Lifanye Neno la Mungu kuwa tiba ndani ya roho yako na mwili wako.
Shalom, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Zaburi 107:20
“Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.”
Neno la Mungu ni tiba kwa mwanadamu(maana aliumbwa kwa hilo yaani Neno la Mungu/Mungu mwenyewe) ni neno ambalo limebeba kila kitu anachokihitaji mwanadamu anachokijua na asichokijua vyote kwa pamoja viko ndani yake na Neno hili kama mtu atatamani kuwa tiba kwake basi itakuwa na litamponya.
Neno la Mungu ni hai na tena lina nguvu..
Waebrania 4:12
“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”
Ni neno ambalo sio hai tu lakini lina nguvu(nguvu iliyouumba huu ulimwengu, iliyowatoa wana wa Israeli utumwani, nguvu ya Msalaba yaani msamaha wa dhambi,wokovu nk) vyote hivi viko ndani ya Neno la Mungu ikiwa utaliamini na kulifanya liwe halisi katika maisha yako haya yote utayaona hivyo hili Neno sio hadithi tu au maandishi kama maandishi mengine!.
Sasa kwa nini Neno la Mungu ulifanye tiba ndani yako? Kwani una ugonjwa wowote?
Jibu ni ndio kama watoto wa Mungu kuna magonjwa ya rohoni mengi tunayo na hayo hayatoki kwa kujifariji au kwa kufundishwa tu peke yake bali inahitajika nguvu iliyoko ndani ya Neno kwa kukaa na kulitafakari na kupata ufunuo utakao sababisha tiba ndani ya roho/nafsi yako.
Na magonjwa hayo ni yapi?.
Ni mengi lakini machache nitayaorodhesha tu wala sitayaelezea ikiwa kuna lolote lipo ndani yako basi anza kulifanya Neno la Mungu kuwa tiba katika maisha yako itakusaidia sana.
Magonjwa hayo ya rohoni ni Hasira, wivu,chuki,tamaa mbaya,uchungu,fitina,faraka nk, mambo yote au tabia zote za mwilini yote ni magonjwa ya rohoni..
Unapoona ndugu yako kafanikiwa,au ana karama fulani,au amefanya jambo zuri na watu wanamtukuza Mungu kwa ajili yake wewe unaingiwa na wivu,chuki, na kwa nje unaonekana sawa tu lakini ndani huko panachemka.
Hutaki kuona wengine Mungu akiwatumia kwa namna mbali mbali wakati mwingine unachukia ndugu yako katika Kristo unamuona anajiona sana yeye ndio yeye na hata hayupo kama unavyomfikiri ndugu hayo ni magonjwa ya rohoni na yanasababisha uwe mgonjwa ndani na yanakuweka mbali sana na Mungu.
Utakuwa unaomba unona kweli Mungu anakujaza nguvu zake unapoomba nk lakini ndugu yangu hutakaa umuone Mungu kabisa..
Sasa haya hayatoki kwa kuombewa tu au kwa kuomba tu, wakati mwingine hutaki iwe hivyo lakini inatokea ni kwa sababu Neno la Mungu hujataka kulifanya kuwa tiba katika roho yako au hujajua namna ya kufanya..
Maandiko yanasema….
Wakolosai 3:16
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.”
Unaona hapo? Hasemi “Mistari ya Biblia ikae wa wingi ndani yenu” bali Neno la Kristo likae kwa wingi Mistari ya biblia Wakristo wengi tunayo lakini si wote Neno la Kristo linakaa ndani yetu.
Neno linapoanza kukaa ndani yako utaona linaanza kukufundisha hata utakapoona wivu,hasira nk hilo litakufundisha ndani yako unapotafakari kwa nini nakuwa hivi Neno litakuja na kukupa sababu zote kwa nini hutakiwi kufanya hivyo na Neno lenyewe litafanya kazi ya kuondoa huo uchungu au chochote kile..
Neno la Mungu lina nguvu ya ajabu mno kazi yako kubwa ni wewe kulifanya kuwa hai ndani yako kwa kusoma sana biblia na kuwa na matamanio ya kubadilika na kisha kuwa mtu wa kutafakari na kuwafundisha wengine utaanza kuona nguvu ya Neno inaanza kufanya kazi ndani yako.
Hivyo ikiwa Neno litaanza kukuponya ndani na nje pia kutaonyesha matokeo makubwa na mazuri zaidi hiyo inachangia/kusababishwa na kuponywa ndani..
Anza kuwafundisha wengine, kusoma biblia na kuomba kwa bidii utabadilika kabisa siku baada ya siku tiba ni Neno wala si kusema ipo siku nitakuwa sawa.. hapana.
Mithali 4
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.21 Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.
Ubarikiwe sana.
Mawasiliano:0613079530.
@Nuru ya upendo.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.