kutekewa ni nini kulingana na mathayo 22:12

Maswali ya Biblia No Comments

Kutekewa ni kukosa maneno, yaani kukosa jibu la kujibu na siyo kuchotewa maji

Katika Habari hii Bwana Yesu asifiwe alikuwa anazungumzia yule mtu aliyeingia katika harusi kisha akakutwa hana vazi la arusi ndipo akatekewa

Mathayo 22:8 “Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili.

9 Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini.

10 Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.

11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.

12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? NAYE AKATEKEWA”.

Hivyo mtu huyo baada ya kukutwa hana vazi la arusi alipo ulizwa alikosa neno la kujibu ndiyo maana akatolewa nje

Huu ndiyo hualisia ulipo siku ambayo atarudi Bwana Yesu, pale anakapo ona watu walioalikwa katika karamu ya wanakondoo lakini hawana vazi la harusi, ndipo hapo Bwana atakapo uliza, nao watakosa neno la kusema “watatekewa” na hatimaye kutupwa nje

Dini siyo vazi, umaarufu pia siyo vazi, kujulikana kama mtumishi mashuhuri unayefundisha vizuri nako si vazi, lakini utakatifu ndiyo vazi ambalo litamtamtabulisha mtu awezw kuingia karamuni

Kumbukumbu pia utakatifu hauji kwa nguvu zetu mbali unakuja kwa uweza wa Mungu pekee, ikiwa Bado ujaokoka basi ni wakati sasa hili upate vazi litakalo kuruhusu uingie karamuni

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *