Unafahamu matumizi sahihi ya Damu ya Yesu Kristo?
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe, Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Kumekuwa na matumizi yasiyokuwa sahihi kwa Wakristo wengi kuhusu damu ya Yesu Kristo huenda kwa kukosa maarifa ya kutosha kuhusu Damu ya Yesu Kristo.
Wakristo wengi wanaitumia damu ya Yesu Kristo katika njia isiyokuwa sahihi hivyo inapelekea watu kukosa matokeo juu ya kile wanachokiomba..
Ni muhimu kufahamu hili kuwa damu ya Yesu Kristo ni Uhai wa Yesu Kristo.. na uhai wa Yesu Kristo ni ukombozi kwetu.
Leo hii utakuta mtoto wa Mungu anaitumia damu ya Yesu Kristo katika mambo yake mbali mbali mfano katika Biashara,vyakula vya mwilini nk..
Utakuta Kristo anasema..”nanyunyiza damu Yesu Kristo katika Familia yangu,nanyunyiza damu ya Yesu Kristo katika Biashara yangu, au navunja madhabahu zote kwa damu ya Yesu Kristo, nawachoma wachawi wote kwa damu ya Yesu Kristo, nateketeza/kuwachoma maadui zangu kwa damu ya Yesu nk”
Wakati mwingine katika kuomba “Mungu Baba kibariki chakula hiki na kitakase kwa damu ya Yesu Kristo nk”
Ndugu ukweli ni kwamba hayo si matumizi sahihi ya damu ya Yesu Kristo ni muhimu sana kuwa na ufahamu juu ya damu ya Yesu Kristo ni nini na kazi yake hasa kubwa ni ipi..?
Mkristo anafukuza wachawi nk kwa damu ya Yesu si matumizi sahihi.. ukiielewa vyema damu ya Yesu Kristo kazi yake ni nini mtazamo wako na maisha yako katika wokovu utaanza kupiga hatua nyingine zaidi..
Sasa katika somo hili tutajifunza kwa undani zaidi juu ya matumizi sahihi na uelewa kwa undani zaidi kuhusu damu ya Yesu Kristo.
Damu ya Yesu Kristo kazi yake ni ipi hasa?
1.Damu ya Yesu Kristo husafisha dhambi.
Kama jinsi maandiko yanavyosema pasipo kumwagika damu hakuna ondoleo la dhambi..maana yake ili dhambi iondoke inahitaji mauti. Ndio maana maandiko yanasema mshahara wa Dhambi ni mauti(Warumi 6:23) maana yake dhambi inadai mauti na mauti hiyo aliichukua Yesu Kristo hivyo pale tunapomuamini yeye Kupitia mauti yake tunapata ondoleo la dhambi.
Waebrania 9:22
“Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.”
Hivyo Yesu Kristo alipokufa msalabani na kumwaga damu yake ili kusafisha dhambi (kuondoa isiwepo kabisa deni ya dhambi) kwa wale wanaomwamini..
1 Yohana 1:7
“bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.”
Hii ni kazi moja wapo ya damu ya Yesu Kristo.
2. Damu ya Yesu huleta wokovu.
Wokovu wa mwanadamu unategemea dhabihu ya Yesu Kristo pale msalabani. Hautegemei matendo nk bali Dhabihu ya Mungu mwenyewe..
Warumi 5:9
“Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.”
Tulistahili kuingia katika hukumu ya milele (ghadhabu ya Mungu kwa sababu ya uasi lakini Yesu Kristo kupitia damu yake basi hakuna hukumu tena juu yetu tulio katika Kristo Yesu.. Haleluya).
3.Damu ya Yesu inatupa ukombozi.
Tunapomwamini Yesu Kristo kwa sababu ya kufa kwa ajiri yetu(kumwaga damu yake) sisi tunapata ukombozi. Utajiuliza ukombozi upi? Kwani tulikuwa wafungwa? Jibu ni ndio mtu yoyote ambaye hajamuamini Yesu Kristo huyo yupo katika utumwa wa pande mbili ni mtumwa wa dhambi na Shetani pia.
Sasa damu ya Kristo Yesu Mwokozi inatuweka sisi mbali na utumwa wa shetani na dhambi pia.
Waefeso 1:7
“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.”
Maana yake tunakuwa hatuko chini ya dhambi tena wala chini ya Shetani bali damu ya Yesu inatuweka huru mbali na dhambi na tunakuwa miliki ya Mungu. Hivyo damu ya Yesu Kristo inatupa ukombozi.
4.Damu ya Yesu Kristo hutufanya kuwa washirika wa agano Jipya.
Tunaagano jipya halijatokea tu, lakini lipo kwa sababu ya damu ya Yesu Kristo. Hivyo kupitia damu yake ilianzisha agano lililo bora kati ya Mungu na Mwanadamu. Na katika hili tuna amani na Mungu wetu na tunaweza kuwasiliana nae na akatusikia saa yoyote na muda wowote maana kaamua kukaa ndani yetu maana yake hatuhitaji tena kuingia hemani nk bali Kristo yupo ndani yetu..
Na yupo ndani yetu kwa sababu ya damu iliyomwagika pale Kalvari.
Luka 22:20
“Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]”
Damu hii ilimwagika kwa ajiri yangu mimi na wewe maandiko yanaendelea kusema…
Waebrania 8:6
“Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.”
5.Damu ya Yesu inatupa ushindi juu ya adui shetani.
Ukweli ni kwamba tusingeweza kumshinda shetani mwanadamu yeyote pasipo Yesu Kristo kumwaga damu yake. Hivyo damu ya Yesu Kristo inatupa sisi mamlaka ya kushinda dhidi ya shetani..
Kwa namna gani unapofahamu Damu ya Kristo kumwagika pale msalabani Bwana alisema “Imekwisha” maana yake Shetani kaangushwa chini.. hivyo si mapepo,majini,wachawi, waganga nk wanaweza kukuangusha la!, Hatumshindi Shetani kwa kusema kwa damu ya Yesu shindwa. La! unaweza kutamka kwa mdomo lakini ukawa huna uelewa wa kutosha juu ya kwa nini damu ya Yesu..
Fahamu kabla ya damu ya Yesu kumwagika shetani alikuwa anatutawala, na baada ya damu kumwagika tunakuwa hatuko chini ya utawala wake tena tunakuwa tuko chini ya utawala mwingine wenye nguvu kuliko ule wa kwanza nao ni wa Yesu Kristo.
Ufunuo wa Yohana 12:11
“Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”
Si kusema tu lakini lazima ufahamu damu ya Yesu Kristo imekupatia ushindi juu ya maadui zako ambao ni Mauti na Shetani..ulifahamu kutoka ndani ya moyo wako kuwa damu ya Yesu Kristo imekupa ushindi pasipo wewe kupigana wala kumwaga damu..
Haleluya ni neema ya ajabu na kubwa ya namna gani tumepewa? Hakika Mungu anatupenda na anajua kutupa kilicho bora..
Hizo tano zitoshe kukupa ufahamu mpana zaidi juu ya damu ya Yesu Kristo katika kutoa pepo tunatumia mamlaka ya jina la Yesu sio damu,, ikiwa ni ulinzi wa nyumba/familia si kwa damu ya Yesu la bali ni kwa mamlaka ya jina la Yesu Kristo nguvu zake zizingile nyumba/familia yako na sio damu ndio ifunike..
Katika Biashara zako kazi nk neema na nguvu za Mungu ndio zinatumika huko na sio damu ya Yesu Kristo..
Hakuna mahali popote katika agano jipya mahali maandiko au watakatifu wa zamani kwamba walikuwa wanatumia damu ya Yesu Kristo katika mambo yote bali jina pekee ndio lilitumia yaani ikijumlisha uweza na mamlaka yaliyo katika Jina la Yesu Kristo..
Mungu akubariki sana na nakuombea Mungu azidi kukupa ufahamu zaidi katika kumjua yeye katika Jina la Yesu Kristo kiu yako kwa Mungu isikate.. Amina
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.