“Mkiwa na Imani, Msipokuwa na Shaka Mtafanya si hilo la Mtini tu,..”

Biblia kwa kina No Comments

“Mkiwa na Imani, Msipokuwa na Shaka Mtafanya si hilo la Mtini tu,..

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Wote tunaifahamu habari inayopatikana katika kitabu cha Mathayo 21:19-22 kama huifahamu ni vyema ukachukua muda wako kusoma na kutafakari naimani Roho Mtakatifu atakupa mengi zaidi kutoka katika habari hiyo fupi.

Kila Habari iliyoandikwa kwenye Biblia ina fundisho kubwa sana nyuma yake na Kristo anatamani sana tufahamu.

Baada ya tukio hilo Bwana Yesu anawaambia wanafunzi wake sentensi hii ambayo nimetafakari nikajikuta napata maswali kadhaa lakini Roho Mtakatifu hakuniacha nibaki nayo bali alinipa majibu sahihi ya maswali hayo..

Tukio lile Bwana Yesu alilifanya ili kuwafundisha jambo wanafunzi wake pamoja na sisi na jambo hilo ni Imani.

Swali nililojiuliza la kwanza kabisa ni hili..

Swali..”Kwa nini tunakuwa na mashaka?

Nilitafakari nikiunganisha na maneno ya Bwana Yesu aliyowaambia wanafunzi wake. “…Mkiwa na Imani,Msipokuwa na shaka Mtafanya si hilo la Mtini tu, lakini hata mkiuambia mkuyu huu Ng’oka,Ukatupwe baharini, litatendeka”

Jibu: “Ni kwa sababu hatuujui uweza wa Mungu. Tunasikia tu lakini hatuna Imani kama mambo hayo yanaweza kutendeka yaani hatuujui uweza wa Mungu katika uhalisia..”

Ndugu msomaji ni rahisi sana kusema Mungu anaweza katika kinywa chako lakini kuamini kwamba inaweszekana moyoni na katika fahamu zako (akili) mwako si rahisi mashaka ndio yatatawala na utajikuta unasema.

Sidhani..itakuwakuwaje kuwezekana kitu kama hichi? Ngoja nione” maana yake tunauweka uweza wa Mungu katika kubahatisha hiki ni kitu kibaya sana.

Lakini niliendelea kujiuliza Maswali zaidi..

Swali: “Tunawezaje sasa kuwa na Imani?”

Kwa namna ya kawaida tunaona kuwa na Imani bila kuwa na mashaka haiwezekani lakini kumbe inawezekana kabisa..

Na kuna kanuni zipo kama tukizifuata basi Imani itajengeka ndani yetu wala hatutaona shaka.. ni swala la muda tu na kumaanisha kweli.. hakuna ugumu wowote katika kujenga imani kama tunavyofikiri bali kuna kanuni za kuzifuata tu.

Kumbuka “kupata kitu chochote kile kiwe ni cha mwilini au cha Rohoni kuna kanuni za kufata”

Pasipo kanuni basi ni ngumu kupata kitu fulani unachokitaka.

Na hapa nilipata majibu kadhaa.

Jibu:

1.Kusoma  sana neno na sio kusoma tu pia kwa kurudia rudia. Unaposoma kwa kurudia rudia kuna vitu vingi sana unavipata

Utakubaliana na mimi kama umewahi kusoma kitabu kizima kwenye Biblia na ukakifahamu vizuri siku ukija kukisoma hata baada ya siku mbili utagundua kuna vitu kama vile hukuwahi kuviona ndio vipya kabisa.

Sasa unaporudia kumbuka maandiko yanasema..

Waebrania 4:12. “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”

Neno la Mungu maandiko yanatwambia kuwa li hai na lina nguvu. Unavyorudia rudia kuna mambo makubwa sana yanafanyika rohoni.

2. Kuomba(kuwa muombaji sana).

Maisha ya mwamini yoyote mwenyewe mahusiano mazuri na Mungu lazima awe ni muombaji.. ni wajibu wa Mkristo kuomba mtu mmoja aliwahi kusema “kama tusipoomba nahisi kama Mungu hafanyi chochote..” na ni kweli kabisa Wakristo wengi waliosimama na Mungu kweli kweli wote walikuwa ni waombaji.

Maandiko yanasema.

Luka 18:1“Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.”

Na mtume Paulo anamwandikia Wathesalonike waombe bila kukoma..Epafra alikuwa ni muombaji vivyo hivyo kuliombea kanisa la Kolosai lisimame na ilikuwa. Wakina John Wesley nk. Hivyo Imani pia inajengeka sana katika maombi Mungu anasema na sisi.

Leo hii maombi yamekuwa ni kama mzigo kwa Wakristo wengi.

3.kufunga.

Tunajua Mifungo tunapata nafasi nzuri ya kuyatisha mapenzi ya mwili chini.. hivyo kama ni hivyo maana yake ni kwamba roho zetu zinakuwa na nguvu zaidi katika kumkaribia Mungu.. Ukristo ni kujikana funga sio mwaka mzima unaisha na unasema ni Mkristo hujawahi kufunga unakulaga tu.

Niliendelea kujiuliza zaidi..

Swali:”Tunawezaje sasa kuona matokeo ya kitu tunachokiomba?”

Nilitamani kufahamu jambo hilo Mungu wetu ni mkuu hakika nilipata jibu lililoufurahisha sana moyo wangu.

Jibu:”Kuamini kuwa yeye yupo na anaweza kufanya.”

Shetani anatabia ya kutudamganya kwamba tunapokuwa katika kuomba tukiwa hata na dosari yoyote basi hatuwezi kupokea wala Mungu ni ngumu kutusikia lakini ukweli ni kwamba Mungu anatusikia na anatujibu kabisa na tunapokea.. inakuwa ngumu mambo yale kudhirika kwa sababu ya Mashaka wakati mwingine.”

Maana kama Mungu hatusukii tukiwa na doa lolote kwanza sisi si wakamilifu asilimia zote sisi tunaweza tukajiona tuko sawa lakini si mbele za Mungu.

Hivyo tunapokea kwa Imani na zaidi sana ni kwa neema katika Kristo Yesu tumehesabiwa haki na sio hivyo tu tumefanyika kuwa Warithi pamoja na Kristo.

Shetani na fikra zetu ndio huwa zinasema uongo na kupingana na ukweli(Neno la Mungu) Fikra zetu,Shetani wote ni waongo lakini Neno la Mungu ni kweli na ni hakika halisemi uongo na halibadiliki… Haleluya.. Glory to God. 

Naimani kupitia makala hii fupi kuna jambo kubwa umejifunza.

Kumbuka katika mambo yote hayo kama vile kuomba,kusoma kwa kurudia rudia(usiridhike kwa kusoma mara moja ukasema najua acha) na kufunga ni mambo yanayohitaji gharama..

Ikiwa mambo ya mwilini kama Elimu,Mali yanapatikana kwa gharama kubwa kwa kufanya kazi kwa bidii na kusoma kwa bidii vivyo hivyo mambo ya rohoni?

Je unatamani kuwa dhabiti katika imani na kumuelewa Kristo? Jikane usiuangalie mwili soma sana jifunze sana, omba sana,kuwa mfungaji itakuwa kama mateso kwa kipindi kidogo lakini nakuhakikishia UTAYAFURAHIA MATOKEO. Umia kwa kitambo kidogo lakini yafurahie matokeo.

Weka kuwa ni maono yako mwaka 2025 kisha kuwa na Nidhamu yatimilize hakika utamuona Mungu kwa viwango vingine. Zaidi.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *