Unataka kumuelewa zaidi Mungu?.
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe. Karibu tuyatafakari maneno ya uzima!
Kumuelewa Mungu katika viwango vingine ni jambo rahisi sana. Na wala Mungu hajaweka ugumu fulani katika kumuelewa yeye!
Mungu ameamua kujiweka katika njia rahisi sana kueleweka kiasi kwamba mtu yeyote mwenye nia ya kutaka kumuelewa Mungu basi ni lazima Mungu atajifunua kwake.
Lakini bahati mbaya watu wengi wanatamani kumjua Mungu hata katika maombi yao wanaomba sana Mungu ajifunue kwao.. wengine wanafunga kwa kipindi kirefu kwa ajiri ya kuutafuta uso wa Mungu lakini bado kumekuwa na changamoto kubwa katika kumuelewa..
Wakristo wengi wanamfahamu Mungu katika vifungu vya maandiko tu lakini sio katika ufunuo halisi wa maandiko hayo ndio maana inakuwa ni rahisi kumuombea adui yako apatwe na mabaya na kushindwa kusamehe nk..(utanielewa baadae kwa namna gani).
“Huwezi kuelewa upendo wa Mungu kama hujakaa na kupata utulivu kisha kuanza kutafakari ukimshirikisha Roho Mtakatifu “ utaishia kuwa na Yohana 3:16 tu nk
Leo hii Wakristo wengi sana wanajua vifungu vya maandiko na kutoka mwanzo mpaka ufunuo yaani wamekariri vifungu vya maandiko tu lakini hawaelewi kwa undani zaidi ufunuo mkubwa ulioko nyumba ya maandiko hayo waloyonayo kichwani.
Inakuwa ni rahisi sana kusema “imeandikwa au maandiko yanasema…..” wanatamka juu juu sio katika uzito na uelewa wa ndani wa andiko hilo. Mungu atusaidie sana kulielewa hili..
Sasa ili uweze kumfahamu Mungu kwa undani zaidi inakupasa kufata hatua kadhaa ni chache sana na ipo kuu moja ambayo ukiweza kuifanya hii itakusaidia sana…
1# kutafakari (Tafakari).
Kutafakari ni uwanja mzuri sana wa kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kukufundisha na kumfunua Kristo zaidi.
Hii ni hatua muhimu na ya msingi sana ikikosekana hii ndugu haijalishi utakuwa unasoma biblia kila siku na unaomba kila siku Lakini hutamuelewa Mungu katika viwango vya juu zaidi utaishia kuwa na ufahamu mdogo tu.
Mungu anataka kujifunua kwetu kwa njia hii ya kutafakari kupitia fahamu zetu na kujiuliza maswali sisi kwa sisi(yaani mwenyewe unajiuliza kwa nini ilikuwa hivi? Hapa alikuwa namaanisha nini? Nk) mambo kama haya lazima uwe nayo ..
Maandiko yanaposema Roho Mtakatifu ni Msaidizi na anatupeleka katika kweli yote ni ngumu kutupeleka katika kweli yote ikiwa hatujiulizi maswali na kutaka kujua zaidi ili tushindwe ili yeye achukue nafasi ya kutueleza kwa nini ilikuwa hivyo atakueleza utajikuta mwenyewe unasema “Anha kumbe..”…(itambue nafasi ya Roho Mtakatifu katika maisha yako itakusaidia sana).
Kukariri vifungu vingi vya maandiko ni sawa na mtu mweye bunduki yenye risasi nyingi lakini hajui kuitumia bunduki.. maana yake wala hawezi kufurahia kukaa na ile buduki hata kama itakuwa ni nzuri kiasi gani lakini kama hajui kuitumia mwisho wa siku ataichoka maana haina msaada wowote kwake..
Ndivyo ilivyo leo kwa watoto wa Mungu wengi wamesoma biblia wamemaliza yote wanajua matukio yote yaliyo rekodiwa kwenye biblia lakini hawajui ufunuo na Kristo anataka wajifunze nini kupitia matukio hayo.
Na utakutanana na watoto wa Mungu unapotaka kuwahubiria au kuwafundisha utasikia wanasema “utanidanganya nini kwenye biblia kila kitu nakijua biblia iko kichwani yote nk..” lakini ukweli ni kwamba wamebeba kweli bunduki na hawaelewi hata sehemu ya kuwekea risasi ziikiisha na hawajui bunduki hiyo inauwezo wa kupiga umbali gani na kwa muda gani na imebeba risasi ngapi? Hawajui..
Mungu anamwambia Yoshua..
Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”
Unaona hapo? Kwa nini Mungu asiishie kumwambia tu Yoshua “kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako. ” Mungu alikuwa anaweza kuishia hapo tu lakini anaendelea kumwambia..
“….BALI YATAFAKARI maneno yake MCHANA na USIKU…” Sasa anaambiwa ayatafakari mchana na usiku ili iweje? Kumbe dhumuni kubwa ni ili apate “.. ..kuangalia(kuona/kujifunza) na kutenda sawa sawa na maneno yote….”
Kinyume chake asipofanya hivyo kuangalia(kuona/kujifunza) hataenda sawasawa na jinsi maandiko yanavyotaka.
“Katika kutafakari ndio unapopata nguvu ya kutenda pasipo kutafakari hakuna utendaji.”
Mwizi hawezi kwenda kabla hajatafari kwanza ataibaje? Na vipi akikamatwa atafanyaje kwahiyo anatafakari kila kitu ndio anatekeleza..
Haamki anasema naenda kuiba la!..
Utendeaji kazi wa neno la Mungu unakuwa ni mgumu kwetu kwa sababu hatulitafakari neno..
Tunapofundishwa jumapili mhubiri akishamaliza kufundisha tunafunika daftari wiki ijayo tunataka kuingiza kitu kipya wakati kile kingine hakijaingia..somo likifudishwa jumapili ndio limeisha hivyo mpaka daftari litaisha mtu hujawahi kupitia na kutafakari. Hii ni ajabu na tunataka kumuelewa Mungu ni ngumu.
Wakina Musa wanakaa milimani siku 40 zote anazitumia kutafakari na kuomba..
“Kama vile unavyoyapa mambo mengine nafasi na kuyafakari kwa kina vivyo hivyo na zaidi Mungu anataka nafasi ya wewe kukaa na wewe kupitia kutafakari akufundishe jambo jipya.”
Lakini ajabu tunaweza kuyatafakari mambo yetu kwa kina sana kuliko neno la Mungu hii ni hatari sana.
Watoto wa Mungu hawatafakari maandiko waki imagine/assume wameelewa kumbe sivyo.
Watu waliotembea na Mungu walikuwa na tabia hii sana ya kutafakari..
Mwanzo 24:63“Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.”
Alitoka kwa kusudi kuu moja tu kutafakari na katika kutafakari huko Mungu akampa hitaji lake..
Ukisoma Zaburi Daudi anaanza kwa kusema heri…(yaani amebarikikiwa) mtu afanyaye yote hayo kwa sababu kuu moja..
Zaburi 1:2“Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.”
Anafanya hayo yote kwa sababu sheria ya Bwana ndio inayompendeza na imempendeza kwa kuitafakari kwa kina na kuona anatakiwa asiende katika shauri la watu wasio haki nk..
Lakini leo hii vijana wengi wa Kikristo wanaanguka katika mambo mabaya wanakaa katika vibanda vya mipira na kubishana na kutukanana na watu wa mataifa kwa sababu hawakutaka kuitafakari sheria ya Bwana.
Pasipo kutafakari Mungu hawezi kujifunua kwako kamwe..usiwe mvivu Jenga tabia ya kutafakari neno la Mungu usilisome na kulijua tu kama somo la historia au uraia. Maana hilo ni uzima wako.
Kadiri Mungu atakavyotupa neema tutazidi kuangalia hatua nyingine.
Mungu akubariki sana.
@Nuru ya Upendo.
Mawasiliano: 0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.