunza MWILI wako maana ni hekalu la Mungu, usikubali kufuata uongo wa shetani unaohubiri kuwa Mungu anaangalia roho tu, na haangalii mwili; Mungu anaangalia roho na mwili, ndio maana amekuumbia huo mwili, tena anasema itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu na ya kumpendeza (Warumi 12:1-2), Mungu anaangalia sana mwili wako maana ni hekalu la Roho Mtakatifu..

2Wakorintho7:1 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa MWILI na ROHO, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu

Kumbuka tena shetani anatafuta roho za watu wengi aende nao jehanam. Na kama biblia inavyotuonyesha kuwa alivyotupwa duniani kazi yake ni kuudanganya ulimwengu wote..

Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, AUDANGANYAYE ULIMWENGU WOTE; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Umeona hapo! Maana yake hakuna kitu kilichoachwa, hakuna mfumo ulioachwa, ulimwengu wote umedanganywa! Lakini tumaini lipo kwa Yesu Kristo yeye aliye njia, kweli na uzima, huwezi kumkwepa shetani bila kuwa ndani ya Yesu Kristo,

Tubu leo dhambi zako, ukabatiwze ubatizo ulio sahihi upokee Roho Mtakatifu akuongoze na kukulinda na udanganyifu wote wa shetani..

Bwana atusaidie!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *