Fahamu njia kuu ya kumuona Mungu. 

Biblia kwa kina No Comments

Fahamu njia kuu ya kumuona Mungu.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Mungu kachagua njia moja kuu ya watoto wake waliomwamini kumuona na kuuona uweza wake. Bahati mbaya sana Wakristo wengi wanapoteza shabaha na kuanza kutaka Mungu wamuone katika mambo fulani ambayo sio mabaya lakini sio njia kuu ambayo Mungu ameikusudia kabisa.

Sasa njia hiyo ni ipi?

Waebrania 11

9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

Ukisoma kitabu chote cha waebrania sura ya 11 yote kinawazungumzia mashujaa wa imani na waliotembea na Mungu kwa viwango vya juu sana.. Ibrahimu aliuona mji ule wenye misingi ambao Mungu ndio mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu mwenyewe..

Aliuona mji huo kwa imani wala si kwamba aliona maono fulani la!.

Sasa Wakristo wengi sana wanalia na kukesha na kuomba wakitaka Mungu wamuone katika maisha yao. Sasa Wakristo wengi wamepungukiwa na imani ndani yao.

Wanataka waone kwanza ishara fulani ndio waamini badala ya kuamini kisha ishara hizo ziambatane na kuamini kwao badala yake wanataka kwanza ishara wanamuwekea Mungu mipaka wakati mwingine mtu anasema “Mungu nikiona jambo fulani ndio nitaamini…nk”  si vibaya lakini huo ni upungufu wa imani.

Ili maombi yako yafike mbele za Mungu na kupokea majibu haihitaji kukesha sana kuomba(kukesha ni muhimu sana) yaani kukesha lakini imani hakuna inakuwa ni sawa na kazi bure.

Mungu kaamua yeye sisi tumuone yeye na uweza wake kwa njia ya imani tu maono,ndoto, ishara nk hivyo ni vitu vya ziada tu!!

Acha kupoteza muda kuomba Mungu akutokee umuone uso kwa uso kama Musa nk imani ndio nguzo na njia  sahihi ya kumuona Mungu.

Ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *