Mhunzi ni nani? (Isaya 54:16)

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom,

tusome pamoja katika kitabu cha Isaya 54:16

Isaya 54:16 “Tazama, nimemwumba MHUNZI avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu”

Mhunzi au wahunzi wanaozungumziwa hapa ni wanaofua vyuma, fedha, shaba, au Dhahabu. Ikimaanisha wanaviyeyusha vyuma au madini husika katika maumbo mbalimbali kutengeneza silaha au Urembo.

Sasa utofauti kati ya mhunzi na mfinyanzi ni hii..

Mfinyanzi hutumia udongo kutengeneza vyombo au zana mbalimbali mfano unaweza kupitia zaidi (Isaya 41:25, Isaya 64:8 na Yeremia 18:6)
Mhunzi hutumia vitu jamii ya metali mfano fedha, Dhahabu, chuma au shaba kutengeneza silaha au vito au zana katika kazi Fulani.
Mistari mingine katika biblia inayozungumzia wahunzi ni kama ifuatayo ( 1Samweli 13:19, 2Wafalme 24:16, Isaya 44:12, Isaya 46:6, Yeremia 24:1, Zekaria 1:20, Matendo 19:24, na 2Timotheo 4:14.)

JE umempokea Bwana Yesu maishani mwako?
Kama bado basi fahamu kuwa upo katika hatari kubwa ya Mwisho mbaya; sote twajua hakuna nafasi ya kutubu uwapo kaburini, Nafasi unayo Sasa mpokee Leo awe Bwana na Mwokozi wa Maisha yako.

Na Mungu atakubariki sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *