Je! Watu watakaookolewa au watakaonyakuliwa ni wachache?

Siku za Mwisho No Comments

Je! Watu watakaookolewa au watakaonyakuliwa ni wachache?

Je! biblia inasemaje? kuhusu hili.

Hebu tusome jibu la Bwana Yesu.

Luka 13:22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu.

[23]Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

[24]JITAHIDINI KUINGIA KATIKA MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba WENGI watataka kuingia, wasiweze”.

Note hilo neno WENGI WATATAKA KUINGIA, WASIWEZE.

Ni wazi kuwa watu watakookolewa siku ya mwisho ni wachache!!

Tusome tena..

Mathayo 7:13 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, NAO NI WENGI waingiao kwa mlango huo.

[14]Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao WAIONAO NI WACHACHE.”

Maandiko hayo yanaeleza wazi kabisa kwamba watakaokolewa ni WACHACHE, kwasababu njia imesongwa sana! lakini swali linakuja je hii njia imesongwa na nini? Ni wazi kabisa imesongwa na mambo mengi ya ulimwengu huu ambayo ni, anasa, upendaji fedha kupita kiasi, wivu, chuki,tamaa, uasherati uliokithiri ambao sasa upo mpaka kwenye mitandao mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo, mitindo ya wanawake kutembea nusu uchi, burudani na miziki ya kidunia,ufisadi n.k. na zaidi ya yote ni kuongezeka kwa wimbi kubwa la manabii wengi wa uongo na hivyo kuifanya ile njia ya kweli isitambulike kirahisi, kwasababu imechanganyikana na njia nyingine nyingi za uongo mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, na jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo ile njia ya ukweli inavyozidi kuwa nyembamba zaidi, imefikia hatua ya kwamba ukristo wa leo unapimwa na kiwango cha mafanikio ya kidunia aliyonayo mtu na sio mafanikio ya kiroho (yaani utakatifu), Neno la kweli limetupwa nje!.

Bwana Yesu Kristo aliweka wazi pale aliposema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu?

Jambo ambalo wakristo wengi hatufahamu, ni pale tunapodhani Mungu ana ile kauli ya “wengi wape”..Yaani, kwasababu ulimwengu huu uliojawa na uovu na waovu wengi Mungu hawezi kuuangamiza au kunyakua wale wachache walio waaminifu kwake..

Yesu alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, na kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, jiulize, waliookoka katika siku za Nuhu walikuwa ni wangapi kama sio 8 tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwa ulimwenguni, vilevile waliookoka katika siku za Lutu walikuwa wangapi kama sio watatu kati ya Malaki ya watu waliokuwa katika miji ile ya Sodoma na Gomora,

Ukitazama tena kwa ukaribu utaona aliye nyakuliwa alikuwa ni mtu mmoja tu (HENOKO) kati ya watu wote waliokuwa wanaishi kipindi chote kabla ya gharika, kwasababu ni yeye tu peke yake ndiye aliyempendeza Mungu.

Vivyo hivyo katika wakati huu watakaonyakuliwa ni wale tu watakaompendeza Mungu, hao ndio peke yao watakaosikia Parapanda ya Mungu ikilia kutoka mawinguni, hata kama watakuwa ni watu 100 katika ulimwengu mzima, hao tu ndio watakoenda, wengine wote waliosalia hawatajua chochote, watashangaa tu mbona kundi dogo la watu wachache sana halipo duniani..

Wengine watadhani, wameibiwa tu, wengine watadhani wametoroka, n.k. Lakini ulimwengu hautaelewa chochote kwasababu litakuwa ni kundi dogo sana, kumbe hawajui wenzao siku nyingi tayari wapo mbinguni wakila karamu ya mwana kondoo, lakini huku chini kitakachokuwa kinaendelea ni dhiki kuu ya mpinga Kristo. Na baada ya hapo ni maangamizo.

Hivyo ndugu tujitahidi tuwe kati ya hao wachache watakaokolewa kwa kupita hiyo njia nyembamba iliyodharauliwa na kuchekwa na ulimwengu wote nayo ni UKRISTO ULE WA MTINDO WA KALE WA MITUME..ikiwa wewe ni mwanamke tupa nguo za kizinzi uvae kama mwanamke wa kikristo mwanamke wa kikristo havai vimini, suruali wala kaptula, hapaki wanja wala lipsticks, mwanamume wa kikristo hanywi pombe, sio mtukanaji, mkristo yoyote hapaswi kupenda mambo ya ulimwengu? Bwana Yesu alisema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako.?

Ni wakati wa kutafuta vitu vya kimbinguni ili siku ile isitujie kama mwivi. Muda umeenda sana tunaishi katika kizazi kibaya kushinda vyote, tuwe macho Bwana yu mlangoni kuja. Amen.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *