YEYE AJAYE ANAKUJA UPESI

Siku za Mwisho No Comments

YEYE AJAYE ANAKUJA UPESI

Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, YEYE AJAYE ATAKUJA, wala hatakawia”.

Angalia muda unavyokimbia, angalia majira yanavyobadilika, angalia maasi yanavyoongezeka kwa kasi.. Je! yote haya unajua ni ishara ya nini?..Si ya kitu kingine bali ya YEYE AJAYE!!.. Ndio! Yupo mmoja anayekuja! na yupo karibu sana.. huyo sio mwingine zaidi ya YESU KRISTO MFALME WA WAFALME.

>Jiulize!…Utajisikiaje siku umeamka asubuhi unajiandaa kwenda kazini, halafu ghafla unapokea taarifa za kuwa KRISTO kashawachukua watu wake, na wewe umebaki?

> Utajisikiaje umeamka vizuri na unaelekea shuleni, halafu unapata taarifa kuwa unyakuo wa kanisa umepita na wewe umeachwa?

> Utajisikiaje ule muda unapewa taarifa kuwa Kanisa limenyakuliwa na jana tu uliyasikia mahubiri na hukuzingatia??..

>Tafakari utakuwa katika hali gani utakapoanza kutafakari mambo yatakayoupata ulimwengu baada ya hapo?..Kwamaana maandiko yanasema baada ya hapo itakuwa ni dhiki kuu na hukumu kwa wanadamu na mlango wa rehema utakuwa umefungwa!.

Isaya 26:21 “Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao…”.

Wakati huo watu watatamani kuingia katika mlango wa Neema lakini watakuwa wamechelewa…kwasababu mwenye nyumba (YESU) atakuwa ameshasimama na ameufunga mlango, hakuna anayeingia wala anayetoka..

Luka 13:23 “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba WENGI WATATAKA KUINGIA, WASIWEZE.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.

Kwanini leo usijitahidi kuingia katika mlango ulio mwembaba???… hao marafiki watakusaidia nini siku ile au watakushauri nini utakapoukosa unyakuo?.. hizo mali zitakutetea vipi wakati huo?… hizo fasheni za kidunia na huo urembo utakupa kibali gani nyakati hizo?… Kumbuka YEYE AJAYE, ANAKUJA WALA HATAKAWIA!!

Ni heri ukayasalimisha maisha yako kwa YESU leo, maana hizi ni nyakati za hatari!.. na muda wowote parapanda inalia!.

Ufunuo 22:20 “Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu”

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushe

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *