Nakusalimu katika jina la Mkuu wa uzima Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Kuoka ni Mwanzo wa kuwa na mahusiano mazuri na Mungu, lakini jambo la kusikitisha watu wengi wanaishia kuokoka peke yake tu. Na wanashindwa kuwa na mahusiano ya karibu na Bwana Yesu.
“Shetani haogopi wokovu ulionao, Shetani anaogopa mahusiano yako wewe na Mungu”
Wakristo wengi wanafikiri kutamka jina la Yesu tu adui hawezi kuwafanya chochote lakini sivyo hivyo kabisa.
Shetani haogopi jina la Yesu unalolitamka kila siku, anaogopa na hawezi kukusogelea ikiwa unamahusiano ya karibu na ya ndani sana na huyo mwenye hilo jina.
Kuna kisa kimoja katika maandiko tunakifahamu lakini leo naomba tukakiangalie kwa kina zaidi.
Matendo ya Mitume 19
13 Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
14 Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo.
15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Baadhi watu huwa wanafikiri hawa walikuwa ni waganga au wachawi lakini sivyo. Hawa watu hawakuwa waganga wala wachawi ukisoma vizuri pale walikua ni wana wa Kuhani mkuu huko Efeso walikua ni Wayahudi na hiyo Skewa alikuwa kuhani mkuu, hakuwa anatambulika Jerusalemu ila Efeso.
Si kwamba hawa wana wa Skewa ilikuwa mara yao kufanya hivyo ilikuwa ni tabia ya Wayahudi wengi waliokuwa huko Soma mstari hapo juu kabisa utaliona hilo.
Walikuwa wanatoa pepo pasipo kuwa na mahusiano na Bwama Yesu yaani walikuwa wakitumia mapokeo ya kidini au desturi za kidini yaani kama wakatoriki wanavyo bariki maji na hayo kwa kufikiri kwamba maji yale ni tiba tosha hata mtu aliepagawa na pepo wanaweza kumwagia maji hayo pepo akatoka jambo ambalo ni si kweli.
Hivyo hawa walikuwa ni watu wa kidini (watu wenye dini na mapokeo lakini hawana Yesu au hawana mahusiano ya ndani na Yesu Kristo).
Na siku hiyo walifanya jambo hilo kwa mapokeo ya kidini/kidhehebu lakini maandiko yanasema yule pepo aliwajibu kaa ukali na hasira maneno haya…
“Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?”
Ukisoma katika tafasiri za kiingereza kama (TPT the passion Translation) anasema
“I know about Jesus, and I recognize Paul, but who do you think you are?”
Maana yake ni “Ninajua kuhusu Yesu, na namtambua Paulo, lakini ninyi mnajidhania kuwa nani?”
Au kwa namna nyingine unaweza kusema “mnafikiri ninyi ni wakina nani hata mnitoe?”
Na tunaona kilichowatokea ni kitu gani pepo yule aliwapiga na kuwajeruhi sana.
Ni jambo gani tunapaswa kujifunza hapa kama Wakristo?
Ni lazima tufahamu mamlaka ya kweli ya kutamka jambo na likatokea yanakuja kupitia mahusiano yetu ya Karibu kati yetu sisi na Mungu. Sio kutumia kanuni fulani za kidini huenda ni ukatoliki,ulokole,usabato nk.
Mapepo yanafahamu kwa kina mahusiano yetu kati yetu sisi na Mungu.
Na mwenye wajibu wa kuimarisha mahusiano hayo ni wewe kwa kuongeza bidii katika kuhakikisha unamkaribia Mungu.
Kwa sababu kadili unavyozidi kumkaribia Mungu ndio unavyozidi kufanana nae ndio unavyo zidi kuwa na nguvu nyingi za rohoni.
Ni sawa sawa na unavyoukaribia moto kadili unavyozidi kumkaribia ndio joto linapozidi kuongezeka zaidi, moto haukusogelei mwenye wajibu huo ni wewe.
2 Wakorintho 3:18
“Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Unaona hapo? Anasema “tunabadilika” sio tutabadilika maana yake jambo la sisi kumfanania Mungu utukufu wake,uweza wake na nguvu zake inahitaji bidii yako.
Wekeza muda wako kwenye maombi na kusoma neno mambo haya yamekuwa mazito kwa Wakristo wengi karibia asilimia 60 ya Wakristo ni wazito kufanya mambo haya.
Na ndio mambo pekee yanayombadilisha mwamini hakuna namna utamkaribia Mungu au kuwa na mahusiano ya ndani na Mungu nje na Neno na maombi hakuna njia ya mkato.
Ukuwaji wa kiroho ni safari ambayo kila Mkristo lazima afanye hivyo hakuna mkato.
Leo hii huwezi kutoa hata pepo au kujisimamia katika mambo ya Kiroho na unatalajia au unataka Kumfahamu Mungu kaa kina? Mahusiano ya karibu na Mungu yanatengenezwa hayaji kama bahati mbaya ni matokeo ya kukaa uweponi mwa Mungu kwa muda mrefu kama wakina Paulo, Musa nk.
Usifurahie Upemtecoste,ukatoliki,usabato vyote hivi havitakua na msaada kwako kama hutafanikiwa kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu. Tamanio langu kila siku ni kutamani kumjua sana Mungu niwe na mahusiano nae ya karibu sana nizidi kumuelewa sijafika. Bado nakaza mwendo.
Nakuombea kwa jina la Yesu kiu hii ndani yako na tamanio hili lizidi kuumbika zaidi ndani yako.
Kwa neema za Mungu wakati mwingine tutajifunza namna ya kuimarisha mahusiano yako na Mungu.
Ubarikiwe sana.
@Nuru ya upendo.
Contacts 0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.