Shalom, Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Yohana 12:35 ” Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.”
Jibu: katika maisha yake hapa duniani Bwana Yesu alijilinganisha na Nuru ya Ulimwengu huu(Jua); na alisisitiza hili sana katika mafundisho yake, Lakini hawakumwelewa(Yohana 11:9,10)
Sasa kwa uelewa wa kawaida kuhusu jua ni kuwa halizimi, halitulii sehemu moja litachomoza, litazama, wakati Nuru Yake inaangaza upande mmoja, mahali pengine ni giza! Na Mizunguko yake itaendelea hivyo.
Kwa habari ya wayahudi kuna waliompokea, waliomwonea wivu, na kumwita mchawi n.k lakini hawa wote neema ya Yesu Kristo ilikuwa juu yao mithili ya Vifaranga vya kuku chini ya mbawa zake (Luka 13:34); Wala hakuthubutu kuwahubiri Mataifa ambao wangalimfanya hata mfalme wao, pamoja na kumpinga kwao vikali.
Ndipo anawaambia wayahudi Jambo hili halitaendelea sana, Bali kuna wakati Nuru hii itawaangazia na Wengine..
Yohana 12:35 ” Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.”
Anapowaambia haya alimaanisha Kuwa Waamini mapema maana nguvu Ile iuguayo mioyoni mwao itaondoka, watakapoikataa neema na kujazwa Roho mtakatifu hakika hawatalishinda Giza kwa nguvu zao.
Haya yote ni kweli, Tunaona mda mfupi baada ya kufa, kufufuka na kupaa injili ilianza kuwaendea mataifa (Mimi na wewe)
Imeshapita miaka 2000 tangu mitume, lakini bado wayahudi hawajafumbuliwa Macho kuamini wokovu.
Leo Mataifa tunayo injili au Nuru, Sasa kanuni ya Nuru ni ileile Huzunguka, basi hata kwetu pia Haitodumu.
Mungu aliahidi Mwisho utakaookaribia (Ambao ndio huu)Atairudia tena Israel kwa muda mfupi, hivyo Neema haitokuwa nasi mataifa Tena!..
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.”
Mwokozi atakuja kutoka Sayuni;
Nae Atamtenga Yakobo na maasia yake.
Mwokozi haneni na wayahudi pekee Bali nasi sote..
Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako
JE unaenenda katika Nuru? Kama bado wangoja Nini mpendwa, Mgeukie Yesu Leo bila kufanya hivyo hutolishinda Giza kamwe!
Maranatha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.