Usishindane na zinaa ikimbie!.
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele yote karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Tofauti na inavyodhaniwa na watu wengi kwamba zinaa(uasherati & uzinzi) kwamba ni tamaa za mwilini/hitaji la mwili lakini ukweli ni kwamba sivyo jambo hili ni vita inayoanzia ndani yaani ni vita vya rohoni baadae ndio vinatokea mwilini hivyo hata kuishinda zinaa ni lazima kwanza uishinde ndani yako kisha nje itakuwa rahisi.
Ili kuelewa jambo hili sio la mwilini tu bali rohoni turejee maneno ya mwokozi wetu alieushinda ulimwengu na kutupa wokovu wetu….( Mungu akitupa neema tutajifunza kwa kina madhara ya zinaa katika ulimwengu wa roho)
Mathayo 5
27Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;28 lakini mimi nawaambia, *Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake* .
Unaona hapo katika Mstari wa 28? “…. kumtamani,amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Kuonyesha jambo hili linatendeka Kwanza ndani ya moyo wa mtu nje inakuwa ni Kama ushahidi tu.!
Na madhara yake yaanzia ndani kisha yanaonekana nje.
Sasa vijana wengi wa Kikristo hawataki kuikimbia zinaa ila wanataka kushindana nayo na inawashinda wanaanguka katika uzinzi. Ndugu yangu ikiwa hutaki kukimbia unataka kushindana nakuhakikishia asilimia zote hutashinda haijalishi unanguvu nyingi rohoni, haijalishi unaomba sana,haijalishi unafunga sana lakini hutashinda. Umeambiwa ” kimbia..”
Zinaa ina nguvu kubwa mno(maana ni kitu pekee ambacho kinaweza kuharibu hatima yako yote ya maisha yako).
Yusufu ilimghalimu kukimbia na si kusema haitawezekana halafu akaendelea kukaa mazingira hayo hayo.
Mwanzo 39
10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.
11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;
12 huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.
Unaona hapo? Kila siku mke wa Potifa alikuwa akisema na Yusufu juu ya jambo hilo hilo. Lakini Yusufu hajutaka kusikiliza maana yake jibu la Yusufu lilikuwa hapana kisha anaendelea na majukumu yake bila kumpa muda wa kumsikiliza.
Katika mstari wa 12 tunaona jambo linalotokea mwanamke akamshika Yusufu nguo yake kwa nguvu yaani mke wa Potifa alitumia nguvu kubwa kuhakikisha Yusufu hatoki lazima litimie jambo lake lakini Yusufu hakuwa radhi kufanya hivyo. Usifikiri tendo la ile nguo kuchanika ilikuwa ni mara moja tu la. Bali kulikuwa na mvutano mkubwa pale na kilichosaidia ni nguo kuchanika isingelikuwa hivyo Yusufu asingetoka fikiria.
Yusufu hakuwa anavaa nguo za kimaskini zilizoisha isha bali nguo nzuri na mpya tena imara. Na nguo za zamani tofauti na za sasa zamani hakukuwa hata na utengenezaji wa vitu ili mradi tu na kumbuka nguo hizo alikuwa anazipatia kwa mtu mkubwa yaani Potifa.
Unaona jinsi ambavyo Yusufu alipambana? Si kidogo bali sana kuhakikisha Mungu hamtendi dhambi, wala Yusufu hakulegea aliendelea kushikiria msimamo.
Umewahi kufikiri kwa nini Yusufu alikimbia? Ni kwa sababu alijua kabisa kama nitaendelea kubaki hapa nitamkosea Mungu. Yusufu alikuwa ni mtu kama wewe na mimi hakuwa na kitu spesho sana la!.
Na tendo lile angelifanya lingezima mpaka hatima yake ya kuwa waziri mkuu wa dunia nzima yaani baada ya Farao ni yeye na dunia nzima ilimjua Yusufu zaidi hata ya Farao.
Paulo anamuonya pia Timotheo kwa maneno haya..
2 Timotheo 2:22
“Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”
Unaona hapo? Hasemi “ lakini shindana na tamaa za ujanani” bali anasema; “ Zikimbie”
Vijana wengi wa Kikristo wanaanguka katika shimo hili wengi kwa sababu wanataka kushindana.
Vijana wa Kikristo wanaagalia picha za uchi, halafu wanajitumainisha hawawezi kuanguka, wanaanzisha mahusiano kwa kujidanganya kuwa hawawezi kuzini(pasipo Mungu kuingilia kati lazima utaanguka tu.) Mtashikana huko nk, binti/kijana mnachati chati tu bila sababu ya msingi kwa mpaka usiku wa manane wala hakuna point ya msingi mnafikiri mtapona.
Unaendelea kuchati na mtu ambe tayari uliamguka nae katika uzinzi badala ya kukata Mawasiliano nae kabisa na kugeuka unafikiri utashinda?
Ndugu yangu toba ni geuko, wala sio machozi na kulia sana hiyo sio toba unasema mpaka hutarudia ni mwisho ndugu toba ya kweli ni kugeuka na kuanza upya kabisa.
Kulia na kujutia tu bila kuacha hizo ni hisia ambazo kila mtu hata amabe hajaokoka anazo pale anapofanya jambo ambalo si sawa mtu yoyote anajuta na wakati mwingine analia lakini baadae ataendelea..
Huyo mtu ambae umezini nae mwambie sasa nimeamua kubadilika napita njia hii ule ulikuwa ni ujinga na tulimkosea sana Mungu. Tubuni na muanze maisha mapya.
Ndugu yangu hutashinda ukitaka kushindana maandiko yanasema “ Kumbia ” wewe unasema “ siwezi kupatwa na kitu chochote “
Zinaa inaharibu kabisa na mahusiano yako na Mungu kuliko kitu kingine unapofanya hivyo ni juu ya mwili wako mwenyewe unauharibu kulingana na maandiko.
Mawazo yako anaza kuyabadilisha. Angalia pia vitu unavyovifanya vinachochea uzinzi au la?.
Mkristo unaangalia na kusikiliza miziki ya kidunia ambayo inachochea uzinzi na umeijaza kwenye simu yako. Mkristo unaangalia tamthilia ambazo nyingi zina promote ushoga/mapenzi ya jinsia moja na wewe unakaa unaangalia kweli wewe ni Mkristo? Au ni Mkristo jina?.
Kile unachokiangalia na kukisikiliza sana kina nafasi kubwa ya kukujenga au kukubomoa. Futa miziki yote ya kidunia,futa tamthilia zote acha kufatilia.
Kisha sehemu uliyokuwa unasikiliza miziki ya kidunia weka maombi,kwenye tamthilia weka kusoma neno na kutafakari, kisha tendea kazi ufahamu wako utabadilika na wewe utakuwa mtu mwilini kabisa.
Ubarikiwe sana na Bwana YESU.
Maranatha.
Mawasiliano:0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.