MADHARA YA KIBURI KATIKA MAISHA YA MWAMINI

Biblia kwa kina No Comments

MADHARA YA KIBURI KATIKA MAISHA YA MWAMINI

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tuyatafakri maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

Ikiwa tunatamani kutembea na Yesu na kumuelewa sana kama watakatifu inatupasa kuwa ni wanyeyekevu, watu tusio na kiburi(kujiinua) tofauti na watu wanavyofikiri kwamba kiburi ni muonekano  wa nje jinsi alivyo.

Labda jinsi anavyoonekana, labda hataki kuchangana na watu wengine ana mipaka yake Fulani lakini sivyo hivyo kiburi sio muonekano wa nje.

Huenda hali unayoipitia ni kwa sababu ya jambo hili tutaona huko mbele…

Bali kiburi ni hali ambayo iko ndani ya moyo wa mtu, haiwezi kuonekana kwa macho, mtu anaweza akaonekana kwa nje ni msikivu, ni mtaratibu lakini kumbe ndani ana kiburi(kujiinua) kiburi ni namna unavyowachukulia watu na watu ndani ya moyo wako sio kwa namna inayoonekana kwa nje na kuwashangilia kinafiki.

Tafsri ya kiburi ni “tabia ya kujiona bora kuliko watu wengine, kujivuna, na kuwadharau wengine”.

nje mtu anaweza kuonekana anawaheshimu watumishi wanapofundisha nk lakini ndani anajina na kusema “ mimi nina maarifa kuliko yeye, anachosema nakijua wala hakinihusu, hana mafunuo ya kutosha wala haombi kwa ,muda mrefu, mafundisho yake ni ya kawaida hata hayana mguso wowote ni kawaida tu nk”

Wakristo wengi tuna kiburi/kujiinua pasipo sisi wenyewe kujua halafu tukiona mtumishi Fulani tunasema “mimi siwezi Kwenda kusali wala kusikiliza mafundisho ya mtumishi Fulani, anajiona sana anajiinua, anakiburi nk” lakini kabla hujamnyooshea mkono na kabla hujasema juu ya mtu Fulani jitathimini kwanza wewe je uko sawa?

Je? Hakuna mtu unaemdharau? Hujioni bora kuliko wengine? Ndani ya moyo wako unamuonaje mchungaji wako? Mama mchungaji wako?, washirika wenzako? Wanaofanya usafi vyoo vya kanisani na kudeki kanisani? Je unawachukuliaje? Wale ambao wanarudia nguo ile ile na viatu vile vile kila jumapili? Vikao unavyokaa kuwasema wenzako unawasema katika mazuri Nk??

Tutaangalia kwa uchache sana madhara ya kiburi katika maisha ya mwamini na baada ya kuona hayo basi ikiwa kuna kasoro yoyote unaona ndani yako anza kufanya hatua za kumhitaji Mungu abadilishe maisha yako maana hao unaowadharau ndani ya moyo wako pengine ndio wanamashauri bora Mungu kaweka ndani yako ili wakusaidie unatamani kupiga hatua Fulani lakini hao unaowadharau ndio wana majibu ya kufanikiwa kwako na kama utaendelea hivyo hivyo basi uwe na uhakika hautapiga hatua kabisa.

MADHARA YA KIBURI

1. Kiburi kinazuia kumsikia Mungu.

Kiburi katika maisha ya Mkristo ni kikwazo kikubwa katika maisha ya mwamini katika kumsikia Mungu na kutokumsikia Mungu kunapelekea uangamivu katika maisha ya mtu. Kwa sababu Mungu anatumia watu kufikisha ujumbe asilimia 80% Mungu anatumia watu asilimia zilizo bakia hutumia huenda Malaika nk ila kwa sehemu kubwa
Mungu anasema na watu kupitia watu. Moyoni mwako ukimdharu/ukiwa na kujiinua ndani yako ukajiona kuwa ni bora kuliko mwingine tafsiri yake hata kile anachokisema hutakisikiliza kwa sababu unajiona una Hekima kuliko yeye, maana yake Mungu atakaposema na wewe kupitia mtu huyo utashindwa kusikia kile ambacho Mungu anakisema kuhusu maisha yako, hutakuwa makini hata kumsikiliza matokeo yake utaangamia kabisa.

Mithali 18:12 “Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.”

Unaona hapo? Kabla ya uharibifu kuja moyo wa mtu hujivuna/kujiinua kuona kila kitu anakifahamu hana haja ya kusikia kitu, ni kwa sababu ananena kwa Lugha, anaona maono, anatabiri nk.

2. Kupingwa na Mungu(Mungu kuwa kinyume naye).

Umewahi kufikiri kiwa Mungu atakuwa kinyume na wewe na mimi ni nani anayeweza kunitetea au kukutetea?

1 Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.”

Unaona hapo “… Mungu huwapinga wenye kiburi …”  kama Mungu akiwa kinyume na wewe usalama wako uko wapi? Tumaini lako na langu liko wapi? Yeye Muumbaji wa kila kitu na mkombozi wa mimi na wewe nk huyu kama akikupinga akiwa kinyume na wewe kuna mahali popote utafika? Kiburi ni kitu ambacho Mungu anakichukia sana.

Kumbuka kiburi ni hali(state/condition) ya moyo sio muonekano wa nje kata namna yoyote ya kiburi ndani yako jifunze kuwaheshimu watu wote. Muombe Mungu akusaidie.

Kama ni msomaji wa biblia unaweza kuona Habari ya Mfalme wa dunia kipindi hicho Nebukadnezza alijitukuza, akaona hakuna mwingine zaidi yake anajiamulia kufanya anayotaka japokua Danieli alimuonya lakini hakusikia na matokeo yake alishushwa kutoka kuwa mfalme mpaka kuishi msituni na kula majani.

4.Mungu huwashusha wenye kiburi (kuwa kinyume nao)

Ukipata muda pitia kitabu cha Danieli sura ya 4 yote kuna jambo la kujifunza nitaweka mistari michache tu..

Danieli 4:33-37 ” Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.

[34] Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;

[35] na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?

36 Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.

37 Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.”

Huenda kuna mahali upo na hujui ni kwa nini upo, unapitia mazingira magumu nk si kwamba shetani lakini huenda ulijiinua na kuwadharau wengine na Mungu akakushusha omba Rehema mbele za Mungu naye atakurehemu na kukurejesha kama alivyofanya kwa mfalme Nebukadneza

  1. MAOMBI YA TOBA
    Baba yangu naomba unisamehe, unirehemu, pale nilipojiinua,nilipowadharau wengine pale nilipofanikiwa nilipopiga hatua nikajiona kuwa ni bora naomba unirehemu na kunitakasa, uniondelee kiburi,majivuno ninashukuru kwa kuwa umenisamehe na kunirejeshea tena nafasi niliyoipoteza ni katika jina la Yesu Kristo Amina”

Mungu akubariki sana
Maranatha
@Nuru ya upendo
Mawasiliano 0613079530

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *