Bali utafuteni kwanza ufalme wake.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakri maneno ya uzima ya mwokozi wetu.
Bwana Yesu aliwaambia maneno haya wanafunzi wake wale ambao tayari walikuwa wamekubali kumfata. Hakuwa anazungumza na wapagani.
Kuna waliomuelewa anamaanishha nini na kuna wale ambao hawakumuelewa alikuwa anamaanisha nini.
kama Yule kijana aliambiwa na Bwana Yesu akauze vyote awape masikini kisha amfuate lakni aliondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Tusome kisha tujifunze jambo hapa.
Mathayo 6:31-34 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
[32] Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua yakuwa mnahitaji hayo yote.
[33] Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
[34] Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”
Mstari huu nimeanza kusikia muda mrefu sana hasa kipindi nimepata neema ya wokovu kutoka kwa mwokozi wangu Yesu Kristo. Lakini sikuwahi kuuelewa vizuri ijapokuwa nilikuwa mpaka nawahubiria watu wautafute kwanza ufalme wa Mungu lakini sikuwahi kufahamu kwa kina siri iliyojificha katika mstari huu.. na baada ya kuijua siri hii imenipa nguvu sana na kubadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa sana. Atukuzwe Bwana Yesu Kristo.
Sasa unaona hapo Bwana Yesu anaanza kwa kuwaambia “ Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?”
Alijua kabisa watoto wake yaani sisi tuliomuamini yeye tutaanza kuwaza na kusumbuka katika mambo mengi tutaanza kufikiri tutakula nini ikiwa na maana hakuna fedha,wala tutaishije ni kutokana na hali za maisha tutakazozipitia kwa kitambo kidogo tu.
Maana yake tusihamishe mawazo yetu,fikra,akili zetu na kuanza kufikiria mambo ya mwilini na mwishowe tukajikuta tunatoka katika kusudi la Mungu au mpango wa Mungu. Kumbuka haya mambo haambiwi mtu aliye nje na Yesu Kristo bali wewe na mimi ndio tunaambiwa haya ili yatusaidie.
Anaendelea kusema hata watu wa mataifa yaani wasioamii nao wanayatafuta hayo na kuyahangakia sana yaani wamekubali kuuza hata nafsi zao kwa sababu ya hayo mambo ya mwilini.
Ndio hapo inabidi tuwe na tofauti kati ya sisi tuliookoka na wale ambao hawajaokoka.
Asiyeokoka anawaza pesa tu hana muda na kumtafuta Mungu lakini mtoto wa Mungu inafikia hatua haendi hata kanisani kwa sababu hali ni ngumu anakwenda kufungua biashara yake siku ya jumapili. Tunawakristo wengi sana katika kizazi hiki ambao hatuujui uweza na nguvu za Mungu mimi zamani pia niwahi fikiri hivyo.
Nilikuwa nasema “sasa niutafute ufalme wake tu yaani niache kwenda kutafuta pesa nitaishije? Yaani muda mwingi niuwekeze kwa Mungu nitakula nini? Nitavaa nini,nitakamilisha mipango yangu lini? Na umri unazdi kwenda? Nimejiwekea malengo mwezi au mwaka Fulani nitimize kitu fulani sasa nisipopambana yatatimiaje nk”
Hivyo nilikuwa nawaza mambo mengi sana sana. Najikuta napunguza nguvu ya kumtafuta Mungu japo mstari huu nilikuwa naufahamu lakini sio katika usahihi wote.
Na katika nyakati hizi za mwisho wakristo wengi wananjaa ya mafanikio ya mwilini kuliko mafanikio ya rohoni.
jambo ambalo ni baya sana maana utaanza kutaabika kama watu wa ulimwengu huu ilihali wewe umebarikiwa kwa baraka zote za mwilini na rohoni kupitia Yesu Kristo.
Si vibaya kuwa na njaa na kiu ya mafanikio ya mwilini lakini haitakiwi njaa na mafanikio ya mwilini kuzudi njaa ya mafanikio ya rohoni.
“ kwa sababu rohoni pakiwa sawa kukiwa kumestawi vizuri lazima matokeo yataonekana tu mwilini”
” mti hata ukiwa kweye ukame mkubwa kiasi gani lakini kama mizizi yake imeenda chini sana kufikia maji juu hautanyauka majani kamwe utaendelea kuwa na majani mazuri na kustawi vizuri tu”
Sasa ni siri gani ipo katika mstari huu…
ambayo kama ukiifahamu itakutia nguvu na wewe
Tusome mstari wa 33 kuna majibu tutayapata hapa.. iko siri ambayo tutaijua hapa.
[33] Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa .
Unaona hapo? Anasema “….. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa ” kuna kitu hapa nataka ukifahamu kwa kina..
Maana yake hayo mengine yote unayoyasumbukia yaani fedha, ndoa, biashara, kazi, nk yako ndani ya ufalme haleluya…..
Maana yake ukifanikiwa kuuteka ufalme wa Mungu yaani kukaa kwa utimilifu ndani yako basi hayo yanayoitwa mengineyo yako ndani ya huo ufalme. Hivyo kazi yako wewe ni kuhakikisha unauteka ufalme wa Mungu ukishafanikiwa kuuteka lazima tu utakuhudumia maana wewe utakuwa mwana wa ufalme je kuna kitu utakosa?
Ndio maana Bwana Yesu anasema..
Mathayo 11:12” angu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”
Wenye nguvu ndio wanaoweza kuuteka ufalme na sio wa nyonge, wenye nguvu zipi sasa? Si za mwilini bali za rohoni na zinatengenezwa haziuzwi wala kupatikana kwa bahati mbaya au bahati na sibu la!. Bali kwa maombi,mifungo,kuifanya kazi ya Mungu, usafi na utakatifu.
Hivyo utafute kwanza ufalme wake fanya kazi ya Mungu jitoe kwa Mungu bila kujihurumia acha yeye akuhurumie na si ujihurumie wewe.
Hayo mengine utayakuta ndani ya ufalme baada ya kuifahamu siri hii imenipa nguvu sana ukiwa na nguvu ndani yako utaweza kuamuru ufalme ukuhudumie maana uko chini yako.
Mungu karuhusu ufalme wake utekwe na watoto wake.
Usiwe mlegevu katika maombi,mifungo,utakatifu,kusoma neno ukifaya haya yote hayo mengineyo utayakuta ndani ya ufalme niyako na ni haki yako kuypata na Mungu ndio anatamani na anataka uyapate.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano: 0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.