SIKU YA PARAPANDA KULIA NA WAFU KUFUFULIWA.

Siku za Mwisho No Comments

 

SIKU YA PARAPANDA KULIA NA WAFU KUFUFULIWA.

1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

[52]kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; MAANA PARAPANDA ITALIA, NA WAFU WATAFUFULIWA, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.

Siku moja inapopita, ndivyo tunavyoikaribia ile siku kuu ya kwenda mbinguni, siku ile ya Parapanda kulia, ambapo watakatifu wote duniani wataisikia, hakika itasikiwa na wao tu, na sio kila mtu duniani kama wengi wetu tunavyodhani…Watu wenye dhambi wakati huo hawataisikia parapanda hiyo hata chembe..

Siku hiyo pengine itakuwa ni asubuhi kwa upande wetu, au jioni au usiku wa manane ukiwa umelala.. Kama wewe ni mtakatifu utasikia sauti nzuri ya shangwe, ikiambatana na parapanda ya Mungu, na wale wafu waliokufa katika Kristo, wao nao pia wataisikia kutoka kule makaburini, na kufufuka na kuanza kutembea duniani, na wewe utawaona, halafu ghafla, tutaliona jeshi kubwa la malaika likitokea, likiambatana na Bwana, na wakati huo huo ghafla tutaona miili yetu ikibadilishwa kutoka katika miili hii ya unyonge ya mauti na kuwa miili ya utukufu, wakati hilo likuwa linaendelea katika kipindi kifupi sana cha kufumba na kufumbua tutajikuta mawinguni na Bwana YESU, huo ndio wakati tutaenda naye kule mbinguni kula naye ile karamu ya mwana kondoo aliyokwenda kutuandalia miaka 2000 iliyopita.

1Wathesalonike 4:16 “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.

Unaweza kudhani jambo hilo ni bado sana, lakini nataka nikuambie mimi na wewe tunaishi katika yale majira ya kuja kwa Bwana mara ya pili. Dalili zote zinaonyesha, Angalia manabii wa uongo waliosagaa kila kona ya dunia, angalia milipuko ya magonjwa mfano wa Tauni (Corona) yaliyotabiriwa na Bwana Yesu yakitokea ulimwenguni (Luka 21:11)..Hiyo ni dalili ya kwamba tupo ukingoni mwa wakati kuliko tunavyoweza kudhani, angalia tena kuchipuka kwa taifa la Israeli, yaani mtini, ndio kunathibitisha kabisa wakati wa majira ya mataifa(yaani mimi na wewe) tupo ukingoni.

Ndugu yangu jiulize, Yesu akirudi leo utakuwa katika upande upi? Na injili zote hizi ulizosikia utajitetea vipi siku ile kusema hujaambiwa? Ishara zote hizi za siku za mwisho utajitetea vipi siku ile mbele za Mungu? Mungu ni mwingi wa rehema lakini pia ana ghadhabu nyingi.

Kama hujaokoka, basi huu ndio wakati wako wa kuyatengeneza mambo yako na Kristo, ili kusudi kwamba hata ikitokea paraparanda italia leo usiku basi uwe na uhakika kuwa na wewe utakwenda kumlaki mawinguni. Unachopaswa kufanya ni kukusudia tu kumkaribisha Yesu maishani mwako, kwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, na kuwa tayari kuyaanza Maisha mapya ya wokovu.

Kama utamaanisha kufanya hivyo ni ahadi yake kuwa atakuja ndani yako na wewe kuanzia huo wakati utaanza kuona badiliko kubwa ndani yako, hivyo kama upo tayari kufanya hivyo sasa,

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuidhibitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana.

Maran atha.

Kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *