Mtu hataishi kwa Mkate tu,ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu
Je! Unaishi kwa kila neno linalotoka katika kimywa cha Mungu?
Mathayo 4:4″ Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”…
Na kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu ni lipi? Ikiwa hufahamu neno linalotoka katika kinywa cha Mungu basi itakuwa ni mgumu kuishi kwa kila neno na hapa ndio Wakristo wengi hajapaelewa vyema.
Neno linalotoka kwenye kinywa cha Mungu ni Biblia, maneno hayo yametoka katika kinywa cha Mungu kupitia watumishi wake kama utaipuuza biblia kuisoma mara kwa mara basi utakuwa unaipuuza sauti ya Mungu iliyo wazi kabisa.
Wakristo wengi wanatamani na wanakesha wanaomba wanataka kumsikia Mungu ndugu yangu ikiwa husomi biblia una asilimia 1% tu katika kumsikia Mungu na aidha unaweza usimsikie kabisa.
Kwa nini uishi kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu(tofautisha kunalisikia neno na kuliishi neno ni mambo mawili tofauti).
Sasa Wakristo wengi hawaishi kwa neno japokuwa tuko katika kizazi cha Wakristo wanaojua vizuri sana kuichambua biblia na wana vifungu vya biblia kwenye akili zao vingi lakini havina matunda yoyote.
“Kuna tofauti kubwa ya kulili neno(kulinakili kuwa nalo kwenye akili tu)na kulitamka na kuliamini”
Yaani unaweza ukalitamka Neno na unalijua lakini usiwe na uhakika nalo yaani ukawa na mashaka nalo ukaanza kusema “hivi ni kweli mhhh. Sidhani” ilihali unalijua lipo kwenye akili yako.
Kama wana wa Skewa walitamka tu kwa jina la Yesu Kristo anaehubiriwa na Paulo toka lakini hawakuwa na ufahamu juu ya Yesu Kristo na kwamba litaleta matokeo juu ya kile wanachokisema.(japo ni nje ya Muktadha lakini nimetolea mfano tutaona mbele kidogo).
Ili Neno la Mungu lilete matokeo katika maisha yako ni lazima kwanza uliamini uwe na uhakika nalo usiwe na shaka. (Katika somo lijalo nitakufundisha namna bora ya kuliamini neno la Mungu ili liwe na matokeo katika maisha yako na uishi kaa hilo).
Hivyo wengi wana mistari ya biblia lakini hawaiamini yaani hawana uhakika nayo japokuwa katika maombi nk wanaitaja kila siku ila hawafahamu uzito ulio katika hiyo mistari wanataja tu kama kiunganishi cha maombi yao.
Na Shetani anaendelea kuwataabisha ilihali wana neno lakini kwa sababu hawalifahamu kwa undani basi wanataabika( ndio maana si ajabu leo Mkristo kuwa na hofu anapaokuta hata damu ya mbuzi ama kuku imenyunyizwa katika mji wake au biashara yake anaaanza kuhangaika amesahau au hajui kuwa damu ya Yesu Kristo aliyonayo/iliyomuokoa ina nguvu kuliko damu ya kitu chochote kile na kupitia hiyo anao ulinzi na kila muda inafuta na kuzuia mabaya yeye anakua salama milele)
“Unaweza ukawa na neno kama hujafahamu uzito au undani wa hilo neno ukakaa na kutafakari na kufundishwa na kuelewa kwa undani haliwezi kukusaidia inabidi ukue uwe na ufahamu zaidi”
Mtu akisema Yohana 3:16 mfano unaelewa kwa undani zaidi nini maana yake.
Neno linakuwa na nguvu na hai katika maisha yako(kumbuka Neno siku zote ni hai) wewe unajukumu ya kulifanya kua hai katika maisha yako na inawezekana lakini usipotaka litaendelea kuwa hivyo hivyo tu..
Ndio maana Mkristo Leo ni Rahisi kunung’unika,kulaumu laumu,kukaa na chuki na vinyongo ilihali kwenye ufahamu wake ana Neno kalikalili “Shukuruni kwa kila jambo “ ana Neno linasema ….
1 Wakorintho 10:
10“Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.”
Analijua hili neno Lakini ni Mkristo anaeomgoza kwa manung’uniko katika kila jambo,
Maandiko yanasema…
Hosea 4:
6“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”
Unaona hapo anasema wanaangamizwa sio wanaangamia kwa kukosa maarifa..
Sasa maarifa ni nini?
Maarifa ni ufamu,uelewa au taarifa mtu anayokuwa nayo kuhusu jambo fulani, mara nyingi hupatikana katika kujifunza,kusoma,uzoefu na kutafakari.”
Hivyo kifupi “Maarifa ni kile unachojua,unachokielewa, na unachoweza kukitumia kwa hekima”.
Vivyo hivyo tunatakiwa kuna na maarifa,uelewa,ufahamu juu ya kweli ya mambo ya rohoni sio kujua tu basi.
Si kwamba neno hawana ndani hapana lakini hawana maarifa ya ndani juu ya hiyo mistari walionayo na kuitamka kila siku.
Amini kile maandiko yanachosema..
Omba maombi haya mafupi kwa imani.
“Eee Yesu Kristo ninaomba uniwezeshe na kunipa wepesi wa kuliamini neno lako na kuliishi, sihitaji kuwa na mashaka,na wasiwasi na neno lako, nahitaji kulifahamu kwa undani zaidi, nahitaji nikujue sana Asante Baba kwa kunisikia,Asante Baba kwa kunijibu,Asante Baba kwa Upendo wako, ninaomba nikiamini ni katika Jina la Yesu Kristo Amen”
Omba kwa kumaanisha na tamka kwa sauti na amini Mungu yupo hapo anakusikia, tambua unaeongea nae ni nani na ana uwezo gani na yeye si muongo,habadiliki aliacha enzi yote na kila kitu kuja kufa kwa ajili yako. Anakupenda na kukuthamini amini hilo na kili kila siku.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano:0613079530.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.