Nini maana ya Neno jehanamu?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu,

Ulishawahi kujiuliza maana ya hili neno na asili yake ni nini, jehanamu ni neno lenye asili ya kiyunani lenye chimbuko la neno Gehenna ambapo sasa kwa asili ya kiyahudi ni ge-hinnom

Lenye maana ya bonde la Mwana wa hinomu, eneo hili lilikuwa kusini mwa Yerusalemu na kujulikana kama ,Toffethi, ndio ilitumika kwa watu wasiomcha Bwana kama sehemu ya kutolea kafara zao za Watoto kwa mungu wao waliyoipata huko kanaani, ambapo kiuhalisia halikuwa jambo jema kwa Mungu wala linalompendeza,ukiwa masomaji mzuri utagundua pia ni jambo lililowafanya hata wapelekwe kwenye utumwa huko babeli,

Zaidi sana biblia takatifu imetuelezea kwa undani kuhusiana na jehanamu, ni jisi gani kulivyo na wa nini kinafanyika huko,hebu tusome baadhi ya vifungu vya biblia..

Tusome..

Jeremia 7:30 “Maana wana wa Yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu, asema Bwana; wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo, iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi.

31 Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.”

Yeremia 19:1 “Bwana akasema hivi, Enenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;

2 ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia,

3 ukisema, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka.

4 Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;

5 nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu;

6 basi, angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo.”

Umeona mambo yaliyokuwa yakitendeka, lakini badae tunaona Mfalme aliyejulikana kama Yosia aliyetabiriwa kwa kipindi kirefu anakuja kuondoa na kulitia unajisi hata lisitumike tena kwenye mambo ya kishirikina kama walivyokuwa wakifanya..

2Wafalme 23:10 “Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.”

Mfalme Yosia baada ya kulinajisi na kulifanya lisifanye kazi za kichawi tena, bonde hili likabakia kama sehemu kutupia takataka chafu,miili ya wanyama na watu waliokufa na kila aina ya uchafu basi ulitupwa huko, hivyo ikafanya bonde hilo kuwa na moshi uliopanda juu nyakati zote pamoja na harufu kali ya uchafu huo,

FUNZA WA JEHANAMU

Kuna sehemu ambazo kwenye bonde hili moto haukuweza kufika na kuchoma takataka au hata mizoga ya miili hivyo ikapelekea funza wengi sana sana kuwepo kwenye bonde, ilikuwa ni sehemu mbaya na chafu sana, sehemu ambayo kibinadamu huwezi kukaa ata dakika moja kutokana na harufu yake kuwa mbaya, funza wake kwenye bonde hili kufa kulikuwa kwa shida, walikuwa hawafi ukilinganisha na funza wengine,hawa walikuwa na utofauti sana..

Na huu ni mfano mdogo sana, ambao tunasoma kwenye maandiko kwa wale wote watakaokufa kama hawajampokea Bwana Yesu, jehanamu imeelezea uhalisia mdogo wa jinsi kuzimu kulivyo..

Embu tusome..

Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;

44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 9.45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [

46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]

47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;

48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.”

Maisha ya kuzimu ni mabaya sana, na asili ya mwanadamu hajaumbiwa kuteseka,mateso yake ni makali sana, na tukiyajua haya yanazidi kutupa sababu za kujiepusha na dhambi ili tusiende kuzimu, Kumbuka ukishaingia huko hakuna kutoka milele, utateseka na kuhangaika,usubiri siku ya mwisho uingie kwenye moto wa milele,uteseke milele yote si mahali pa kutamani kabisa,

Yesu pekee ndiye awezaye kukuepusha na mateso haya endapo utaamua kumpokea leo na kuwa Bwana wa maisha yako, unasubiri nini, utajauje kama kesho utakuwa hai tena, mkabidhi Yesu Kristo moyo wako..

Warumi 13:11

[11]Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini

Shalom..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *