Upo karibu na Yesu?
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe Karibu tuyatafakari maneno ya uzima!
Sio Wakristo wote wako karibu na Yesu Kristo au wanaushirika wa karibu naye. Kil Mkristo alieokoka ana Yesu ndani yake(Roho Mtakatifu) lakini si kila Mkristo ana ushirika wa karibu sana na Yesu Kristo.
Kuwa karibu na Yesu Kristo sio jambo ambalo linatokea tu kwa bahati bali ni mchakato na nia/ shauku ya mtu mwenyewe ndani yake.
Ni nini maana ya kuwa karibu na Yesu Kristo? Ni hali ya mwamini kutokuanza kujiona mwenyewe(kujipendeza mwenyewe, kufanya atakalo nk) bali kuanza kumuona Yesu Kristo na kutembea katika mapenzi ya Mungu. Matokeo yake anakuwa sio yeye tena bali Kristo ndani yake.
Mtume Paulo analiweka wazi hili..
Wagalatia 2:20
“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.”
Anasema amesulibiwa na Pamoja na Kristo lakini yupo hai lakini sio kwamba yupo hai yeye kama yeye bali Kristo ndio yuko hai ndani yake..
Maana yake Mtazamo wake,mwenendo wake,ufahamu wake,Matakwa yake nk vyote ninamfanania Kristo. Maana yake nia yake imebadilishwa ndani yake(Warumi 12:2).
Sio Kila Mkristo ana ukaribu au ushirika na Kristo na si Kila Mkristo Kristo yuko hai ndani yake. Na hata uhai alionao si kwa ajiri ya Kristo bali kwa ajiri yake mwenyewe.
Ikiwa upo karibu na Yesu Kristo ni lazima utabadilika tu huwezi kuendelea kuwa vile vile tu tutaona viashiria ambavyo kama unavyo basi bado haupo karibu na Kristo na fanya hima kuwa karibu nae.
Ukiona kila siku unakemewa kuhusu kuvaa vizuri na kustiri mwili wako kila jumapili mchungaji anasisitiza uvae mavazi ya heshima na husikii unachukia na huoni shida yoyote unavyovyaa hivyo dada yangu,kaka yangu jua uko mbali na Kristo.
Kwa sababu kama upo karibu na Kristo Karibu lazima Kristo atakushuhudia tu moyoni mwako kabla hata hujainunua hiyo nguo na kwenda kuvaa.. utaona kabisa hupaswi kuvaa hivyo.
Ukiona unasukumwa sukumwa kwenda ibadani mikesha nk jua kabisa haupo karibu na Kristo au huna ushirika wa karibu nae maana kama unaushirika nae wa Karibu sana huhitaji kukumbushwa hata inapofika jumamos kabla ya jumapili utajua kesho ni ibadani na utaanza kujiandaa usiku na kuuweka ufahamu wako sawa kwa ajili ya ibada.
Ukiona unasongwa na anasa za ulimwengu huu muda mwingi unautumia social media,kuangalia tamthilia, kupiga soga vijiweni,mipira nk
Huna ushirika wa karibu na Yesu Kristo kwa sababu hivyo vitu unavyoviona ni vya kawaida Kristo atakwambia hivi vitu sio acha mara moja. Utaelewa si sahihi wala hatakwambia mtu acha hiki acha kile ni wewe mwenyewe tu utaacha.
Nakumbuka nilikuwa mshabiki wa mpira, msikilizaji mzuri wa nyimbo za kidunia na nina Yesu Ndani yangu ninaona kawaida tu.
Lakini kadiri ninavyomsogelea Mungu Kristo ananionyesha mapungufu na ubaya wa vile vitu, hakuna mtu alinishawishi kuacha, ila ushawishi wa Roho Mtakatifu na baada ya kuona mapungufu/jinsi yale mambo yanavyoniharibu ndani nikaacha kwa neema za Mungu (Epuka kushawishiwa kuacha kitu kama hujaona madhara yake.. maana ni rahisi kukirudia muda wowote maana ndani yako hujaona shida yoyote. )
Lazima utaanza kutambua hata kasoro zilipo kwenye maisha yako na kuanza kujirekebisha kwa sababu Kristo yuko karibu..
Petro alipokuwa karibu na Yesu mwanzo kabisa pale Yesu hakumwambia “ wewe Petro una dhambi?” Lakini Petro anasema “ondoka kwangu mimi ni mwenye dhambi..”
Kumbuka wakati huu Petro hajui kama Yesu ndio mkombozi wa ulimwengu.
Luka 5:8
“ Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.”
Hivyo Kristo anapokuwa karibu na wewe lazima utatambua mahali palipo na kasoro na ukianza kupafanyia kazi Kristo atakusaidia na utazidi kumkaribia zaidi mwisho utakuwa kama yeye.
Hivyo anza leo kupiga hatua za kuwa karibu na Yesu Kristo, yuko ndani yako hata sasa unachotakiwa kufahamu anatamani sana kuwa na ushirika na wewe. Anza kusoma biblia (itakupa mwongozo wote unatakiwa kuwa vipi na ili umsogelee yeye unatakiwa ufanye nini) kuwa mtu wa kuomba(hii itakusaidia kupata nguvu ya kuendelea mbele na kuyakumbuka uliyojifunza kwenye biblia na maombi yanaamsha nguvu ndani yako.)
Tendea kazi(anza kutendea kazi kwa kuomba msaada wa Mungu na usikate tamaa unapoona pana ugumu jua kabisa kuna ushindi mkubwa mbele yako lifahamu hili “ *sio asili yako kushindwa baada ya kuzaliwa mara ya pili,”* Haleluya!!)
Omba maombi haya mafupi.
“ Eh Bwana Yesu ninakushukuru kwa ajili ya Neno lako, ninahitaji kuwa na ushirika na wewe wa karibu,niwe karibu na wewe,najua ni mchakato kuwa na mahusiano na wewe lakini ninaamini kuanzia leo nimeanza ushirika wa karibu na wewe nisiishi kwa ajili yangu bali kwa ajiri yako ninaomba nikiamini ni katika Jina lako Takatifu Yesu Kristo Amina”
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano:0613079530
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.