Itengeneze tabia ya Mungu ndani yako.

Biblia kwa kina No Comments

Itengeneze tabia ya Mungu ndani yako.

Shalom,  Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Mwenye jukumu na wajibu wa kufanya tabia ya Mungu iwe ndani yako yaani uwe kama Mungu jinsi alivyo ni wewe”

Kupokea Roho Mtakatifu haimaanishi unayo tabia ya Mungu ndani yako,  kuwa na karama ikiwa ni unabii,Neno la hekima,nk vyote hivi havimaanishi unayo tabia ya Mungu ndani yako la!”

Unaweza ukawa na vitu vyote lakini bado isiwe kitu mbele za Mungu kama utakosa kufanana na yeye au kuwa na tabia yake ndani yako.

Na tabia ya Mungu/asili ya Mungu ni nini yaani uhalisia wa Mungu.  Maandiko yanaweka wazi…

 

1 Yohana 4:8“Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.”

Unaona hapo anasema “Mungu ni upendo” hasemi “Mungu anaupendo” mwandishi huyu huyu anasema..

1 Yohana 4:

16“Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.”

Umewahi kulitafakari hili andiko? “Yaani anaekaa katika pendo huyo mtu anakaa ndani ta Mungu,  na si hivyo tu bali Mungu pia hukaa ndani yake..”

Hamaanishi kwamba mtu asiyekuwa na upendo ndani yake basi Mungu hakai ndani yake la! Bali huyu Mtu hajamjua vyema Mungu, hana mahusiano ya karibu na Mungu.

Kwa lugha ya kiingereza ni INTIMACY maaa yake ni Intimacy with God means having a deep, personal, and close relationship with Him. It is not about religion or routine, but about walking with God daily, knowing His heart, hearing His voice, and responding to His love with trust and obedience..

Maana yake..

hali ya kuwa na uhusiano wa karibu sana, wa ndani na wa binafsi na Mungu. Si suala la kufanya ibada kwa kawaida tu, bali ni mahusiano ya moyo kwa moyo, mahali ambapo unamjua Mungu kwa undani na Yeye anajifunua kwako.

Ni hali ya ndani mno kwa namna nyingine.

Ni hali ya kutembea na Mungu kila siku, kusikia sauti yake, kuelewa mapenzi yake, na kufurahia uwepo wake hata bila kuomba chochote.

Na hii ni kwa kila mtu kama utaamua kuanza kutengeneza mahusiano ya karibu sana na Mungu.

Sasa ikiwa Mungu ni Upendo je upendo ni nini hasa? Na kama tunaomba upendo basi ni nini tunapaswa kufahamu??

Upendo ni hali ya ndani ya moyo ya kujitoa kwa mwingine kwa hiari(bila kulazimishwa), kwa nia njema(sio kwa kujionyesha), kwa uaminifu, na kwa unyenyekevu bila masharti, chuki, wala kutegemea kurudishiwa.

Hii ni katika hali ya kawaida lakini upendo wa Mungu ambao tunapaswa kuwa nao ndani yetu kwa kufanya bidii sana ni ….

Upendo wa Ki-Mungu ni tabia ya Mungu ya kujitoa kwa ajili ya wengine bila masharti, hata kwa wale wasiofaa, kwa njia ya rehema, neema, msamaha, na uvumilivu usio na mipaka.

 

Sasa sifa za upendo tunazipata katika kitabu cha 1 Wakorintho 13:4-8 mwandishi ameelezea kwa kina sana upendo ni nini!?

 

1.Upendo hauhesabu mabaya.. ikiwa unataka upendo wa Ki-Mungu uanze kuumbika ndani yako kwanza kabisa usiwe mtu wa kuhesabu mabaya kwa watu kwa namna yoyote ile JIFUNZE  na inahitji muda na maombi sana na kuhitaji msaada wa Mungu.

Usiwe mwepesi wa kuangalia makosa kuwa mtu wa kuangalia yaliyo mema tu, kawaida ya mwanadamu ni kuangalia makosa lakini kuanzia sasa kataa kuwa mtu wa hivyo unapoanza kuangalia makosa ya watu rudi kwenye hilo andiko je huo ni upendo utagudua sio Neno litaanza kukutengeneza kuna furaha ya ajabu mno kutokuhesabu makosa.

Na hapo unakuwa kama Mungu yeye hahesabu makosa kabisa.

2.Upendo huvumilia..

Anza kujifunza kuvumilia hili jambo haliji tu basi lazima uanze kuchukua hatua mahali ambapo unakosa uvumilivu huenda kwa watu wanaokuudhi,huenda katika eneo lolote anza kujifunza na tamani hiki kitu kiwe ndani yako.. Mungu yuko ndani yako lakini haya mambo ili yaonekane lazima uingie kwenye utendaji kazi .

Ukristo sio maneno Ukristo ni vitendo.

3.upendo hauhusudu

Maana ya “ kuhusudu/husudu” wivu. Na katika eneo hili wivu unaozungumziwa ni pale unapoona ndugu yako katika Kristo anafanikiwa aidha kapata kazi/mke,nk hii ni tabia ya Mungu haoni wivu kwa mwanadamu juu ya mafanikio yake au alichonacho.

Vivyo hivyo na wewe jitahidi sana kukataa hali hii unapoanza kuona wivu rudi kwenye maandiko je huu ni upendo au ni tabia mimi kama mtoto wa Mungu napaswa kuwa nayo?.

Kwa muda wako ikiwa unataka tabia ya Mungu hii iingie ndani yako tumia muda wako vizuri kutafakari na kuanza kufanyia kazi utaona hili jambo linawezekana na kunaamani utaanza kuiona ndani yako na hutakuwa mtu tena wa Mashindano nk.

Kanisa la leo limekuwa na Mashindano kwa sababu hakuna upendo huu ndani ya watoto wa Mungu.

Mwandishi anamlizia kwa kusema..

 

1 Wakorintho 13:13“Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.”

Anasema lililo kuu ni “UPENDO” unaweza ukawa na hayo yote mawili lakini kama ukikosa hili la tatu wewe si kitu hata ufanye nini. Iwe unafundisha kwa ufasaha sana,unanena kwa lugha sana,unatoa unabii sana na wa kweli kabisa,  unaona maono ya Mbinguni,  unasikia sauti ya Mungu,  unaomba sana nk kama huna upendo wewe ni kama shaba iliayo na upatu uvumao.

 

1 Wakorintho 13

1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

Omba maombi haya mafupi.

Baba Yangu ninaomba unijaze upendo wako ndani yangu, sitaki kuwa mtu wa kuhesabu mabaya kama jinsi ulivyo wewe Yesu, sitaki tena kuwa mtu wa kujivuna,wakuona wivu,nk ninaomba nikiamini ni katika Jina lako Yesu Kristo Ameni”.

@Nuru ya upendo.

Mawasiliano: 0613079530

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *