Fahamu utendaji kazi wa Shetani katika kuwaangusha watoto wa Mungu.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Katika nyakati hizi za Mwisho Shetani anazidi kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi tofauti na hapo mwanzo ilivyokuwa. Kama Mkristo ni muhimu sana kulifahamu jambo hili ili uzidi kujithatiti na kusimama vyema na Kristo.

Ni muhimu kumuelewa adui yako mbinu anazozitumia ili kukuangamiza. Ukishindwa kumuelewa vyema adui yako basi jua kabisa hutaweza kumshinda hata kidogo.

Shetani yuko bize na amewekeza sana muda mwingi kuwawinda watoto wa Mungu yaani waamini(Wakristo) na wengi sana anafanikiwa kuwanasa katika maeneo mbali mbali kwa sababu hawaombi,hawasomi neno nk. Shetani hayuko bize na watu ambao hawajaokoka yuko bize na watu ambao tayari wameokoka maana ambao hawajamuamini Yesu Kristo hao wako katika milki yake.

Hivyo anawinda sana Wakristo yaani wale kweli walioamua kumfata Kristo hao anawawinda sana.

Na tofauti na watu wengi wanavyofikiri kuwa labda Shetani ili ampate mwamini au amuangushe basi atikise katika eneo la Familia,uchumi,afya,nk ndugu hii ni mbinu ya kizamani sana aliyokuwa anaitumia. Ijapo hata sasa anaitumia lakini kwake hii ni mbinu ya mwisho kabisa. Ukiona Shetani anagusa katika maeneo hayo jua tayari katika maeneo mengine ameshakushindwa.. ambayo tutayataza kwa ufupi hapa.

Na kama ameshakushindwa katika maeneo mengine basi fahamu kabisa hata atikise uchumi wako, Familia yako nk hataweza kukuangusha.. kama Ayubu alishindwa ndani na nje pia.

Anapokushindwa Shetani katika mitego yake basi ndio anahamia nje sasa lakini hawezi akataka kukuangusha kupitia nje ikiwa hajakushindwa ndani.. hivyo ndani panavyokuwa imara ndio kunamaimarisha hata nje.

Sasa ni mbinu zipi/utendaji kazi upi ambao Shetani anautumia kwa sasa ili kukuangusha?

1.kukuweka mbali na Mungu.

Shetani kitu anachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha anakuweka mbali na Mungu na akishafanikiwa hili basi wewe ameshakuweza.

Kwa namna gani anakuweka mbali na Mungu?.

Ni kupitia majaribu yanayoangukia(kusababishwa ) katika tamaa zako.. kama maandiko yanavyosema kuwa mtu hujaribiwa kwa tamaa zake mweyewe.

Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.”

Unaona kupitia tamaa uliyonayo na Shetani akishalijua hilo udhaifu wako uko wapi hapo hapo ndio anapambana kuhakikisha anakuamgusha kupitia hicho hicho. Au pale unapompa Shetani nafasi basi anahakikisha anaitumia vyema wala hafanyi makosa.

Sasa kwa nini anakuweka mbali na Mungu na ni kupitia nini?

Shetani anapofanikiwa kukuangusha katika dhambi fulani ni wazi kabisa itaathiri uhusiano wako na Mungu.. si kwamba Mungu atakuacha lakini wewe ndio utamuacha Mungu kama usipokuwa imara. Unapotenda dhambi inaondosha ujasiri hata wa kusogea mbele za Mungu. Katika fahamu zako na ndani kabisa unashuhudiwa kuwa hiki kitu si sawa badirika..

Unapozidi kukawia kufanya maamuzi utajikuta unakosa amani na ujasiri tena wa kusogea mbele za Mungu. Sasa kitu anachokifanya Shetani atakwambia kupitia fikra zako “umeshaharibu Mungu hawezi kukusamehe hata ufanye nini kwa hili ulilotenda..”

Sasa unapompa nafasi kwa kuyasikiliza maneno hayo utajikuta unaenda mbali zaidi na uso wa Mungu kwa kuona kuwa wewe haustahili na bahati mbaya unaweza kuingia katika maombi na usione uwepo wa Mungu ambao umezoea kuuona kila siku.

Ukishindwa kuzituliza fikra zako vizuri Shetani atakuja akwambie “unajichosha wewe mwenye dhambi acha kuomba maana Mungu hakusikii..” 

Kitu anachokitafuta ni wewe ufikie hatua ya kukata tamaa kabisa na ukishakata tamaa kabisa hapo yeye ndio anakuja Sasa kukumalizia vyema na mwisho utajikuta unasema “mimi nimeshakosa na Mungu hawezi nisamehe Sasa niendelee kuomba ya nini? Bola tu niendelee na maisha yangu… Mungu akiamua kunisamehe siku moja basi..”

Ndugu yangu msamaha wa Mungu upo wakati huo huo unapodhamiria kutubu na kuacha hicho ulichokifanya kutoka moyoni kabisa. Mungu anakuwa ameshakusamehe na anasahau kabisa..

Wewe ndio utabaki unateseka na mawazo yako tu lakini yeye kashaachilia kabisa.

Sasa mbinu kubwa anayoitumia Shetani baada ya hapo ni kuanza kucheza na ufahamu wako tu. Na ndio anapowaweza watu wengi.. Shetani anacheza na mfumo wa akili yako kwa kuendelea kukuambia kuwa wewe (kwa sababu huna ufahamu juu ya Mungu maana husomi neno na kujifunza)“…hujasamehewa. waliosamehewa hawafanyi kama ulivyofanya wewe. Wewe bado ni mwenye dhambi..”

Tena umefungwa na laana za mababu na bibi zako ili uweze kuwa salama omba msaamaha kwa ajili yao na watole sadaka kabisa nenda kwenye makaburi yao kawaombe msamaha…nk”

Na saa hiyo atakuwa ameandaa watu wake mahali na mahali ambao ukishatoka kuwaza mambo kama hayo utasikia hata kwenye radio/Television wanatangaza mambo kama hayo hayo..

Itafikia hatua ataanza kukwambia ibilisi “nyota yako haiko sawa imeibiwa nk” utajikuta anakutaabisha mpaka anafanikiwa kukumaliza kabisa.

Na unapofata yote hayo ndio unavyozidi kwenda mbali na Mungu. Hivyo kuwa makini mno juu ya jambo kama hili.

Unapoona umekosa mbele za Mungu usijione kuwa hufai hata kama umekosa kweli kwa kujua tambua wewe ni mwanadamu unafanya makosa na Mungu anachokiangalia baada ya kufanya Kosa ni wewe kugeuka..

Mungu hatunzi makosa pale unapogeuka na kuiacha njia mbaya ambayo ulikuwa unaielekewa ni furaha kwake na anazidi kukutia mguvu.

2.Mafundisho ya uongo.

Mbinu nyingine hii Shetani anaitumia kuhakikisha anakumaliza kupitia mafundisho potofu. Na anayatoa kwenye biblia kabisa uliyonayo anayapindua tu..

Unaposikiliza mafundisho ya kurudisha nyota,shuhuda za kichawi na kuzimu,mafundisho ya kukomboa ardhi,mara mzaliwa wa kwanza,mafundisho uchumi tu,kuwapiga maadui zako ambao ni wanadamu, mafuta ya upako ili kufukuza majini na mapepo(ndugu pepo au jini halifukuzwi kwa mafuta bali kwa jina la Yesu na inakuhitaji uwe muombaji na msomaji wa neno.. unateswa na majini nk kwa sababu ya ufahamu wako ni mdogo juu ya Yesu Kristo).

Hivyo yako mafundisho mengi sana ambayo hayana kiini cha kukupeleka mbinguni ni kukutisha tu na muda wote ukute unajifikilia kwa Muda mwingi kuzimu kuliko kumtafakari Yesu Kristo. Mwisho wa siku utajikuta unayaota na Shetani anakuwa kashakunasa .

Hivyo kuwa makini na fundisho unalofundishwa au kulisikiliza lina mchango mkubwa wa kukusaidia au kukuharibu kabisa.

Usimpe shetani nafasi na endelea mbele unapoanguka rekebika endelea mbele ndio Kristo anavyotaka kutuona.

Maana kuanguka na kuinuka na kupiga mbio na kutokurudi nyuma ni maisha yako ya kila siku ikiwa umemuamini Yesu Kristo. Na utakapoanguka utaumia na itakuwa ni funzo kwako la kutokurudia makosa.. Bali kuendelea mbele.

Ubarikiwe sana.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *