Ninazo funguo za mauti na kuzimu

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Mungu muumba wetu.

Neno la Bwana linasema.

Ufunuo 1: 17 “…Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu”.

Alimaanisha kuwa hizo funguo Yesu hakuwa nazo mkononi mwake Bali zilikuwa kwa ibilisi.

Hapo mwanzo Mungu alimuambia Adamu na Hawa wasile tunda la mti wa uzima ambapo wangekula matunda hayo mwisho wa siku wangebaki uchi na kuupoteza utukufu wa Mungu aliouweka NDANI yao pia ingepelekea kigo Cha Moja kwa Moja kwa upande wao.

Katika agano la kale waliokuwa wanauhakika na maisha baada ya kifo ni Wana WA Israeli ambao baadhi Yao walikuwa wanafuata masuala ya mesiya ambaye alitabiriwa kuwa atawafufua watu lakini baadhi Yao hawakulijua Hilo.

Ikapelekea mashindano kati ya mafarisayo na masadukayo kwakywa baadhi waliamini ufufuo na baadhi hawakuamini kama inavyosemwa katika matendo ya mitume 4:1_2, 23:7_8 na Marko 12:18 kwakuwa suala la ufufuo halikuwa wazi kabisa katika maandiko.neno linasema

Warumi 5:14 “walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja”.

Wakati huo wote shetani alikuwa nazo hizo funguo na Kuna wakati alikuwa anao uwezo wa kuongea na wafu soma (1samweli 28).

Yesu alifanya mapinduzi ya badala ya mauti ni kifo akaweka uzima ambapo alizungumzia zaidi kwa habari ya mauri itokanayo na kula matunda ya mti wa mema na mabaya.neno linasema

Waebrania 2:14 “Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,

15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa”.

Aliiteka kuzimu iliyokuwa ikimilikiwa na shetani ambayo ni makao ya watu wote.

Hata akasema makaburi yalipasuka na watakatifu wengi watafufuka.neno linasema.

Mathayo 27:51 “Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;

52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;

53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”.

Hivyo inatupasa kumfuata na kumkimbilia yesu kristo aliye kimbilio na msada wetu kwakuwa anazo yeye funguo za mauti na uzima.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *