Karibu tujifunze maneno ya uzima kutoka kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Mwanzo 4: 16 “Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.
17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe”.
Henoko hakuandikwa kuwa ni mtoto wa kaini na hakuondoka pamoja na Yesu kristo. Henoko ambaye ni mtumishi wa Mungu ametokea katika familia ya sethi uthibitisho zaidi tunapata katika vifungu hivi
Mwanzo 5:18 “Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.
19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.
23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.
24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa
Henoko ndiye mwana wa yaredi aliyetokea katika uzao wa sethi ambaye alienda na Mungu na ndiye mtu wa saba kutoka kwa Adam.
Jambo tunalojifunza kutoka kutoka kwa henoko aliyeenda na Mungu ni hili kwamba aliyatenda yote yanayompendeza Mungu na alikuwa karibu zaidi na Mungu hata ikapelekea kutwaliwa na Bwana wetu Yesu Kristo.
Nasi yatupasa kuenenda katika njia za Bwana na utii kwa Bwana tukijua kuwa hapa duniani ni wapitaji na makao yetu yapo kwa Bwana wetu Yesu Kristo hivyo hatuna budi kufanya yampendezayo kristo ili mwisho wa siku tumpendeze yeye na tuufikie ufalme wa Mbinguni tukiwa wakamilifu.
Pia tusome
“Mathayo 24:42 kesheni basi; kwa maana hamjui siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
Pia tuwe watu wa kuomba, kusoma neno,kulitafakari na kuliishi ili tumuone na kumlaki Bwana wetu Yesu Kristo.
Yuda 1:14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake”
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.