Je! Utoaji wako unamgusa Mungu?

Biblia kwa kina No Comments

Je! Utoaji wako unamgusa Mungu?

SEHEMU YA 03.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu katika mwendelezo wa somo hili sehemu ya tatu ikiwa hukupata sehemu ya kwanza na yapili unaweza wasiliana nasi ili kupata masomo hayo.

Katika sehemu ya pili tunaona kanuni ya pili ambayo ni upendo “hatutoi kwa sababu tunavyovingi vya kutoa bali tunatoa kwa sabahu ya upendo” 

Katika sehemu hii tutakwenda kuangalia kanuni ya tatu ambayo ni muhimu sana kuifahamu.

3. Kanuni ya kuchagua

Kitu pekee kinachomtofautisha mwanadamu na viumbe vingine karibu vyote ni uwezo wa kuchagua. Mungu alimuumbia mwanadamu uwezo wa kuchagua.

Ikiwa na maana Mungu hakutaka kabisa kumtawala mwanadamu bali alitaka mwandamu awe huru kimaamuzi. Hivyo kwa uwezo huu ambao Mungu kauweka ndani ya mwanadamu yupo huru kuchagua chochote anachokitaka ikiwa na maana hata kuchagua kinyume na Mungu.

Kanuni ya kuchagua ni kiini cha utoaji unaomgusa Mungu”

Ulivyo ulimwengu leo ni matokeo ya uchaguzi wa mwanadamu vivyo hivyo ulivyo leo ni matokeo ya uchaguzi wako.

Tunaona hata katika Bustani ya Edeni mwanadamu alichagua kula tunda la mti wa ujuzi wa mti wa mema na mabaya, Shetani hakumlazimisha akamuwekea mdomoni la! Bali alishawishiwa ndio akachukua maamuzi alikuwa na uwezo wa kukubali qu kukataa.

Katika kanuni ya kwanza kabisa nilieleza juu ya kanuni ya asili kila kitu kiliumbwa ili kitoe na kwamba kutoa ni kanuni ya asili ya uumbaji wa Mungu.

Lakini tofauti na vitu vingine mwanadamu ili atoe ni lazima achague kutoa au kutokutoa.

Mfano mpapai au muembe nk ukiwa na mapapai au maembe yaliyokomaa hauna uamuzi juu ya matunda yake wenyewe hutoa kwa yoyote anayehitaji. Hivyo ni suala la mhitaji kwenda tu kuchukua matunda yake.

Lakini maembe hayo hayo au mapapai yakiwa mkononi mwa binadamu yeye anauwezo wa kuyafanyia chochote yaani kutoa au kutokutoa na wakati mwingine kama utayataka kutoka kwake basi ni lazima umuombe na anao uamuzi wa kukupa au kutokukupa.

Tafakari mfano huu una mtoto mdogo wa miaka kama 6 au 7 na ukamletea zawadi mfano gari au cake ukampa. Kitendo cha kumpatia zawadi hiyo haimaniishi kwamba ukitaka kumuomba atakupa kwasababu umempa wewe. Anauchaguzi wa kukupa au kutokukupa kabisa haijalishi wewe ndio umenunua na kumpa.

Hii ndio sababu watu wengi sio watoaji si kwamba hawana chakutoa la! Si kwamba hawampendi Mungu la! Bali wamechagua kutokutoa. Mungu akusaidie ulielewe hili..

Hebu tutafakari neno hili kwa ufupi na kwa kina zaidi..

Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Angali hapo anasema “Hata akamtoa” inaonyesha uchaguzi alioufanya Mungu kwetu sisi kufa kwa ajiri yetu. Hebu Jaribu kulitoa hilo neno “hata” halafu isome hiyo sentensi utaona kuna uzito fulani kwenye hilo andiko umepungua.

Hivyo inaonyesha uchaguzi mkubwa uliomgharimu Mungu kuliko uchaguzi wowote Mungu aliowahi kuufanya. HALELUYA.

Halikuwa jambo rahisi Mungu alivitazama vitu vyote mpaka malaika wakuu na watakatifu lakini hakuona katika hao na katika viumbe vyote kitu chenye thamani kubwa cha kukitoa kwa ajiri ya kumkomboa mwanadamu aliemuumba kwa sura na mfano wake. Tafakari vyema hili.

Jaribu kufikiri ni kipi Mungu angeweza kutoa ili kukukomboa na kukupa uzima wa milele? Hakuna utaona hapo kuwa wewe ni wa thamani na unavinasaba vya Mungu ndani yako tofauti na viumbe vingine Haleluya, Haleluya, Haleluya.

Atukuzwe Mungu aliefanya uchaguzi mkuu namna hii amabo umekuwa ukombozi kwetu sisi. Nafikiri sasa taratibu unaanza kuona jinsi kuchagua kulivyona nguvu.

Tumtafakari Ibrahimu hebu Jaribu kufikiri umepata mtoto uzeeni tena kwa machozi na kwa kusubiri kwa kipindi cha miaka 25 ndio unampata halafu unaambiwa ukamtoe sadaka yaani afe.. litafakari hili vyema kwa wewe mwenye mtoto naamini kuna namna unaona uzito wa hili jambo.

Mwanzo 22:3 “Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye na Isaka Mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.”

Ukisoma tangu Mungu anamwambia Ibrahimu jambo la kujifunza hapa tunaona Mungu hakumlazimisha Ibrahimu kumtoa Isaka lakini Ibrahimu alichagua hivyo na Ibrahimu alikuwa na uwezo wa kukubali au kukataa jiweke katika nafasi ya Ibrahimu na una miaka 100 hapo naamini wengi sana wangepishana na Mungu.

“Inahtajika imani ya kuchagua kama tunataka kuwa na utoaji unaomgusa Mungu.”

Ukatafakari mwandishi wa kitabu hiki cha Waebrania kuna jambo analiesema hapa kumaanisha Ibrahimu alitafakari sana mwisho akaamua kuchagua kumtoa akihesabu Mungu anaweza kumfufua..

Waebrania 11:19 “Akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua [Isaka mwanawe] hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.”

Ukirejea mfano wa Tajiri alieambiwa na Bwana Yesu akauze mali zake awape masikini kisha awe mwanafunzi wa 13 wa Bwana lakini hakuchagua kufanya hivyo kumbuka biblia inamuita tajiri maana yake alikuwa na vingi vya kutoa na si kwamba alikuwa hampendi Mungu alikuwa anampenda katika sehemu ndio maana alikuwa akizishika amri tangu utotoni.

Je? Unampenda Mungu? Kama unampenda kweli kwa moyo wako wote utakuwa tayari kutoa vitu unavyovipenda kwa ajiri yake.

Vinginevyo bado hujampenda Mungu kweli kweli kama wakina Musa,Ibrahimu nk.

Mwitikio wako upoje? Inawezekana Mungu amekusemesha kutoa sadaka fulani kwa ajiri ya kazi yake au kwa ajiri ya watumishi wake lakini umekuwa mzito kufanya uchaguzi na kupelekea kupishana na baraka zako nyingi sana.

Fikiri Ibrahimu angechagua kutokumtoa Isaka je? angekuwa baba wa mataifa? Angekuwa baba wa imani? Baraka zote alizobarikiwa je angezipataje kama asingefanya vile? Kuna viwango Mungu anataka akupeleke lakini umekuwa mzito kuachilia vitu vyako kwa ajiri ya Mungu ndio maana imekuwa ngumu kwako.

Katika kuchagua kutoa kuna baraka nyingi sana zipo kwa ajiri yako..

Mama mmoja alikuwa na tatizo ambalo alizunguka sehemu nyingi sana Kwa muda mrefu kuombewa siku moja akiwa anaenda ibadani kama ilivyo desturi yake akasikia msukomo ndani yake wa kutoa zawadi kwa mama mchungaji baada ya kutoa sadaka/zawadi ile mama mchungaji alikuwa akimshukuru sana Mungu na katika shukrani zile mama yule alieleta zawadi kule kule akaanguka chini na akafunguliwa tatizo alilokuwa nalo kwa kipindi kirefu..

Fanya uchaguzi ni kwa faida yako na si kwa faida ya Mungu.

Unahitaji hatua moja tu kuyafikia mafaniko na ahadi zote alizokuahidia Mungu huzioni kwa sababu maandiko yanasema “umepungukiwa na jambo moja” wewe ni mzito katika kutoa una kila kitu cha kutoa lakini umekuwa mzito kufanya hivyo na ndio maana huoni mambo hayo yakitimilika..

Mtu wa Mungu elewa hili unapotoa hupungukiwi bali unafungua mlango wa kupokea kitu kingine kizuri zaidi kuliko kile ulichokitoa ukiendelea kunga’ng’ania utaendelea kubaki hivyo hivyo..

Pokea moyo wa kuchagua kutoa katika Jina la Yesu Kristo nimekuombea kwa jina la Yesu Kristo na fanya uamuzi kumbuka kutoa ni uamuzi binafsi..

Jilazimishe kufanya hivyo haitakuja kama bahati mbaya Lakini inahitaji kujifunza kufanya hivyo na Mungu atakupa nguvu ya kufanya hivyo.

Ubarikiwe sna na uwe na utekelezaji mwema..

Maranatha.

Mawasiliano: 0613079530.

@Nuru ya Upendo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *