Wagerasi ni nchi gani?

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Wagerasi ni watu waliokuwa wakiishi katika mji wa Gerasi, Kusini mashariki mwa Bahari ya galilaya. Ilikuwa ni moja ya nchi ya Dekapoli iliyokuwa ya watu mataifa.

Tunaona ni kule Yesu aliko kutana na aliyekuwa na kichaa kikali akamponya..

Marko 5:1-3

[1]Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.

[2]Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;

[3]makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 

JE sisi Tujifunze nini kutoka kwa wagerasi?

Wagerasi walithamini sana Mali, Utajiri na kufunguliwa kwao, tunaona wanapogundua nguruwe wamekufa wote walimsihi Yesu aondoke kwa hofu ya kuhisi angesababisha hasara zaidi.

Unaona, hawakuuona ule wokovu uliowafikia, Bali waliona mabaya tu, jambo hili si jema kabisa

Maranatha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *