JE! Kiongozi wa dini anaruhusiwa kusamehe dhambi?

Maswali ya Biblia No Comments

 

Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe sana.

Mpendwa mwenzetu anauliza JE ni sahihi kwenda kutubia dhambi zako kwa kiongozi wa dini mfano padre, kama ilivyoandikwa katika (Yohana 20:23) ?

Jibu: kwanza turejee mstari husika..

Yohana 20:23 ” Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.”

Tuongezee..

18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19 NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.”

Sikiliza, anaposema amempa Petro funguo za Ufalme wa Mbinguni yaani kufunga na kufungua Ambayo yaweza kumaanisha kumsamehe au kumhesabia mtu dhambi, alimaanisha kuwa Petro pamoja na mitume wale wengine kuwa wamepewa uwezo wa kumwomdolea mtu dhambi zake kwa kumpa uelewa au Neno la Mungu [injili]. Lakini SI kwa mamlaka ya kutamka tu kama ilivyoeleweka na wengi, la!

Ndio maana walipohubiri walisema “TUBUNI NA MKABATIZWE, KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO” (Matendo 2:38)

Unaona! Hawakuwasamehe wao Bali waliwapa njia Ambayo kwa hiyo wangepata Msamaha wa dhambi zao na kupokea kipawa Cha Roho Mtakatifu.

Hivyo tukirejea Maandiko suala Hilo la kiongozi wa dini kusamehe dhambi sio sahihi! Kwanini? Hakuna mwanadamu aliyepewa mamlaka ya kusamehe dhambi!, na kwanini ifanyike hivo angali Mungu wetu Yu hai?
Huo ni Upotovu mkubwa kiongozi kumtamkia mtu kuwa amesamehewa dhambi.

Huko ni Kuangamizwa!, kwa kukosa Maarifa sahihi ya neno la Mungu kama alivyosema Mungu kupitia Hosea, kuwa watu wanaangamizwa!

Hosea 4:6a ” watu wangu WANAANGAMIZWA kwa kukosa Maarifa…..”

Kuwa Mwangalifu, Na Mungu akubariki sana

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *