Nini maana ya mtu asinie makuu kuliko ilivyompasa kunia (warumi 12:3)

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana Yesu Kristo Lihimidiwe. Karibu tujifunze maneno ya Uzima…

Maandiko yanasema katika..


Warumi 12:3
” Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu ASINIE MAKUU KUPITA ILIVYOMPASA KUNIA; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.”

SWALI linakuja, JE! Huko Kunia makuu ndio kufanyaje?

Warumi 12:4-8
4″ Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;

5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.

6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.”

Maana yake ni usiwe na moyo wa kujiona au kuwaza moyoni mwako na kujiona unaweza kuwa ” una karama au vipawa vingi kuliko mwingine..
Mfano pale mwamini mmoja anapojiinua na kuhisi yeye ndie muinjilisti, nabii, mwalimu au mtume Yani anaona kuwa karama za Rohoni zote ni zake hawezi kuwa nayo moja tu, “Yani mimi niwe mwalimu pekee? Hapana lazima nitakuwa nabii, mtume au hata nabii mkuu .” Maswali Hayo ndio hujaa kichwani mwake
Sasa hayo ni machache kati ya Yale biblia inatuasa tusinie makuu kuliko itupasavyo kunia.

Roho ya unyenyekevu ndani ya mtu hufa kwa kunia makuu, hatimaye mtu huyo kufa kabisa Kiroho


1 Petro 5:5
“……… Mungu huwapinga wenye KIBURI, lakini huwapa wanyenyekevu NEEMA.”

Sikuzote karama tulizopewa SI za mashindano! Yupi kabarikiwa kuliko wote, la! Karama tupewazo si kwa matumizi hayo. Na shetani huwa ndani ya Kila karama yenye fikra hizo.
Karama zetu ni kwa ajili ya kuujenga mwili wa kristo na kuwakamilisha watakatifu wake, si kwa mengineyo!

Waefeso 4:11-12
11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;”

Hakika Bwana atusaidie.

Kama hujampa Kristo maisha yako kikamilifu, Mlango u wazi Sasa lakini hakutakuwa hivyo sikuzote. Fanya maamuzi Leo maana kesho inaweza kuwa tayari umechelewa, muda tulio nao duniani SI rafiki ni mchache sana! Parapanda Italia wakati wowote kristo atalinyakua kanisa lake, kitakachobaki juu ya usi wa nchi ni hukumu! Mpendwa Ni Imani yangu Mimi na wewe hatutakuwa miongoni mwa watakaokutwa wa hukumu ya Mungu.

Mpendwa Mbingu IPO pia na kuzimu nayo ipo. Uchaguzi wa uzima na mauti u hapa hapa duniani angali tupo hai, baada ya kifo hakuna nafasi ya uchaguzi. Fanya maamuzi sahihi ingali upo hai!

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *