JE! UMEJULIKANA NA MUNGU?

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

 

Watu wengi sana wanafikiri kujulikana na Mungu ni kwenda kanisani kila siku,kufanya matendo mazuri, kuomba kila siku, kuwaombea watu na watu kupona,kutoa mapepo,kunena kwa lugha,kuona maono na kusikia sauti ya Mungu nk.

Mambo haya ni mazuri lakini hayakufanyi kujulikana sana na Mungu katika ule uhalisia wenyewe ambao Bwana anatamani tujulikane nae kwake. Yako mambo baadhi ambayo ikiwa mtu akiyafanya ama akiwa nayo ndani yake kweli kweli basi huyo mtu anakuwa amejulikana kweli kweli na Mungu.

Sasa tuyatazame maaadiko ili tuyafahamu haswa ni mambo gani yanayofanya tujulikane sana na Mungu.

1 wakorintho 8:3 “Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejulikana naye.”

 

Mstari huu umebeba siri kubwa sana ndani yake kama tukiusoma juu juu tu tunaweza tukauchukulia ni kawaida tu, lakini sivyo tutautafakari kwa kina na kwa undani zaidi ili tuelewe zaidi kw undani wake.

 

MAMBO MAKUU  MATATU YANAYOFANYA UJULIKANE NA MUNGU.

Kama mstari hu hapo juu unavyosema kwamba “Lakini Mtu AKIMPENDA MUNGU…..”  Sasa tunapomwamini Yesu Kristo ndani yetu huwa anaweka kitu ambacho kinatufanya tumpende hata pasipo kulazimishwa na jambo hili linawekwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani yetu.

 

  1. Heshima na upendo wa dhati kwake.

Mtu mweye heshima na upendo wa dhati tena pasipo kulazimishwa(anaejitoa kwa ajiri yake) kwa Mungu ni mtu anaejulikana nae sana. Unapokuwa mtu mwenye kuliheshimu neno la Mungu na kutokulichukulia kawaida. Unapolichukulia kwa uzito neno lake na kuliheshimu(maana ndio yeye mwenyewe na ndio uzima wenyewe na tumaini kwetu maana hakuna mahali tunapata tumaini na furaha ila katika neno lake).

Daudi anasema..

 

Zaburi 199:97 “Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.”

 

Daudi alikuwa na upendo wa dhati kwa Mungu na ndio maana hata alipokosea hakudhubutu kurudia kosa kabisa na aliupendeza moyo wa Mungu kwa sababu alimpenda Mungu kwa upendo wa dhati.

 

  1. Utii wa haraka bila kusita sita au kuchelewa.

Mungu anapendezwa sana na mtu anaeisikia sauti yake na kuitii pasipo kusita sita tena kwa haraka pasipo kujiuliza uliza itakuwaje. Mtu wa namna hii anakuwa anajuilikana sana na Mungu. Utii una thamani sana mbele za Mungu kuliko hataa sadaka. Lakini ikiwa hatuitiii sauti yake tunafanya tunayotaka na tunaponya wagonjwa, tuna nena kwa lugha nk ikiwa hatuitii sauti yake yeye/maagizo yake ambayo wakati mwingine tunayaona ni ya kawaida tu hapo tunakuwa hatuajulikana nae.

 

mambo unayoyachukulia ni ya kawaida kwako ni tofauti na Mungu jinsi anavyoyachukulia” na siku zote maagizo ya Mungu yapo katika hali ya kawaida sana ambayo Mtu anaweza akayachukulia kwa juu juu tu lakini sivyo.

 

Mungu anathamini sana utii kama anavyosema katika neno lake…..

 

1 Samweli 15:22 “Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? ANGALIA, KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu”

 

Hivyo kutii amri za Mungu bila kuchelewa hii inaonyesha kuwa tunamwamini na tunamdhamini kwa moyo wetu wote” maana utii wa haraka unaonyesha unaimani nae yeye.

 

Mungu anapendezwa sana na shukrani za dhati kwa mtu Yule anaetambua Baraka za Mungu katika maisha yake. Mtu anaetambua Mungu ndio chanzo cha baraka zote na kumshukuru kwa kila kitu anachopokea huyu ni mtu anaejulikana sana nae. Tusiwe ni watu wa kulalamika na kunung’unika.

 

Maandiko yanasema pia….

 

Wakolosai 3:15  “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.”

 

Hivyo  wale wanaompenda Mungu kwa namna hii, wanajulikana sana na Mungu maana Mungu anawatambua na kuwatazama kama watu wenye thamani sana na ambao pia wanastahili kuwa haribu naye, hivyo Mungu anawajua si kwa jina pekee tu bas, bali anajua mioyo yao, na awapenda kwa namna ya kipekee. Na hii inaonyesha dhahiri watu wa namna hii Mungu anamiliki maisha yao kwa sababu wamejitoa kwake yeye kikamilifu pasipo kujali kitu chochote kile.

 

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *