Mungu alimaanisha nini, kusema Mimi niko ambaye niko?

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana libarikiwe, karibu tujifunze.

Kipindi Musa anamuuliza Mungu kuhusu jina lake alitegemea kutajiwa jina fulani kama vile baali, Ashtoreth n.k
Zaidi tunaona Mungu anamjibu kwa jumla akisema, wakikuuliza jina langu waambie Mimi ni ” Niko ambaye Niko”

Kutoka 3:14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

Ukiangalia katika biblia yako kwa chini utaona tafsiri nzuri ya sentensi hii ikimaanisha ” NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA”i

Akimaanisha si kama nina jina moja tu maalumu, na lenye sifa fulani, Bali nitajulikana niwapo katika tukio hilo,tatizo au haja fulani, kwa hapo hilo ndio jina Langu.
Na tunaona baada ya muda mfupi, kitendo cha farao kugoma kuwaruhusu Wana wa Israel kuondoka misri, tena kwa kuwaongezea mateso zaidi, hapo ndipo Mungu alipoanza kujifunua majina yake

Kutoka 6:1-8[1]BWANA akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.

[2]Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;

[3]nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.

[4]Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.

[5]Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.

[6]Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;

[7]nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.

[8]Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni

YEHOVA.

Hilo ndilo jina lililowatoa Wana wa Israel misri ni jina la YEHOVA
Haikuishia hapo tunaona pia sehemu mbalimbali akijifunua kwa majina mengine kama Yehova nisi, Yehova shama, Yehova shalom, Ebenezeri n.k hivyo nyakati za vita, mahitaji huzuni n.k na hiyo ilitokea pale walipohitaji Msaada wa Mungu Mungu aliwasaidia..

Lakini mwisho kabisa anajifunua kwa jina kuu la UKOMBOZI nalo ni YESU, lenye maana Yehova Mwokozi.

Hi inatufundisha nini

Sikuzote imetupasa kumwelewa Mungu wetu kama ” NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA” kujifunua kwake kwetu hakuna mipaka, tukimaanisha wakati wa Raha, wakati wa shida, mabondeni, milimani Atajifunua. Jangwani, Nyikani, Visiwani Mabondeni, hata uendapo Mbinguni au kushuka mahali pa wafu Utamwona Mungu wako Akijifunua kwa maana yeye ni vyote kati ya yote.
Unapomwamini Yesu Kristo huhitaji tena kuwa na hofu, wasiwasi wala kumwekea mipaka ya kwamba jambo hili ataweza hili hataliweza…

Jiulize ndugu umemwamini Mungu Aliyejifunua kwako kama Mwokozi? Yani Kristo? Yakupasa uingie kwanza kwenye ukombozi ulioletwa na mwanae Yesu Kristo, kwasababu upo Katika dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti,

Ukimwamini Yesu Leo atakupa ondoleo la dhambi zako, nawe utakuwa na uzima wa milele. Ukifurahia katika wokovu sababu tayari umevushwa kutoka mautini kwenda uzimani…

Hizi ni siku za mwisho Kristo yupo mlangoni kuja kuwachukua walio wake, Jiulize siku ya unyakuo utakuwa wapi?

Maran atha..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *