Mwenye kitu atapewa,naye asiye na kitu hata kile alichonacho atanyang’anywa.
Jina la Mwokozi Yesu Kristo lihimidiwe milele yote karibu tuyatafakari maneno ya uzima..
Umewahi kufikiria kauli hii aliyoizumgumza Bwana Yesu kwa wanafunzi wake na watu waliomzumguka? Kuna jambo kubwa hapa ambalo Kristo anataka tulifahamu.
Marko 4:25 “Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.”
Swali la kutafakari kama mtu hana kitu atanyang’anywa je tena kitu alichonacho wakati hana? Je alichonacho ni nini mpaka anyang’anywe?
Ni vizuri hapa tujifunze juu ya maneno haya Mwenye kitu ni mtu wa namna gani na asiye na kitu ni mtu wa namna gani? Kiblia..
Mwenye kitu. Ni mtu anaekizalisha kile kitu alichonacho. Anahakikisha kinaongezeka hakibaki vile vile.
Asiye na kitu. Ni mtu alie na kitu lakini kitu alichonacho hakizalishi kinabaki kama kilivyo.
Ni kipi tunatakiwa kukifahamu hapa? Siku zote na ndivyo ilivyo kwa mtu yeyote anaemwamini Yesu Kristo kuna kitu anapewa ndani yake(Mungu anawekeza ndani ya huyo mwamini).. lakini Mungu anatazamia kitu alichokiwekeza ndani yake/yako ukizalishe kisibaki kama kilivyo.
Ila kiongezeke na kifanyike baraka kwa wengine na kiwasaidie pia. Kila mmoja amepewa kwa nafasi yake usijidanfanye ukasema “mimi nimeokoka hakuna kitu chochote Mungu kawekeza ndani yangu nitakuwa mshirika tu wa kawaida sitajishughulisha na chochote katika mwili wa Kristo.” Ndugu sivyo hivyo.
Maandiko yanasema…
Ufunuo wa Yohana 3:11“Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.”
Hakuwa anamaanisha ukae nacho kama kilivyo tu la! Lakini ni kuhakikisha ulichonacho hakibaki vile vile.. kama ni wokovu uliyopewa usibaki vile vile! Uendelee kukua/kuukulia wokovu usibaki mtoto mchanga kama ni karama isibaki vile vile bali itende kazi kwa manufaa ya mwili wa Kristo.
Mfano ukisoma Mathayo 25:14-30 yule bwana alietaka kusafiri na kuwagawia watu wa watatu(watumwa wake) taranta mmoja 5, mwingine 2,mwingine 1. Lengo kubwa la bwana wao atakaporudi akute zaidi ya kile alichokiacha yaani kimezalishwa.
Na kila mmoja alimpa kwa kadili ya uwezo wake hakuna aliependelewa.. kitu chochote Mungu anachokupa ni lazima utakuwa na uwezo wa kukimudu.
Sasa kwa namna gani asiyekuwa nacho atanyang’anywa??.
Ikiwa wewe umepewa karama ya uponyaji,uimbaji,miujiza,nk kama hutoki kwenda kuwaombea wagonjwa wapone,hutaki kuimba Mungu atukuzwe kupitia wewr na unaona ni kitu kiko ndani yako,hutaki kuomba ili miujiza itendeke na Mungu atukuzwe kupitia hiyo..
Neema hiyo uliyopewa juu ya karama hiyo itaondoka kwenda kwa mtu mwingine anaefanya hivyo anatoka kuwabea watu wapone,anafanya bidii katika kuimba kuhakikisha Bwana anatukuzwa kupotia sauti yake watu wanaokoka na wanabarikiwa.. anaomba miujiza itendeke kupitia yeye watu wamwamini Kristo.
Karama utabaki kuwa nayo lakini ile neema inayofanya karama hiyo itende kazi itakuwa haipo tena muda huo imeshaondoka kama ulikuwa unafanya kwa kujisikia nk.
Utabaki kuwa mtu wa kawaida tu usiye na mchango wowote katika mwili wa Kristo.
Usiwe mlegevu katika kitu alichokupa Bwana iwe ni wokovu hakikisha unakua kila siku kwa kuongeza maarifa,kuomba,kusoma neno nk kuwa na bidii na katika hicho ulichopewa usijione kuwa wewe ni spesho.
Wana wa Israeli walijiona kuwa wao ni spesho walidhani Mungu ni wao tu peke yao wala si wa mataifa na hawezi kuwa Mungu wa watu wa mataifa kabisa. Ikapelekea kuishi kama wanavyotaka wakaisukumia neema mbali.
Lakini wakati hui kulikuwa na watu wa mataifa ambao walikuwa hata hawajawahi kumjua vyema Mungu ila walikuwa na bidii tu katika kuhakikisha wanampendeza yeye kama wakina Ayubu,Kornelio,nk Mungu alijidhirisha kwao.. na kujisifu kupitia wao. Hivyo ulichopewa kishike sana.. shika wokovu wako hakikisha unaendelea kukua kumuelewa zaidi Yesu Kristo.. hakikisja karama yako inafanya kazi na kuujenga mwili wa Kristo.
Vinginevyo utanyang’anywa maana ya kunyang’anywa ni kitu ambacho ni chako lakini kinachukuliwa kwa nguvu na mwingine kwa sababu ya uzembe wako.
Naimani na nimekuombea Bwana Yesu akusaidie na ushike sana ulichonacho kifanyike baraka kwa wengine na Bwana atukuzwe kupitia wewe.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.