Jina la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo lisifiwe,
karibu tujifunze maneno ya uzima
tusome
Mathayo 9:2
[2]Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
tunaona katika habari hii bwana Yesu anamwambia yule mgonjwa ajipe moyo mkuu
hivyo hakumwita mkuu bali alimwambia ajipe “moyo mkuu” kwa maana Bwana Yesu ndiye Mkuu wa wakuu hakuna alie mkuu zaidi ya Bwana Yesu yaani Mungu.
Hivyo jibu ni hapana atupaswi kumwita mtu mkuu wala kuitana sisi kwa sisi wakuu..
kwa maana anaestahili ukuu na kuheshimiwa ni mmoja tu naye ni Mungu wetu Yesu Kristo.
lakini unaweza kujiuliza nini maana ya neno “jipe moyo mkuu” au Moyo mkuu kama lilivyotumika mara nyingi kwenye biblia?
tusome baadhi ya maandiko Yafuatayo….
Mathayo 9:22
[22]Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.
.
2 Wakorintho 5:8
[8]Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.Matendo ya Mitume 27:22
Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu.
2 Mambo ya Nyakati 32:7
[7]Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye;
hio ni baadhi ya mistari katika biblia yenye maneno hayo ipo mingine mingi zaidi inayozungumzia moyo mkuu..
jipe moyo mkuu au kua na moyo mkuu maana yake ni kua na ujasiri wa imani katika Kristo Yesu, kubaki au kuendelea kuamini mpaka mwisho, pia kuto kukata tamaa na kua na tumaini katika Kristo Yesu. maana unakua na uhakika na yule unaemtegemea au unaemuamini kwamba ni uhakika kua utapokea majibu yako.
ukisoma
2 Mambo ya Nyakati 32:7
[7]Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye;
unaona apo ni kama wanaambiwa kuweni na ujasiri katika Mungu wala msikate tamaa maana yupo mkuu atakae watetea..
hivyo ata wewe ndugu yangu jipe moyo mkuu katika Kristo yesu..
weka tumaini lako katika yesu Kristo kwa maana ni lazima atakushindia au atakutoa katika changamoto yako yoyote ile..ameni
Ubarikiwe na bwana Yesu.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.