ACHA DHAMBI!! ACHA DHAMBI!!!

Dhambi No Comments

ACHA DHAMBI!! ACHA DHAMBI!!

Hakuna muujiza wowote wa kumfanya mtu aache dhambi, ni yeye mwenyewe aamue kuacha kabisa kwa akili zake. Unapodhamiria kuacha dhambi kwa vitendo kabisa ndipo msaada wa Mungu utakuja ndani yako na kukusadia, lakini kama unasubiri muujiza ukushukie tu hivi hivi nakuambia ukweli utasubiri sana, wala usidhani kuna maombi yatakufanya uache dhambi ondoa hayo mawazo kabisa ndani yako, maombi yanakufungua tu katika vifungo lakini jukumu la kuacha dhambi bado lipo kwako!!, na huwezi kutoa sadaka ili upokee muujiza wa kuacha dhambi.. haijalishi utatoa mamilioni ya pesa, bado unayojukumu la kuacha dhambi mwenyewe…na usipoacha utaendelea kuwa mtumwa wa dhambi mpaka unashuka kuzimu.

Nakuambia haya, si kwa lengo la kukuogopesha, lakini nitakuambia mapema ili leo ujue na uchukue hatua ya kuacha dhambi mara moja.

Tukisoma katika biblia ile habari ya Paulo Mtume, ambaye hapo kwanza alikuwa anaitwa sauli kabla hajakutana na Bwana Yesu, tunasoma baada ya kukutana na Bwana alipewa agizo la kwenda kuwageuza watu waachane na matendo maovu na sio akawaombee ili waache, tunasoma..

Matendo 26:13 “….ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.

14 Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.

15 Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi.

16 Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;

17 nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao;

18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza WAIACHE GIZA NA KUIELEKEA NURU, WAZIACHE NA NGUVU ZA SHETANI NA KUMWELEKEA MUNGU; KISHA WAPATE MSAMAHA WA DHAMBI ZAO, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi”.

Unaona mstari wa mwisho aliambiwa awafundishe watu WAIACHE GIZA WAIGEUKIE NURU, kuacha giza maana yake ni kuacha matendo yote ya giza, kama uasherati, ulevi, wizi, uongo, uchawi, n.k.

Lakini pia aliagizwa awageuze watu WAZIACHE NGUVU ZA SHETANI NA KUMGEUKIA MUNGU: zingatia hilo Neno ‘WAZIACHE’ sio wakaombewe! Wengi sasahivi wanatafuta kwenda kuombewa waache uasherati, au uchawi, au wizi, utasikia mtu anakuambia niombee niacha uasherati!…Ndugu hivyo vitu haviwezi kuondoka kwa kuombewa peke yake kama wewe mwenyewe kutoka moyoni mwako hujakusudia kuviacha…hata uombeweje haviwezi kuondoka kama hujakata shauri..Maana ya kutubu ni kuacha kile ulichokuwa unakifanya hapo kabla…sio tu kuomba msamaha peke yake! Hapana msamaha lazima uambatane na vitendo. Unapotubia uasherati maana yake unaachana na huyo mtu unayetembea naye sasa ambaye si mke wako au mume wako, unaachana na utazamaji wa pornography, na ufanyaji wa pornography, na ufanyaji wa masturbation, unakwenda kuchoma nguo zote za kiasherati, na mambo yote yanayohusiana na uasherati, kadhalika na uchawi ni hivyo hivyo unachoma nyenzo zote za kichawi na unaacha kabisa na hayo mambo…hiyo ndio maana ya kutubu!

Mithali 28:13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye NA KUZIACHA atapata rehema”.

Usiendelee kumpa ibilisi nafasi, amua leo kubadilika kwa KUACHA DHAMBI.. ACHA DHAMBI, ACHA DHAMBI..Hakuna dawa nyingine zaidi ya hii ACHA!, na MUNGU atakusaidia..

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *