USIUIGE UBAYA

Dhambi No Comments

USIUIGE UBAYA

3Yohana 1:11 “Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.

Kama wana wa Mungu hatupaswi kuiga mambo mabaya kwa watu wa kidunia.

Hutupaswi kuiga uvaaji mbaya, mitindo ya kidunia, anasa, ulevi, uasherati, uhuni, na kanuni za ulimwengu huu.

Warumi 12:1″Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

[2]WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.

Ikiwa umeokoka kweli kweli, fahamu kuwa wewe si wa ulimwengu huu tena, we ni mzao mteule, taifa takatifu la Mungu.

1Petro 2:9 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

Je! wewe unayesoma habari hizi, umefanyika mzao mteule wa taifa takatifu la Mungu?

Kama bado hujampokea Yesu maishani mwako, fahamu kuwa we ni mwana wa ulimwengu huu, na ulimwengu huu na watu wake umewekewa akiba ya kuangamizwa katika maangamizo ya milele.

2Petro 3:6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

[7]Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.”

Hivyo ni heri leo uamue kumpokea YESU ili upewe uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu, mzao mteule. Sawa sawa na Yohana 1:12.

Na kumpokea Yesu sio kusema tu kwa kinywa nimempokea basi. Hapana kumpokea Yesu ni kupokea badiliko la maisha yako yote kuanzia ndani mpaka nje. Ikiwa na maana kama hauna mabadiliko yoyote tangu uliposema nimempokea, fahamu kuwa bado haujamaanisha kumpokea, hata kama unaenda kanisani na kutoa sadaka, hata kama unatumika na Mungu katika viwango vya juu.

Kumpokea Yesu ni kuamua kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha kabisa kabisa, na pia kuacha kanuni na mitindo yote ya kiulimwengu. (Kwa ufupi unaamua kuwa kinyume na ulimwengu huu) na hiyo huna budi kujikana nafsi.

Ikiwa tayari kufanya hivyo na unahitaji huo msaada, basi wasiliana nasi kupitia namba uzionazo chini ya somo hili nasi tutakusaidia bure.

Bwana akubariki.

Maran atha.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *