Unataka kupendwa na Mungu?.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Ni wazi kila mtu katika huu ulimwengu hasa kwa jamii ya watu wanaomwamini Yesu Kristo wanatamani kupendwa na si kwamba Mungu hawapendi la! Mungu hakuna mtu ambae anamchukia hata   mpagani anampenda! Na ndio maana anataka aokoke asiende katika jehanum ya moto.

Lakini jambo ninalotamani tujifunze ama kulitaza kama mtu ulieamini unatakiwa ufanye nini ili upendwe na Mungu yaani ni jambo gani unatakiwa kuwa nalo ili uwe na uhusiano/imara mzuri na bora kabisa na Mungu?.

Kuwa na mahusiano mazuri na Mungu  ni jambo la muhimu sana kwa mtu aliezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyoharibika.

Katika jambo hili watu wengi ukiwauliza watakujibu ukitaka upendwe na Mungu zishike amri zake. Ni jambo la kweli kabisa hili unaposhika maagizo ya Mungu yeye mwenye ameahidi atakuja yeye na Baba wataweka makao ndani yako.

Yohana 14:23“Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.”

Umeona hapo! Kuwa mtu anaempenda Yesu Kristo akalishika neno lake huyo mtu atapemdwa sana. Na Yesu Kristo na Baba watakuja kuweka makao ndani yake. Si kwamba hawapo la!

Lakini jambo ambalo natamani tulifahamu siku ya leo ambalo pia litatusaidia sana kwenye maisha yetu ya wokovu na kila siku kuzidi kumsogelea zaidi Mungu wetu.

Siku ya leo natamani tuyaangalie maisha ya mtu alieupendeza moyo wa Mungu sana naye si mwingine Mfalme Daudi. Maandiko yanaweka wazi ukisoma 1 Samweli 13:14.

Ukisoma pia…

Matendo ya Mitume 13:22“Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.”

Maandiko yanathibitisha  kweli aliupendeza sana moyo wa Mungu.. lakini tukirudi nyuma na kuanza kuangalia maisha ya Daudi tunaona kabisa Daudi alikuwa na mapungufu au makosa mengi lakini kwa nini Maandiko yanasema kuwa alieupendeza moyo wa Mungu?  Tutajifunza jambo kubwa sana juu ya hili litakalotusaidia wote..

Tutatazama kwa ufupi sana baadhi ya makosa makubwa manne ambayo Mfalme Daudi aliyafanya.

1.Kuzini na Bethsheba.

Daudi alifanya uzinzi na mke wa Jemedari wake Uria wakati akiwa vitani na hata mke wa Uria(Bethsheba)akawa na mimba ya Daudi. Soma 2 Samweli 11:2-4.

2.Mauwaji ya Jemedali wake Uria mhiti.

Daudi hakuishia tu kuzini na Bethsheba mke wa Uria lakini pia alifanya njama za kumuuwa uria na jambo hili lilifanikiwa. Soma 1 Samweli 11:14-15.

3.kufanya Sensa.

Daudi baada ya kukaa muda mrefu kidogo bila vita akaagiza askari wote wahesabiwe idadi yao jambo ambalo lilikuwa ni chukizo kwa Mungu . Daudi alifanya sensa bila kuzimgatia kuwa Mungu ndio alikuwa chanzo cha ushindi wa taifa. Hili lilikuwa mj tendo la kiburi na kuonekana kutegemea nguvu za kibinadamu. Soma 2 Samweli 24:10.

4.Kushindwa kuthibiti Familia yake vyema.

Ingawa halikuwa kosa mbele za Mungu lakini lilisababisha maangamizi mabaya katika familia yake na aibu kubwa sana.

Hapa amnoni alimbaka dada wa kambo Tamari( 2 Samweli 13:1-14).

Absalomu anamuuwa ndugu yake kwa kulipiza kisasi baada ya dada yake kubwakwa na kaka yake Amnoni(2 Samweli 13:28-29) lakini baadae tena Absalomu anaasi na kumpindua Daudi madarakani (2 Samweli 15:1-12).

Adoniya Mtoto wa Daudi alijitangaza kuwa mfalme bila ruhusa ya baba yake Daudi.(1 Wafalme 1:5-10).

Hayo ni baadhi yaliyoorosheshwa kwenye maandiko lakini kwa namna gani Daudi aliupendeza Moyo wa Mungu pamoja na Makosa yote hayo?.

Sababu gani ilipelekea Daudi kuupendeza moyo wa Mungu?.

1.Toba ya dhati/kweli.

Daudi alikuwa ni mwepesi sana kugeuka pale anapotambua amekosa alikuwa mwepesi kukiri makosa yake na kubadilika kwa kumaanisha kabisa.

Kipindi Nathani nabii anamwambia kuhusu kosa la kuzini na Bethsheba alikiri na kujutia na geuko la Daudi lilikuwa kutoka moyoni.

Na ndio maana Daudi katika makosa aliyofanya hakuwahi kabisa kurudia kosa hata moja. Kuonyesha Daudi alikuwa anamaanisha katika kile alichokuwa anakiungama mbele za Mungu

Sisi pia Mungu anachotazamia kuona toba ya kweli kwetu yaani geuko kwetu la kweli Mungu anapendezwa sana na moyo wa namna hii unaokiri na kudhamiria kuacha kabisa. Ukisoma Zaburi 51 utaona Daudi anaomba pia aumbiwe moyo mpya. Ni maombi ya Daudi kwa Mungu juu ya yale aliyokuwa ameyafanya.

2.kurejea kwa Mungu.

Daudi hakuwahi kabisa kumkimbia Mungu au kwenda mbali na Mungu. Hakuwahi kufanya hivyo alipokosa alitambua usalama wake ni kwa Mungu pekee.. Daudi alijifunza kumtegemea Mungu hata kama alikuwa na makosa alijua awezae kumfanya upya na kumtengeneza Ni Mungu peke yake hakuthubutu  kumuacha Mungu kama Sauli ambaye alifikia hatua ya kwenda kwa  wachawi.

Alijua msamaha wa kweli si kujitetea kwa watu fulani kama manabii nk ila kwa Mungu pekee tu.

Makosa haya yote ya Daudi na jinsi alivyofanya ilifanya kuimarisha sana uhusiano wake na Mungu hata akaahidi Yesu atatoka katika uzao wake.

Hivyo inatufundisha pia sisi umuhimu wa kujutia dhambi zetu tusifanye dhambi na kuanza kujivuna bali tujutie kabisa. Lakini pia na kutafuta msamaha wa Mungu kama vile Daudi alivyofanya. Siku zote Mungu anaangalia moyo uliotayari kukiri makosa na kurekebika.

Lakini Mwisho kabisa inatufundisha kumtegemea Mungu katika kila jambo licha ya mapungufu na madhaifu yetu tumtegemee yeye. Atatuimalisha na kututengeneza na tutazidi kuwa imara siku baada ya siku na yeye ameahidi tunapomuita anaitika na anatututakasa na kutufanya imara kabisa. Tukiwa na haya mambo ni wazi kabisa tutakuwa na mahusiano bora na Mungu.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *