KWANINI MAOMBI
Nakusalimu katika jina tukufu, jina la Bwana Yesu Kristo Mfalme wa Wafalme na BWANA WA MABWANA.
Karibu tujifunze hekima ya Mungu, Neno la Mungu ambalo ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu (Zab.119:105).
Leo kwa neema za Mungu tutajifunza somo zuri linalohusu maombi. tutaangalia maana ya maombi na ni kwanini tuombe. hivyo nakusihii fuatilia somo hili kwa umakini mpaka mwisho naamini utaongeza maarifa katika eneo lako la kiroho.
Maombi ni nini?
Neno maombi limetokana na neno kuomba, Kwamfano mtu unapokuwa na hitaji ya kitu Fulani, labda tuseme kazi, basi huwa unatuma maombi yako kwanza kwenye ofisi husika au shirika, kisha wanapitia wasifu wako na kule wakisharidhiwa na maombi yako ndio wanakurudishia majibu ya kile ulichokiomba.
Kamwe huwezi ukapeleka maombi ya kazi, halafu yakarudi majibu ya mkopo, ya ufadhili, au ya kupewa bima badala yake..Hilo jambo halipo, kwa namna ya kawaida chochote kile unachokiomba ndicho utakachopewa, ukiomba ajira utarudishiwa majibu ya ajira, ukiomba mkopo utarudishiwa majibu ya mkopo, ukomba zabuni utarudishwa majibu ya zabuni, kamwe haiwezi ikavuka hapo.
Kwanini maombi?
Maombi ni kama maji, kamwe haiwezekani kiumbe yeyote anayepumua kuishi bila maji, vivyo hivyo na maombi pia ni sehemu ya kila kiumbe hai, jambo ambalo yamkini watu wengi hawafahamu ni kwamba hata viumbe vingine kama ndege, wanyama, n.k huwa wanapeleka maombi yao kila siku kwa muumba wao, Biblia inatuambia hivyo.
Ayubu 38:41 Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutanga-tanga kwa kutindikiwa na chakula?
Sasa kwanini maombi? Ni kwasababu ndiyo njia Mungu aliyoichagua kwa viumbe vyake kuwapatia mahitaji yao..kwamba lazima waombe japokuwa anajua kwamba wanahaja na hayo ila anataka aombwe (maombi ni ishara ya unyenyekevu), Mungu anataka unyenyekevu.
Pia maombi sio kupeleka mahitaji tu, ni zaidi ya hapo, maombi ni mawasiliano kati ya Mungu asiyeonekana na viumbe vyake kwa njia ya Imani. Kama vile uhai pasipo maji haiwezekani kuishi, vile vile maisha bila maombi huwezi kufanikiwa.. maana utahitaji tu kuwasiliana na yule mwenye nguvu ya kukusaidia.
Na ndipo hapo unakuta maombi ya watu yanatofautiana kulingana na yule anayeombwa.
Kama tulivyosema, huwezi kufanikiwa pasipo maombi, vile vile huwezi kuwa salama bila kuomba, katika kuomba kuna kuomba ulinzi, kuna kuomba usalama n.k
Itakuwa ni ajabu sana kama huombi! unawezaje kuishi, unawezaje kuwa salama, kama kunguru anamlilia Mungu wake kila siku ili apewe mahitaji yake..wewe imekupasaje?
Lakini swali, ni je maombi yako unapeleka kwa Mungu yupi? Maana hata shetani naye mandiko yanatuambia ni mungu wa ulimwengu huu.
Usidhani kuwa wale watu wanaokwenda kwake na kupeleka mahitaji yao, hawana akili, wametambua umuhimu wa maombi kwamba bila kwenda kwa huyo mungu wao (shetani) hawawezi wakatoboa, bila kupeleka kafara na kuwasilisha maombi yao hawawezi kuwa salama.
Na ndio hapo utakuta mwingine anaenda kwa waganga wa kienyeji, na mwingine kwa waganga wa kisasa (manabii wa uongo), na mwingine kwa miungu yake labda ni mti, au jiwe, au sanamu ya mtu fulani anayedhaniwa kuwa ana nguvu za rohoni, au wengine wanachonga sanamu ya kitu fulani ndiyo mungu wake anamwomba.
Sasa hao watu wote wanaye muomba ni mungu mmoja tu ambaye ni shetani mwenyewe, isipokuwa wametofautiana tu njia, wengine wamepitia njia za kidini na wengine wakapitia kwingineko… lakini mwisho wa siku wanayemwabudu na kumwomba ni shetani aidha kwa kujua au kutokujua.
Umeona umuhimu wa maombi? umeona sababu ya kuomba, maombi ni zaidi vile tunavyojua, na bila maombi hatuwezi kuishi kwa amani.
Sasa ni vizuri kufahamu unayepaswa kumuomba maana usipofahamu ukaenda kuomba tu kwa vile unavyojua wewe, mwisho wa siku hutopata hiyo amani, wala hatoweza kuishi vile ambavyo Mungu aliyekuumba alikusudia uishi.
Maandiko yanasema “shetani” anao uwezo wa kujibadilisha na kuwa malaika wa nuru (2Wakorintho 11:14), hivyo unaweza kudhani unamwabudi na kumwomba Mungu aliye hai kumbe unamwabudi shetani…na matokeo yake ni kukosa uzima, kwani shetani kamwe hawezi kumpa mtu uzima wala amani, wala usalama wowote maana yeye mwenyewe hana huo uzima ndani yake, tayari ameshahukumiwa ziwa la moto na wote wanaomwabudu pia watapata hiyo hukumu..biblia ndivyo inavyosema.
Sasa katika somo linalofuata tutangalia ni kwanamna gani tunaweza kuwa na uhakika wa tunayemwomba na kumwabudu kuwa ni yule aliyetuumba, Mungu muumba wa mbingu na nchi.
Je! umemwamini Yesu na kumpokea awe Bwana na mwokozi wako?
Unafahamu kuwa Yesu ndiye mwokozi wa ulimwengu na yeye ndiye njia ya kweli na uzima na pasipo yeye hakuna awezaye kumuona Mungu. Hebu soma haya maandiko na uyatafakari tena.
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
[17]Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
[18] AMWAMINIYE YEYE HAHUKUMIWI; ASIYEAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yohana 8:24 Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; KWA SABABU MSIPOSADIKI YA KUWA MIMI NDIYE, MTAKUFA KATIKA DHAMBI ZENU.
Je! unataka kufa na dhambi zako? Unafahamu hatari kubwa itakayokupata ukifa na dhambi? kwanini usimwamini huyu Yesu leo ambaye alilipa deni lote la dhambi pale msalabani.
Hebu, fanya maamuzi sahihi ya kumpokea Yesu na kuanza kufuata njia yake.. hapo ulipo piga magoti halafu fuatisha sala hii ya kumkaribisha Yesu Kristo maishani mwako. Tamka kwa sauti na kwa Imani, sema..
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.
Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Hongera kwa kuokoka.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada zaidi, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.