Neno Maavya ni nini kibiblia ?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu asifiwe nakusalimu kupitia Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu katika kujifunza

Neno hili Maavya ni neno au tunaweza kusema kwa lugha nyepesi kuwa ni cheo cha mtu, mfano mama, baba, mjomba nk.. kwahiyo maana halisi ya neno hili limaanisha ” mama mkwe”

Neno hili tunalipata katika kitabu cha

Mika 7:6 “Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na MAVYAAYE; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.

7 Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia”.

Katika kifungu hiki, kinaeleza wazi kuwa adui wa mtu atoki mbali, anatoka hapo hapo ulipo, ndiyo maana hapo maandiko yanasema adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake

Jambo hili hata Bwana Yesu, alilieleza wazi katika

Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.

Haswa mambo haya huwa yanatokea pale tu , inapogundulika mmoja anatembea katika njia ambayo familia au watu wake hawatembei katika njia hiyo, mfano inatokea katika familia anaokoka mtu mmoja  anakubari kuacha mambo yote ya ulimwengu huu, mtu kama huyu kiuhalisia anakuwa ametangaza vita kati ya ndugu zake, ndiyo jambo hili Mungu alifafahamu toka zamani ndiyo maana amelieza vizuri ili mwamini anapoliona jambo hili linatokea asiteteleke

Hivyo unapoona hali kama hizi zinatokea baada ya kupokea wokovu, kutengwa na ndugu, wazazi, marafiki, kufikiwa kazi, isiwe sababu ya wewe kuacha kumtumikia Mungu, neno la Mungu linasema

“Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.”

(Mathayo 10:37)

Kubari kupitia yote, ukijua kabisa hupotezi chochote zaidi ipo thawabu kubwa mbeleni ambayo Mungu ametuandalia

Mathayo 10:22

[22]Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

Bwana Yesu akubariki..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *