MAOMBI YA MFUNGO

Maombi na sala No Comments

MAMBO UNAYOPASWA KUYAEPUKA KATIKA MAOMBI YA MFUNGO ILI UWE NA MAOMBI YENYE MATOKEO.

Tutatazama mambo baadhi ambayo tunapaswa kuyaepuka kipindi ambacho tutakuwa katika Maombi ya mafungo, ili tuwe na  maombi yenye MATOKEO…

1. KUFUNGUA BILA KUOMBA
Ukiwa katika kipindi cha mfungo kisha ukamaliza maombi yako labda ya masaa 12, 24 nk, na huku ukiwa ujachukua hatua yeyote ya kuomba, hapo utakuwa umeamua kushinda na njaa basi hakuna lililotendeteka katika roho yako, ndiyo maana unapaswa uhakikishe unapata mda wa maombi, usisubirie au usiwe makini kusubiri mda wa kufuturu tu, FUNGA NA OMBA

Matendo ya Mitume 13:2-3

[2]Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.

[3]Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

2: KUFUNGA BILA KUSAMEHE WENGINE
Epuka kuingia maombi huku ndani yako, yaani ndani ya moyo wako una uchungu una hasira na mtu fulani, labda kwa sababu ya jambo fulani usianze maombi ikiwa kama ujasamahe, acha kabisa  maombi ya mazoezi na desturi jitahidi kufata kile BABA YAKO ANAKUELEZA, yeye unayempelekea hoja anataka uwe na moyo ambao umesamehe na umeachilia ili maombi yako yapate kibari na majibu,  jitahidi sana   ndani ya moyo kuwa na AMANI wala huna mtu ambaye umembebelea, bali mbebe YESU WAKO uwe naye moyoni ili maombi yako yawe harufu nzuri mbele za Mungu..

Marko 11:25-26

[25]Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [

[26]Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]

3 KUFUNGA HUKU UNAENDELEA KUTENDA DHAMBI
Ukijizoesha akili na mwili wako kuchukulia mambo ya rohoni ya kawaida tu na kuona unaweza kufanya unavyojisikia au kufanya lolote  tu, tambua hata maisha yako yatakuwa ya kawaida hivyo hivyo utafunga lakini hutaona badiliko lolote. Tunafunga ili kufungua kamba za nira zinazotuzuia kuona wema wa Mungu, sasa ikiwa kama una maombi yako alafu unaendelea na dhambi fulani, ni sawa kumdharau Mungu, takasa saumu yako, hii ni sehemu ya kutengenezwa na mwenye hekalu lake nyenyekea acha mazoea shetani hana mchezo na mtu yeyote kabisa, ukimpa nafasi anakumaliza hata kama upo kwenye maombi ya mfungo.

Isaya 58:3-6
[3]Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
[4]Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
[5]Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?
[6]Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

4. KUFUNGA BILA KUWA NA LENGO MAALUMU
Lazima uwe na lengo au kusudi la kufunga, je unafunga unataka nini kifanyike, pengine labda unatamani huduma yako uongozwe na Bwana, kuombea Taifa na uongozi wake, mwenendo wako, familia yako, kazi yako au mahusiano nk. Haya ndiyo malengo au makusudi, ambayo unaweza ukawa na moja au mawili ili kumpelekea Mungu hoja, usifunge kwa sababu unataka kufanya diet, au kwa sababu umeona chakula kilichoandaliwa huwa ukipendi hivyo ukaamua ufunge, hapo ndugu utakuwa  haujafunga, hakikisha unakuwa na lengo hii inasaidia sana katika Maombi soma habari ya watu wa ninawi

Yona 3:5-6,9-10

[5]Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.

[6]Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.

[9]Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?

[10]Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.

5. KUFUNGA ILI UONEKANE MBELE ZA WATU
Kosa ambalo litakufanya kuwa wa kawaida siku zote katika wokovu wako, ni kuwa na bidii katika kufunga ili tu kutaka watu fulani, au kiongozi wako akuone wewe ni hodari wa mifungo sana, hilo ni kosa maana siyo tabia ambayo  MUNGU anataka kwako bali   anachotamani aone kwako funga huku yeye mwenyewe akuone siyo ujionyeshe mbele za watu

Mathayo 6:16-18
[16]Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
[17]Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
[18]ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

6.KUFUNGA HUKU UKIWA NA MASHAKA NA HOFU
Jambo ambalo linatesa watu wengi sana, hata mimi kuna kipindi nilikuwa mmoja wapo wa kundi hili nilikuwa nafunga kweli na kuomba lakini ndani  yangu nilikuwa SIAMINI kabisa, hili ni jambo mbaya sana ambalo Mungu apendezwi nalo,  lazima tujue mbinu za shetani maana hapa yeye hutumia sana silaha hii ya hofu ili kukudhoofisha uone kama Mungu hawezi chochote ili uanze kumtengemea yeye shetani, hivyo ni kitu cha kukizingatia sana, hakikisha kabisa unapokuwa katika maombi MAWAZO YA KUSHINDWA YAKEMEE ALAFU INUA IMANI YAKO UTAONA MATOKEO….

Yakobo 1:6-8
[6]Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
[7]Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
[8]Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

Waebrania 11:1

7.KUFUNGA BILA KUSOMA NENO NA KULITUMIA
Usifunge alafu unakuwa bize na mambo yako au shughuli zako, Lazima uwe na mda wa KUSOMA NENO NA KUTAFAKARI maana huko huko Mungu atakupa mafunuo kuhusiana na yale mahitaji yako, kufunga bila kusoma neno nako ni sawa na gari bila mafuta utachoka na utaona MAOMBI NA MATESO NA MZIGO kwako, hakikisha unatafakari, tunamuona hata danieli aliweza kufahamu hesabu ya miaka 70 ya kuutimiza ukiwa ya Yerusalemu, wakati alipo kuwa katika kusoma na kutafakari. nawe leo badilisha mfumo wa maombi yako
Danieli 9:1-12

NI MAOMBI YANGU MUNGU AKUPE HATUA NYINGINE NA AKILI NJEMA KATIKA KUMUELEWA MUNGU ILI UJUE KANUNI ZAKE NA UISHI KWA KUONA MATOKEO..

ZINGATIA HAYO NA MENGINE ZAIDI AMBAYO ROHO MTAKATIFU ATAKUFUNDISHA
UBARIKIWE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *