Vitanga ni nini kama ilivyotumika katika biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Ni sehemu ya mwisho iliyo katika mkono wa mwanadamu inayotumika kusaidia kushika au kubeba vitu au kitu.

Au

Ni sehemu ya mwisho mkononi iliyounganika na kuacha za mwanadamu au mnyama.

Hebu tujifunze katika maneno ya Mungu ili tupate maana iliyo Bora zaidi.

Danieli 5:24-25
[24]Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.
[25]Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI

Mambo ya Walawi 14:26-27
[26]kisha kuhani atamimina sehemu ya hayo mafuta katika kitanga cha mkono wake mwenyewe wa kushoto;
[27]kisha kuhani atanyunyiza baadhi ya hayo mafuta yaliyo katika mkono wake wa kushoto, kwa kidole chake cha mkono wa kuume mara saba mbele za BWANA,

Mambo ya Walawi 11:27
[27]Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni

Isaya 49:16
[16]Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

Pia tunaona kitanga kilitimika kuandika maneno yaliyobeba ujumbe wa Mungu kwenda kwa mfalme Belshaza.

Hivyo vitanga hutumika kufanya shughuli mbalimbali hivyo vitanga vyetu inatupasa tuvitumie katika wema zaidi badala ya ubaya. Ikiwemo ubadhilifu wa pesa.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *