Umepandwa kandokando ya vijito vya maji.?.
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Zaburi 1
1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Kama Mkristo ni muhimu sana kufahamu kuwa sisi sote tunafananishwa na mti, na mti unaweza ukastawi vizuri au usisitawi kutokana na mahali ulipo pandwa.
Hivyo hivyo na sisi wa Kristo katika Roho kuna Mkristo ambae amestawi vizuri katika roho na ambae hajastawi vizuri katika Roho. Kutokana na mahali alipo na yeye anamakusudio ya kustawi au la!
Sasa mtu ambae anastawi katika roho ni mtu wa namna gani ambae maandiko yanasema “ Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”
Huyu mtu ili afananishwe na mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji(sio kijito bali vijito maana yake ni vingi, kikikauka hikiz vingine vitaendelea kustawisha) .
Ni mtu asiyekwenda katika shauri la wasio haki yaani asiyekwenda katika mipango, Mikakati mashauri ya watu wasio haki yaani waovu ambaye yeye hakubaliani na mambo yasiyokuwa ya haki bali amesimama katika haki yaani neno la Mungu. Ikiwa yuko kazini linatokea dili la wizi au ganji lakini yeye hashiriki katika hilo hata kama ni dili lenye faida kubwa.
Hata kama atashawishiwa na bosi wake au na mtu yeyote juu ya mipango hiyo basi hatakubaliana nayo wala kuchukuliana nayo.
Vivyo hivyo na katika nyanja zingine zote ikiwa atashauriwa na ndugu, marafiki kwenda sehemu zisizofaa au zisizomtukuza Mungu basi yeye anakuwa kinyume.
Yaani kifupi ni mtu anaekwenda kinyume na mifumo ya ulimwengu huu, ni mtu mwenye mipaka na kiasi.
Na ni mtu asiyeketi barazani/mahali pa watu wenye mizaha anajiepua na kuwaambia ukweli hawatakiwi kufanya hivyo ikiwa ni mtumishi wa Mungu si mwenye mizaha hata anapokuwa madhabahuni.
(Leo hii watumishi wengi wanasimama madhabahuni wanadhubutu kufanya mizaha mbele ya kanisa wakati mwingine wanazungumza maswala ya mipira kabisa Sijui simba na yanga mara “leo hamtoki tunawanyoosha nk” sehemu ambayo hatakiwi kusema maneno hayo na hata kinywa chake tu hakitakiwi kunena hivyo.)
Mkristo anamaneno ya mizaha hata anapokuwa kazini kinywa chake badala ya kumtukuza Bwana Yesu ni stori tu za mipira, kuwatania wengine nk ndugu jua kabisa katika roho hutastawi.
Ili uweze kustawi ni lazima uwe mtu wa namna hii.. ni lazima Sheria ya Bwana au maagizo yaani kuanzia kwenye eneo la mtazamo wako,maelekezo kutoka kwa Mungu unatii, kutafakari kila siku neno la Mungu kwa kadiri Mungu anavyokupa neema ya kuiona siku basi usiruhusu ipite bila kutafakari neno la Mungu.
Yaani Soma kisha pata muda wa kutafakari, na kuomba Bwana akuwezeshe kuyashika/kuyatendea kazi yote ambayo amekufundisha katika tafakari yako kisha mfundishe pia na mwingine.
Ukifanya hivyo maandiko yanasema ni lazima utasitawi tu.
Japokuwa unaweza kuona mbona unajibidiisha sana katika Mungu lakini hakuna kitu chochote ndugu yangu nikutie moyo endelea na kuwa mvumilivu utavuna kile unachokipanda.. Haleluya.
Sasa ili kuelewa vizuri Soma kwa makini sentensi hii kuna jambo kubwa hapa utalipata na liinginze ndani ya moyo ago na uwe hivyo siku zote tafakari kwa kina andiko hili anasema…
Zaburi 1:3
“Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”
Unaona hapo anasema “….. Uzaao matunda yake kwa MAJIRA YAKE…”
kwa nini kwa majira yake? Tafakari leo hii miti yote inayotoa matunda ikiwa ni maembe,machungwa nk utaona hii miti haitoi toi tu matunda muda wowote lakini kuna vipindi na nyakati miti hii hutoa matunda pale msimu wake unapofika wala hauhitaji kujilazimisha lakini automatikali tu unatoa wenyewe.
Hata kama utatunzwa vipi hauwezi kutoa matunda kabla ya msimu wake.
Maana yake vivyo hivyo kwetu sisi watakatifu wewe endelea kukaa katika neno la Mungu maadamu unaona ndani yako hujamuacha Mungu na huoni matokeo ndugu Wakati utafika na hutatumia nguvu kabisa kutoa matunda utajikuta kila unalolifanya litafanikiwa maandiko yanasema hivyo.
Litafanikiwa kwa nini kwa sababu umekaa katika sheria ya Mungu unaishi maisha ya haki,utii, na utakatifu songa mbele maisha ya utakatifu na haki ni kibali kikubwa sana rohoni cha kufungua mambo mengi sana na kukupa nguvu na mamlaka makubwa sana rohoni.
Utakuwa ni Kristo duniani lolote utakaloliomba kwa Mungu itakuwa rahisi kupokea kwa sababu ya maisha unayoyaishi yanakupa kibali mbele za Mungu.
Yatakufanya uzidi kumkaribia zaidi Mungu na kuingia katika moyo wa Mungu kweli kweli.
Utakatifu ni gharama ambayo inakupasa uingie ili uweze kumuona Mungu kwa viwango vya juu zaidi.
Hivyo sisi ni miti mizuri iliopandwa katika shamba la Mungu mbegu iliyoko ndani yetu yaani neno la Mungu sisi ni kuendelea kulishika na kulitunza tu lenyewe litatoa matunda kwa wakati wake kadiri tunavyozudi kulitunza.
Zaburi 52:8
“Bali mimi ni kama mzeituni Umeao katika nyumba ya Mungu. Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.”
Shika sana ulichonacho Bwana Yesu anarudi upesi kukupa thawabu yako. Acha maisha ya kujifurahisha dhambini kataa kuanzia leo sema mimi nitakuwa Mtakatifu kama Baba yangu alivyo Mtakatifu (Mathayo 5:48).
Kuwa mvumilivu unaona kama hupigi hatua au unajitahidi huoni kitu Amini Mungu yupo pamoja na wewe ndani yako anakusaidia tii na kubali kuishi maisha matakatifu.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano 0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.