Vitimvi ni nini kama ilivyotumika katika biblia?
Ni mipango inayopangwa na kikundi cha watu kwa lengo la kuvurugwa, kuharibu, au kutenda ubaya kwa mtu au watu ili kuitimiza mikakati na makusudi waliyonayo juu ya huyo mtu.
Baadhi ya watu hukutana ili kufanya ubaya kwa mtu kwa lengo la kudhulumu mali alizonazo, kulipiza kisasi kwa ubaya waliotendewa na huyo mtu pia kwa Yesu vivyo hivyo walikutanika kwa Siri ili kufanya njama za kumuangamiza (kumuua) na walikutanika walikuwa ni mafarisayo masadukayo na wayahudi.
Pia katika biblia tunaona baadhi ya mitume walifanyiwa vitimvi ambavyo vilibeba madhumuni ya kuwaangamiza ili wasiendelee kuhubiri kweli ya Kristo mfalme. tunaweza kusoma maandiko haya ili tuelewe na kujifunza zaidi.
Matendo 20:2 “Naye akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.
3 Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi KUMFANYIA VITIMVI, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia”.
Pia tunaona mtumishi wa Mungu Stefano alifanyiwa vitimvi na watu wa sinagogi lililoitwa mahuru, wakirene, waiskanderia na wakilikia tutapitia tuone kama ilivyoandikwa katika biblia.
Matendo ya Mitume 6:9
[9]Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;Matendo ya Mitume 6:9,12
[9]Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
[12]Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.Matendo ya Mitume 6:9,12-13
[9]Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
[12]Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.
[13]Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;
Na hata mwisho wa siku waliungana na kumpiga Stefano kwa mawe mpaka umauti ukamkuta hata akasema hivi.
Matendo ya Mitume 7:59
[59]Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.
Hivyo kutokana na Imani tuliyoibeba juu ya Kristo kuna wakati utafikia tutakuwa tukionewa, kuzushiwa, kuhuzunishwa na kutaabishwa katika yote inatupasa tujipe moyo kuwa tunaye Mungu ambaye ndiye msaada na kimbilio letu hivyo tutashinda.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.