Kwa nini unaomba na hauoni matokeo?.

Biblia kwa kina, Maombi na sala No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Watu wengi wana bidii katika maombi wengine wanafunga kwa kipindi kirefu lakini mwisho wa siku hawaoni matokeo katika kile walichokuwa wanakiomba. Mwisho inapelekea kukata tamaa na kuona kama Mungu hawasikii ama yupo mbali na wakati mwingine wanahisi kuwa huenda wamekosea mahali fulani ndio maana hakuna majibu wanarudi kuomba maombi ya toba lakini bado wanaingia kuomba tena na majibu yanakuwa ni ya kawaida sana tofauti na walivyojitaabisha.

Wakati mwingine wanapanda. Milimani na kutafuta sehemu za utulivu kabisa wanaomba lakini hakuna matokeo yoyote na bado wanajiona ni wakavu kabisa ndani.

Ukweli ni kwamba Mungu hayuko mbali yupo karibu sana zaidi ya tunavyodhani pale tunapompelekea maombi yetu.

Yeremia 23:23.“Mimi ni Mungu aliye karibu, asema Bwana, mimi si Mungu aliye mbali.”

Unaona hapo? Maandiko yanaweka wazi kuwa Mungu hayuko mbali yuko Karibu hivyo unavyoingia kwenye maombi cha kwanza amini kuwa Mungu yuko Karibu na wewe na wewe sana.

Na Mungu kujibu maombi yetu haihitaji ukamilifu wetu ikiwa tutaelewa ama tutafata kanuni sahihi za kuomba. Na Mungu amesema kuwa..!

Yeremia 33:3“Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.”

Mungu ameahidi kuwa tukimuita atatuitikia Mungu wetu si sanamu bali ni Mungu aliehai. Lakini sio kuitika tu lakini ameahidi na kutuonyesha mambo makubwa na magumu tusiyoyajua kupitia kumuita kwetu yaani maombi..

Hivyo unavyoingia katika maombi yako elewa na amini kabisa Yesu Kristo atakuitikia lakini kama utafahamu kanuni sahihi ya kuomba.

Hivyo tutakwenda kuangalia sababu zinazofanya maombi kutokuwa na matokeo.

Sababu zinazosababisha maombi kutokuwa na matokeo.

1.Mashaka(kutokuamini)

Hii ni sababu kubwa sana inayksababisha maombi kukosa matokeo. Mungu haangalii wingi wa maombi unayoyapeleka mbele zake,haangalii wingi wa machozi unayolia,wala kufunga kwako miezi au mwaka si kitu anachokiangalia sana Mungu anachoangalia je kile unachokitamka unaamini? Kuwa yeye anaweza kukifanya? Je humtilii mashaka?

Mungu alieziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo si wa kutiliwa mashaka kabisa kama utamuelewa.

Yakobo 1

6 Ila na aombe kwa imani, PASIPO SHAKA yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7 Maana mtu kama yule ASIDHANI YA KUWA ATAPOKEA  KITU KWA  BWANA.

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

Unapokuwa na mashaka kuwa “sijui kama Mungu atajibu au atanipa, nahisi hiki kitu kama siwezi kupokea ngoja nijaribu tu kuomba huenda nikapata nk”  unaonesha kutokumuamini Yeye. Maandiko yametupa hakikisho..

Marko 11:24“Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.”

Si kazi yako kujua Mungu atakujibu kwa njia yako kazi yako ni kuamini tu kuwa Mungu ameshafanya katika hili kuwa na ufahamu huu unapoomba “hakuna kitu ambacho Mungu hajasikia na kujibu amejibu vyote

Amini tu hivyo mengine yote muachie yeye.. kuwa kama mtoto mdogo anamuamini mama/baba kuwa akisikia njaa atakula swala la kuanza kuchunguza chakula kimo au hakuna baba/mama ana hela sio jukumu lake jukumu lake yeye ni kudai chakula anaposikia njaa.. swala la mama atatoa wapi pesa si lake..

Maandiko yanaendelea kutuhakikishia..

Mathayo 7:7“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;”

Hakikisho ni kwamba ukiomba utapewa.. ukitafuta utaona.. ukibisha utafunguliwa.

Kazi yako wewe amini ukiomba utapata Mungu si muongo..

2.Fikra.

Hiki pia ni moja ya kitu kinachosababisha maombi kutokuwa na matokeo. Ikiwa unaomba kwa mdomo lakini ufahamu wako/fikra zako ziko zinawaza mambo mengine itakuwa ngumu sana kuona matokeo ya kile unachokiomba..

Unapoomba elekeza fahamu zako katika kile kitu unachokiomba na zielekeze kwa Mungu usiombe unataka Mungu akuze karama yako ukafanyike baraka kwa wengine lakini akili yako inawaza mikoani,mumeo,mkeo,biashara itakuwa ngumu.. Roho Mtakatifu anahitaji pia muunganiko wa fikra zetu na roho zetu kwake inakuwa rahisi kuingia kati na kuanz kuomba na sisi..

Roho Mtakatifu hawezi kuomba na wewe ikiwa fikra zako hazipo katika kile unachokiomba.. hivyo unapoomba onyesha nia ya kukihitaji hicho kitu ruhusu ufahamu wako ujae kitu hicho.. na hakikisha kile unachokitoa kinywani mwako ndio unachokihitaji katika roho yako.

Ukiwa unaomba ukuwaji wa kiroho kuwa na shauku kabisa ya kutaka kuongezeka na mwambie Yesu Kristo hiki kitu naomba kiwe ndani yangu..

Unapoomba huku fahamu zako zinawaza kazini, nk ni sawa na unapeleka mahitaji ksa baba yako ukiwa na earphones masikioni..

3.uvumilivu.

Maombi yanahitaji uvumilivu usiombe kidogo ukaona hakuna matokeo ukakatisha maombi yako . Unapohisi Mungu hakusikii ndio wakati Mungu anakusikia sana. Hivyo usiombe dakika 30 ukaacha au lisaa au mwezi au mwaka ukaona inatosha maandiko yanasema.

Luka 18:1“Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.”

Jifunze kuwa mvumilivu sana katika maombi unapoomba unaona hakuna dalili unaona jangwa Mungu yupo pamoja na wewe na anakusikia hivyo usiahirishe endelea na Bwana atakujazi katika hicho unachoomba..

Maandiko yanasema ombeni bila kukoma. Hivyo omba usikome wala kukata tamaa..

Mambo haya ukiyazingatia vyema utaanza kuona mabadiliko mengine kabisa katika maombi yako.

Hivyo hupokei si kwamba wewe si mkamilifu,au si kwamba huendi kanisani,au hufungi,hapana.. bali hivi vitu mashaka,fikra,uvumilivu havijawa kwa wingi jitahidi kuzidhibiti fahamu zako uwapo kwenye mombi,kuwa mvumilivu,

Usiruhusu mashaka ndani yako na mashaka yanaondoka kwa wewe kuanza kusikiliza sana mafundisho na kusoma biblia sana imani inaanza kujengeka ndani yako mwisho unaenda kuomba pasipo kuwa na shaka..

Kumbuka imani chanzo chake ni kusikia hivyo wekeza sana kusikia kwa makini unapokuwa ibadani.. usilale ibadani. Kuwa Makini imani itajengeka kabisa..

Bwana wangu Yesu Kristo akubariki sana naimani ukizingatia haya utaona matokeo makubwa sana maombi yako hayatakuwa ya kawaida.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema

kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *