LAKINI SASA YAWEKENI MBALI NANYI HAYA YOTE.
Wakolosai 3: 8 Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.
[9]Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;
Biblia imetuhasa tuweke mbali mambo hayo yote yaliyotajwa hapo juu; yaani hasira, ghadhabu, uovu, matukano, matusi vivywani mwenu. Utaona tena yametajwa na mengine katika..
1 Petro 2:1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
Haya ni mambo tisa ambayo sisi kama watakatifu wa Mungu hatuna budi kuweka mbali kabisa mambo hayo..na mengine mengi tu ambayo hayajatajwa hapo.
Kumbuka hayo mambo ni sisi wenyewe tunapaswa kuweka mbali na sio kutafuta msaada kwingineko. Msaada wa Mungu unakuja pale ampapo sisi tumedhamiria kwanza kupiga hatua.
Na hapo biblia haijalenga watu wa kidunia wasiomjua Mungu kabisa, kwani hao siku zote wanaishi katika hayo maisha ya dhambi. (Kwahiyo hao wanahitaji neema wasikie Injili watubu, na ndivyo wakae mbali na mambo hayo). Kwahiyo hapa Mtume Paulo kwa uweza wa Roho anawaandikia watakatifu walioko Kolosai waweke mbali mambo hayo yote…na sisi pia tunaambiwa hivyo hivyo.
Sasa tutawezaje kuweka mbali mambo hayo katika mazingira tunayoyaishi.
Jibu ni kwa kuomba na kusoma biblia pamoja na kukaa mbali vyanzo vya uovu, mfano vijiweni, mabarazani pa wenye mizahaa, makundi mabaya, n.k
Mkristo ambaye sio mwombaji.. hawezi kushindana na dhambi..atashindwa tu! Haijalishi amekomaa kiasi gani kwenye wokovu. Hasira, wivu, matusi yatamshinda tu. Kwahiyo maombi ni muhimu sana kwa mkristo aliyeokoka kweli kweli.
Je! Umeokoka kweli kweli au una jina la kuwa mkristo lakini ni mtu wa kidunia. Unaweza ukadanganya kwa nje lakini huwezi kudanganya moyo wako, labda moyo wako ukudanganye.
Kama hujaokoka, ni heri leo ukaamua kuchukua uamuzi wa kubadilika na kuacha maisha ya dhambi na ulimwengu..ukampokea Yesu kabla hujafika hatima ya safari yako hapa duniani.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.