Turejee neno la Bwana ili tupate maana iliyo Bora zaidi.
Isaya 66:3 “Yeye achinjaye ng’ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao”.
Kutokana na hili neno tunaweza kuona kuwa hatuna ruhusa ya kula nyama kwakuwa unaonekana ni chukizo lakini katika uhalisia ni kwamba Bwana wetu Yesu Kristo anapendezwa na matoleo tunayoyasongeza mbele zake na ndiyo maana Wana wa Israeli walikuwa wakimtolea Bwana sadaka za amani na za kuteketezwa naye alikuwa akizipokea hivyo katika hili neno haijamaanisha kuwa tusile nyama.
Kwa upande mwingine utaona kwamba watu wanadhani kuwa kutoa matoleo mengi zaidi kwa Mungu ndiyo anapendezwa nayo hapana! Mungu wetu anaangalia mioyo yetu ikiwa tunamtolea kwa kupenda ndipo anapopendezwa nasi kwakuwa unaweza toa vingi pasipo kupenda inakuwa sawa na Bure.
Pia anasema Dunia na vyote vilivyopo ni Mali yake kwakuwa hatuwezi kumtolea Bwana kitu cha kipekee ambacho hajakiumba na kuifanya yeye bali tunaweza kumtolea katika alivyotubarikia kwa moyo wa kupenda tukijua kuwa yeye ni Mungu.neno la Bwana linasema.
Isaya 66:1 “BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?
2 Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu”.
Pia Mungu wetu anapenda sadaka za watu wanyonge, walionyenyekea na kupondeka mioyo na wale watendao maovu sadaka zao hazitakubaliwa mbele zake zitakuwa ni machukizo tu.
Hivyo mtu mwovu atoapo sadaka mbele za Bwana inahesabika kuwa ni sadaka ya hatia na ya dhambi.
Neno la Bwana linasema
Mithali 15:8 “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA…”
Hivyo sadaka ya mwenye dhambi ni chukizo kwa Bwana linatupasa tutende yaliyo mema ili tuwe karibu na Mungu.
Neno la Bwana linasema
Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili
Inatupasa tutende yaliyo mema yanayompendeza Bwana ili sadaka zetu zipokelewe na yeye pia tusiwe na chuki sisi ikiwa unachuki na mtu nenda kapatane naye ndipo utoe sadaka kwa Bwana nazo zitapokelewa.Neno linasema
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.