Nini maana ya mstari huu warumi 1:25

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mwana wa Mungu karibu tujifunze neno la Mungu ambalo ni maji ya uzima.

NI KIUMBE GANI KINACHOSUJUDIWA HAPO KATIKA WARUMI 1:25?

Warumi 1:25 inasema”kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya muumba anayehimidiwa milele” Amina.

Kiumbe ni kitu chochote chenye uhai kama vile wanyama na mimea.

Maandiko yaliposema kuwa wameibadili kweli ya Mungu kuwa uongo na kukisujudia kiumbe inamaana kuwa ni kiumbe chochote chenye uhai kama vile ng’ombe, mbuzi, ndama, mtu, miti, n.k ambavyo ni machukizo kwa Bwana.

Wanaofanya hivyo maandiko yanasema wanafanya kwa makusudi kwakuwa wanajua hivyo vyote siyo Mungu.maandiko yanasema katika

Warumi1:20”kwasababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumwa ulimwengu yanaonekana,na kufahamika kwa kazi zake;yaani,uweza wake, wa milele na uungu wake; hata wasiwe na udhuru;

21 inasema”kwasababu, waliopomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu Wala kumshukuru; Bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo Yao yenye ujinga ikatiwa Giza.

22 inasema” wakinena kuwa wenye hekima walipumbazika;

23 inasema” wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu,na ya ndege,na ya wanyama na ya vitambaavyo.

24 inasema” kwaajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo Yao,waufuate uchafu,hata wakavunjiana heshima miili Yao.

25 inasema”kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya muumba anayehimidiwa milele. Amina”

Ikiwa wewe unamuogopa mtu,unamtegemea mtu,unamsujudia mtu Haina tofauti na kuabudu kiumbe hata pia kuwa bize na kukosa muda na kukosa muda na Mungu.

Yeremia17:5 “ Bwana asema hivi,amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha Bwana.

6 inasema” maana atakuwa kama fukara nyikani,hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame,katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

7 inasema” Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana,ambaye Bwana ni tumaini lake.

8 inasema”maana atakuwa kama mti, uliopandwa kando ya maji uenezao mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo,Bali Jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.

Mfanye Bwana awe tegemeo lako

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *