YULE BIBI WA MAMBO YA UCHAWI, AUZAYE MATAIFA KWA UKAHABA WAKE.

Biblia kwa kina No Comments

YULE BIBI WA MAMBO YA UCHAWI, AUZAYE MATAIFA KWA UKAHABA WAKE.

Nahumu 3:4-7 “Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa YULE KAHABA MZURI, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake.

[5]Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.

[6]Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau.

[7]Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikutafutie wapi wafariji?

Isaya 47:1 Haya, shuka, keti mavumbini, Ewe bikira, binti Babeli; Keti chini pasipo kiti cha enzi, Ewe binti wa Wakaldayo; Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.

[3]Uchi wako utafunuliwa, Naam, aibu yako itaonekana. Nitalipa kisasi; simkubali mtu ye yote.

[6]Nalikuwa nimekasirika na watu wangu, naliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; uliwatia wazee nira yako, nayo nzito sana.

[7]UKASEMA, MIMI NITAKUWA BIBI MILELE; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.

[8]Sasa, basi, sikia haya, wewe upendaye anasa, ukaaye na kujiona salama, wewe usemaye moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi; sitaketi mfano wa mjane, wala sitajua kufiwa na watoto;

[9]lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno.

[10]Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.

[11]Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua.

[12]Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.

[13]Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.

[14]Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao.

[15]Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa”.

Huu ni mfufulizo wa masomo yanayohusu ile dini ya Babeli (KATOLIKI), kumbuka hapa hatupo kwa ajili ya kubeza au kushabikia dini au dhehebu fulani, wala wakatoliki sio watu wabaya, lakini ni vizuri ukweli usemwe ili watu wa Mungu wafunguliwe.

Hivyo, wewe kama ni mkatoliki au mwanamadhehebu kutoka katoliki, unachopaswa kujua ni ukweli kuhusu dhehebu lako na mambo yanayoendelea huko…ulinganishe na ukweli wa Neno la Mungu ukiomba Roho Mtakatifu akusaidie kufahamu ukweli wa maandiko.

Ukifuatilia katika historia huku ukilinganisha yaliyoandikwa katika biblia takatifu, utajua kuwa Kanisa katoliki ndio kanisa mama na ndio chipuko la madhehebu yote, Kanisa mama ikiwa na maana ni kanisa lililozaa makanisa mengine yanayofananaye, ndio yule MAMA WA MAKAHABA tunayemsoma katika…

Ufunuo wa Yohana 17:1 “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule KAHABA MKUU aketiye juu ya MAJI MENGI;

[2]ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi WAMELEVYWA KWA MVINYO YA UASHERARATI WAKE.

[3]Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya MNYAMA MWEKUNDU SANA, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

[4]Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

[5]Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

[6]Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.”

Kumbuka katika biblia mwanamke anawakilisha KANISA, Sisi wakristo tunatambulika kama BIBI-ARUSI wa KRISTO, (2Wakoritho 11:2 Paulo anasema “..Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo BIKIRA SAFI. “) Na pia..

Ufunuo 19:7 inasema..” Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na MKEWE amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Pia Taifa la Israeli Bwana alilitambua kama MKE WAKE” [soma ezekieli16:1-63, ezekieli 23] utaona jambo hilo. Hivyo mahali popote Mungu anapozungumza juu ya kundi la watu wake huwa analifananisha na mwanamke.

Lakini hapa tukisoma hiyo habari hapo juu tunaona mwanamke mwingine ametokea ambaye anaonekana ni KAHABA, amelewa kwa DAMU za watakatifu na za mashahidi wa YESU, na tena wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake ana jina limeandikwa, la SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Hivyo tunaona tabia ya huyu mwanamke (ambaye anawakilisha KANISA fulani) kuwa ni KAHABA, Na kama tunavyofahamu kanisa la KRISTO haliwezi kuwa kahaba, kwasababu ni BIKIRA SAFI, na haliwezi kuua watakatifu wa Mungu, kwasababu lenyewe ni TAKATIFU, Hivyo hili Kanisa haliwezi kuwa lingine zaidi ya KANISA KATOLIKI chini ya uongozi wa PAPA.

Kwanini ni Kanisa KATOLIKI na si kitu kingine?

Tunajua siku zote shetani anatabia ya kuunda “copy” inayofanana na ya Mungu ili aabudiwe kirahisi, au kudanganya watu kirahisi, vinginevyo asingeweza kupata wengi, ili noti feki iweze kufanya kazi ni lazima ifanane sana na orijino, shetani anataka kuabudiwa kama Mungu hivyo atatumia njia zote zinazofanana na za Mungu ili apate wafuasi wengi. Na ndio maana Mungu alikataza Mtu kutengeneza mfano wa Kitu chochote kama Mungu ili kukiabudu kwasababu mtu anaweza akadhani anamwabudu Mungu kumbe anamwabudu shetani mwenyewe kwa kivuli cha ile sanamu pasipo kujua. Mimi sipo kinyume na wakatoliki, wala siwahukumu ndugu zangu wakatoliki, bali nipo kinyume na mifumo ya kanisa Katoliki kwasababu Mungu alishaihukumu, na kupiga mbiu watu wake watoke huko wasishiriki mapigo yake!.

Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

[5]Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.”

Sasa mpango wa Mungu aliouunda tangu awali ni kumleta “MTU” atakayesimama kwa niaba yake ili kuwakomboa wanadamu (VICAR) katika dhambi zao hivyo akamleta mwanae anayeitwa YESU KRISTO, ambaye kwetu sisi ni Mungu mwenyewe katika mwili..shetani kuona hivyo akaanza kuiga kwa kumtengeneza mtu wake (VICAR), ambaye naye atasimama kwa niaba yake hapa duniani, na akampa jina lililo maarufu (VICARIUS FILII DEI) yaani tafsiri yake, ni “Badala ya mwana wa Mungu duniani”, hivyo huyu mtu wake anasimama hapa duniani badala ya mwana wa Mungu (yaani YESU KRISTO), na shetani akamvika uwezo wake bandia kwamba na yeye anaweza kusamehe dhambi duniani kama vile BWANA WETU YESU KRISTO alivyo na uwezo wa kusamehe dhambi.

Na kama vile Mungu alivyounda kanisa lake takatifu kwa kupitia BWANA YESU KRISTO, ambalo ndilo linaloitwa BIBI-ARUSI safi, vivyo hivyo shetani naye alilitengeneza Kanisa lake kwa kupitia huyu (VICARIUS FILII DEII) yaani PAPA, Kutimiza kusudi lake la kutaka kuabudiwa na kupeleka watu kuzimu na hilo KANISA ndilo KAHABA, Na si lingine zaidi ya KANISA KATOLIKI.

Na tunajua Kanisa la Kristo safi linaongozwa na ROHO MTAKATIFU kwa kupitia zile huduma na karama za roho, yaani mitume, manabii, wachungaji, wainjilisti na waalimu lakini hili kanisa kahaba na lenyewe limevuviwa vyeo vya uongozi kama Upapa, Ukadinali, upadre, paroko, ukasisi n.k.

Kwahiyo unaweza ukaona ni jinsi gani cha uongo kinavyofanana na cha ukweli, na watu wengi wamepofushwa macho na shetani wakidhani kuwa wanamwabudu Mungu hapo kumbe ni shetani.

Na ni kwasababu gani ni kahaba?

Ni kahaba kwasababu biblia inasema wafalme wa nchi wamezini naye nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo wa uasherati wake, si ajabu Kanisa hili lina nguvu nyingi katika mataifa mengi kwa utajiri wake kwa jinsi linavyotoa misaada na miradi mingi ya kimaendeleo na ya kijamii, linajenga mashule na mahospitali linatoa misaada ya majanga na kusapoti siasa za nchi, linafanya hivi kwa lengo moja tu! kupumbaza mataifa na wafalme wa nchi ili kuwalewesha kwa kupenyeza mafundisho na itikadi zake za uongo kwa watu ambazo zipo nje ya MANENO MATAKATIFU YA MUNGU.

Na ndio maana tunaona mwanamke huyu ana jina limeandikwa kwa SIRI katika kipaji cha uso wake “BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI”..Umeona hapo, jina lake lipo katika SIRI, hivyo inahitaji HEKIMA kumtambua, kwasababu shetani huwa hafanyi vitu vyake kwa wazi wazi, anatumia kivuli cha “orijino” ili kuwadanganya watu.

Ni BABELI mkuu kwasababu tafsiri yenyewe ya neno BABELI ni “MACHAFUKO”, Hivyo Mji wa Babeli ndio ulikuwa chimbuko la machafuko yote, ibada za kipagani za kuabudu miungu mingi na uchawi ndipo zilipozaliwa, Nimrodi akiwa muasisi wa mji ule na mke wake Semiramis pamoja na mtoto wao Tamuzi, waliabudiwa kama miungu, ndipo baadaye Waroma wakaja kutohoa mfumo huo wa kuabudu miungi mingi, na sio ajabu tunaona baadaye wakaja kumweka Yosefu kama Nimrodi, Semiramis kama Mariam na Tamuz kama mtoto YESU ili kutimiza matakwa yao ya ibada zao za sanamu ambazo walikuwa nazo tangu zamani, kwakweli haya ni machafuko makubwa sana katika KANISA LA KRISTO.

Na mji huu huu wa Babeli baadaye ndio uliohusika kuutesa na kuuchukua uzao wa Mungu (ISRAELI) mateka, sasa hii ilikuwa ni Babeli ya mwilini iliyolichukuwa Taifa la Israeli mateka sasa hii iliyopo leo ni BABELI YA ROHONI (ambayo ni kanisa Katoliki ) inawachukua wakristo wengi mateka kwa kuwafanya waabudu miungu mingine mbali na YAHWE YESU KRISTO MUNGU WETU.

Lakini Biblia inasema hakika BABELI HII ya sasa itaangushwa tu! kama ilivyoangushwa ile ya kwanza ya mwilini… Tunasoma

Ufunuo wa Yohana 18:1 “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

[2]Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

[3]kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za KIBURI CHAKE.

[4]Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

[5]Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.

[6]Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.

[7]Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.

[8]Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.

[9]Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;

[10]wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

[11]Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;

[12]bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;

[13]na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.

[14]Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.

[15]Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza,

[16]wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu;

[17]kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali;

[18]wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa!

[19]Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.

[20]Furahini juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na mitume na manabii; kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.

[21]Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.

[22]Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;

[23]wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa UCHAWI WAKO.

[24]Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi”.

Nadhani kuanzia hapo utakuwa umeanza kupata picha ni kwanini mwanamke yule anajulikana kama BABELI MKUU. Sasa tuone ni kwa nini anaitwa “MAMA WA MAKAHABA”.

Ni Mama wa makahaba kwasababu amezaa mabinti ambao nao pia ni makahaba kama yeye na si mengine zaidi ya madhehebu yote yanayoshirikiana naye, wale waliokuwa wanajiita ma-protestants mwanzo sasa hivi hawapo hivyo tena, wanashirikiana naye kwa namna zote. Kanisa Katoliki limefanikiwa kuwalewesha na kuwavuta tena kwake, lutheran imeshaungana na katoliki rasmi, pamoja na madhehebu mengine mengi, na ndio maana linaitwa “KANISA MAMA”. Sasa ni rahisi kuelewa hapo kwanini ni “MAMA WA MAKAHABA”..Kwasababu yeye ameshakuwa kanisa mama, na mabinti wake wameshafuata mifumo yake ya ibada zisizotokana na NENO la Mungu.

Na ni kwanini ni “Mama wa Machukizo ya nchi”?.

Hili kanisa lenyewe ndio linalohusika na machukizo yote ya nchi yanayovuta ghadhabu yote ya Mungu juu ya nchi, kama ya kuwauwa watakatifu wa Mungu, kimwili na kiroho, kwa ibada zake za sanamu, kanisa hili limeua zaidi ya wakristo milioni 68 katika historia hiyo ni idadi kubwa sana, hata Bwana YESU alishatabiri juu yao alisema..Yohana 16:1-3″Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania KILA MTU AWAUAYE YA KUWA ANAMTOLEA MUNGU IBADA. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. ”

Hiyo ndio sababu ya yule mwanamke kuonekana amelewa kwa damu za watakatifu ..Haya yote ni machukizo makuu mbele za Mungu, na yule mpinga-kristo atakayetokea huko ndiye atakayelisimamisha lile CHUKIZO LA UHARIBIFU lililotabiriwa na nabii Daneli na BWANA wetu YESU KRISTO, ndio maana anajulikana kama “MAMA WA MACHUKIZO YA NCHI”.

Hivyo ndugu leo umeujua ukweli, huwenda umezaliwa katika dini ukafundishwa tararibu zote, lakini leo umeujua ukweli, biblia inasema njia iendayo uzimani ni nyembamba tena imesonga, amua leo kuingia katika mlango huu mwembamba ili uwe bibi-arusi wa Kristo atakayekwenda kwenye karamu ya mwanakondoo maana karamu i tayari. Ni wazi kabisa muda umeshaisha, amua kuwa bibi-arusi wa kweli asiyeabudu sanamu, bibi-arusi aliyebikira kwa NENO tu na sio pamoja na mapokeo mengine yaliyo nje na NENO LA MUNGU Kama kusali Rosari na ibada za wafu. Bibi-arusi Anayemwabudu Mungu katika Roho na kweli sio katika mifumo ya ki-DINI na ya-kimadhehebu, Bibi-arusi aliyepokea kweli ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kama tunavyofahamu asili ya bibi-arusi ni kuvaa vazi refu la kujisitiri, je! na wewe mwanamke mavazi yako ni ya kujisitiri?, Utakuwa mkristo na bado uwe kahaba kwa mavazi unayovaa? kumbuka fashion zote ni dhambi! lipstic,vimini, wigy,suruali, wanja nk. vitakupeleka kuzimu mwanamke.

BWANA YESU ANASEMA…

Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, NA HAO WAABUDUO SANAMU, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.

17 NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

TUBU ANGALI MUDA UPO.

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *