Lugha iliyonenwa siku ya pentekoste ilikuwa haieleweki kwa akili za kibinadamu?
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu katika mjadala huu tulitafakari neno la uzima!
Swali:”Je ni kweli ile lugha iliyonenwa wakati wa kunena kwa lugha(siku ya pentecoste haikuwa inaeleweka kwa lugha ya kawaida?Mbona katika matendo 2:3-11 watu walielewa kile kilichokuwa kinanenwa na mitume?”
Ukisoma Matendo ya Mitume 2:3-11 utaona Baada ya Roho Mtakatifu kushuka duniani siku ya pentekoste watu walianza kunena kwa Lugha na si kwamba walikuwa wananena lugha zisizo eleweka la! Bali zilikuwa zinaeleweka kabisa. Na hapa walikuwa wananena kila mmoja mmoja lugha tofauti tofauti na jambo hili lilifanyika makusudi ili Mungu kudhirisha uweza wake(maana walianza kuzungumza lugha ambazo hawazijui wala hawajaawahi kuzisikia ilikuwa ni kuonyesha matendo makuu ya Mungu)
Yaani ni sawa umsikie mzungu alieko ulaya hajawahi kuja Tanzania halafu unamsikia anazungumza Kihaya au Kisukuma au kimasai au kiha, au hata kiswahili ni wazi ni jambo ambalo litakushangaza. Sasa ndio jambo lile lilotokea kwa watu wale 120 kila mmoja walukuwa wakizungumza lugha za mataifa na ili hali hawakuwa wanazijua kabisa.
Tusome mstari wa nne katika tafasiri tofauti tofauti.
Matendo ya Mitume 2:
4“Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”
Sasa ukisoma Amplified Bible inasema..
Acts 2:4
[4]And they were all filled (diffused throughout their souls) with the Holy Spirit and began to speak in other (different, foreign) languages (tongues), as the Spirit kept giving them clear and loud expression [in each tongue in appropriate words].
Maana yake..
Matendo ya Mitume 2:4 “Wote wakajazwa (Roho Mtakatifu akaenea ndani ya nafsi zao) kwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine (tofauti, za kigeni), kama vile Roho alivyoendelea kuwapa uwezo wa kusema kwa sauti wazi na maneno sahihi kwa kila lugha.”
Unaona hapo walianza kunena kwa lugha zingine za kigeni yaani kulikuwa na watu wa kapadokia wakasikia lugha yao inanenwa,kulikuwa na Wamisri wakasikia Lugha yao ikinenwa,watu wa Mesopotamia wakasikia lugha yao na kama(kungekuwa na watanzania wangesikia Kiswahili pia).
Hii ilikuwa kudhirisha matendo makuu ya Mungu na anasema “kuwapa uwezo wa kusema kwa sauti wazi na maneno sahihi kwa kila lugha.”
Maana yake hawakuwa wanazungumza kwa kigugumizi au kukwama kwama, au kukosea kosea maneno la! Bali walikuwa wanaongea maneno kwa usahihi kana kwamba ni lugha yao asilia.. kama mtu anaszungumza lugha yake asilia anavyozungumza kwa ufasaha bila kukosea kosea.
Ndio maana baada ya wale watu kusikia kila mmoja lugha yao wakaanza kushangaa kwamba hawa wote ni wagalilaya inakuwaje wanazungumza lugha zetu? Tena kwa ufasaha kabisa kana kwamba wamekaa muda wakajifunza wakati ni tendo la muda mfupi tu(na katika lugha hizo walikuwa wanamtukuza Mungu)
Maandiko yanasema..
Acts 2:11[11]Cretans and Arabians too–we all hear them speaking in our own native tongues [and telling of] the mighty works of God!
Maana yake
Matendo ya Mitume 2:11 “Wakrete na Waarabu pia — sisi sote tunawasikia wakisema kwa lugha zetu za asili wakieleza matendo makuu ya Mungu!”
Kweli ni Matendo makuu ya ajabu mno.
Fikiria mtu anamaliza miezi mitatu labda anajifunza kiingereza na si kwamba ataelewa kila kitu inabidi aendelee kujifunza lakini jambo hilo linatokea ndani ya muda mfupi si jambo la kawaida tunae Mungu mkuu sana sana, Haleluya..
Sasa kunena kwa lugha nyingine ambayo hiyo ni lugha ya rohoni ambayo hakuna mtu anaeweza kuielewa hata anayenena nae pia hawezi kufahamu anaomba nini.. mpaka awesome mtu mwenye karama ya kufasiri hiyo lugha ndio ataoe tafasiri..
Paulo analiambia kanisa la Korintho kuwe na utaratibu wa kuzungumza kwa Lugha na kukiwa hakuna mtu wa kufasiri basi na wakae kimya wanene wao kama wao na Mungu..
1 Wakorintho 14 27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.
28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
Unaona hapo! Mmoja anaenena hawezi kufasiri anasema na mmoja afasiri kile kilichonenwa ikiwa ana karama hiyo maana ya kuhitaji tafasiri kwa sababu hakuna alielewa ni sawa Wazungu walipokuja huku kutuletea ijili aidha walilazimika kujifunza lugha zetu au wawe na watu wa kufasiri kile wanachosema..
Ndio maana Paulo anasema..
1 Wakorintho 14:14“Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.”
Unaona hapo? Kwamba akiomba kwa Lugha roho yake inaomba(maana ni lugha ya rohoni hivyo inatambulikana rohoni na si katika ulimwengu wa mwili.) Anasema akili zake hazina matunda yaani akili haina ufahamu juu ya kile kinachozungumzwa.
Hivyo kukiwa na mtumishi anafundisha kwa kuzungumza Lugha ya rohoni basi awesome mfasiri bila hivyo ni kazi bure maana watu wanasema
Paulo anasema..
1 Wakorintho 14:23 “Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?”
Hivyo hata unapomhubiria mtu usinene kwa lugha haelewi atakuona kama una wazimu hata kanisa linakutanika linaanza kunena kwa lugha tu ibada yote watu wanamaliza wanaondoka wageni waliokuja na wengine wataona ni watu mlio Pagawa maana hawafahamu juu ya hayo.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano:0613079530
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.