Je mapepo yanaweza kurudi tena ndani ya mtu baada ya kutolewa?

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Maombi ya kukemea au kufukuza mapepo hayamfungui mtu au kumweka huru moja kwa moja! Bali yanafukuza Yale mapepo kwa muda, na baadae watarudi kuangalia Hali ya maskani yao, kama kuna upenyo wa kurudi watarudi, tusome..

Mathayo 12: 43 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate

.44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa

.45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.”

Watu wengi wanaosumbuliwa na vifungo vya mapepo hudhani kwenda kwa watumishi Fulani, wakaombewa na mapepo hayo yakaripuka basi ndio kiashiria Cha kwamba wameshapona au kuwa huru, hii sio kweli! Pepo hao watarudi tu, maana wewe ni maskani yao.

Kama usipopata fundisho na kusimama katika wokovu kweli kweli.

Baada ya kufukuzwa yule Pepo kwa Maombi Yale, ataondoka, lakini hawezi acha maskani yake kiurahisi, hivyo atarudi kutazama kama badiliko lolote kwenye maisha ya yule mtu?

Akikuta hamna atakwenda na kuita wengine Saba wenye nguvu kumzidi yeye(ili kujihakikishia ulinzi na usalama akae pasipo mashaka yoyote maana watakuwepo wanaomzidi nguvu wengine saba na watakuwa wakimlinda), aje kufanya nao makao kwako kama ulinzi, ili siku nyingine asitolewe kirahisi Tena, na ndio maana Hali huwa mbaya kuliko ya kwanza.

Sikiliza, Kufunguliwa kunaanza na mtu mwenyewe. Mfano unakuta mtu anatoa ushuhuda kuwa aliombewa na akapona ugonjwa Fulani, lakini baada ya mda Fulani ugonjwa ule umerudi na kuwa wa hatari zaidi!

Pia si Kila Pepo ni la kuripuka! Mengine hukaa ndani ya mtu kama tatizo Fulani, lakini kuna mengine ni yale Ambayo huja na kuondoka. Aina zote hizi haziwezi kuonekana kwa kusubiri kuombewa pekee, mengine ni ya kujitathmini kibinafsi! Yeyote ambae hajazaliwa mara ya pili au yupo nje ya Kristo anayo Roho Fulani au Pepo linalompelekea kufanya uovu Fulani kama vile.. (Uasherati, Ulevi, masturbation n.k)

Mtu anapookoka kiukweli kabisa, kwa kumpa Yesu maisha yake, kuziacha njia zake zote zilizo ovu, kubatizwa ubatizo sahihi na kuwa na Roho Mtakatifu basi anafanya Hali ngumu isiyoweza kuvumilika na wale Pepo wabaya, hayatakuwa na uwezo wa kurudi Tena maana ni Mali ya Kristo. Na hapo ndipo mtu anakuwa amefunguliwa rasmi!

Tunajifunza hata kwa Yesu Kristo, alipowafungua wenye Pepo aliwaasa wasifanye dhambi Tena(Wazaliwe mara ya pili), maana ndio deliverance iliyo na nguvu na kumweka mtu huru daima.

Mungu akubariki sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *