Nuhu aliuhukumu je ulimwengu?

Maswali ya Biblia No Comments

Nuhu aliuhukumu je ulimwengu?

Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Maandiko yanasema kuwa Nuhu aliuhukumu ulimwengu makosa, je Nuhu alikaa katika kiti cha enzi na kuanza kuuhukumu ulimwengu?

Waebrania 11:7
“Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo *akauhukumu makosa ulimwengu,* akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.”

Unaona hapo? Anasema… “….. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu,….” Sasa ni hukumu ipi aliuhukumu ulimwengu?

Sasa ili kufahamu kwa kina Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anawazungumzia mashujaa wa imani moja wapo Nuhu. Maandiko yanasema kwa imani maana yake Nuhu hapa hakuongozwa na uzoefu au ubunifu wake binafsi bali aliona uhalisia kamili kwa imani na akaamini kwamba hayo mambo yanakuja maana “imani ni kuwa na hakika… Waebrania 11:1).

Na kupitia imani hiyo iliambatana na matendo na utii kwa Mungu juu ya kile alichoonyeshwa.

Sasa Nuhu aliuhukumu vipi ulimwengu? Maandiko yanaposema hivi maana yake ni kwamba kutokana na imani aliyokua nayo Nuhu na kupelekea kutii hiyo ikafanya ulimwengu uhukumiwe kwa sababu yake._

Yaani kwa maana nyingine kwa sababu Nuhu alitii na wengine hawakutii kielelezo cha haki kilisimama dhidi ya uasi wa wengi ambao hawakuikubali kuitii kweli ijapokuwa Nuhu aliwashuhudia hata wao dhamiri zao ziliwashuhudia lakini hawakutaka kusikia wala kutii.

Ndipo hapo Mungu akauhukumu ulimwengu kupitia imani au utii kwa Nuhu.

Na hii ikionyesha dhahiri kuwa Mungu hana “ Wengi wape”yeye siku zote anasimama katika Neno lake alitimize, hatishwi na wingi wa watu.

Je na sisi tunauhukumu/ulimwengu tutauhukumu?

Jibu ni ndio kama kipindi cha Nuhu watu walihubiriwa injili hawakutii kama ilivyo Sasa ingawa watu wanashuhudiwa ndani yao na Roho Mtakatifu lakini hawataki kutii wakati utakapofika Bwana Yesu atalichukua kanisa lake(Sisi tuliotii) na wengine wote waliobakia watahukumiwa.

Injili tunayo hubiri ni huku pia maana ya hukumu sio adhabu tu kwa tafasiri pana hukumu ni uamuzi mtu anaochukua. Hivyo tunapohubiri Injili mtu akikubali maana yake amefanya maamuzi ya kutii akikataa maana yake amefanya maamuzi (hukumu) ya kutokutii na huyo ameshakwisha kuhumiwa..

Maandiko yanasema…

Marko 16:16
“Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”

Mwandishi anasema tena..

Yohana 3:18
“Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.”

Na watu watakuhumiwa si kwa sababu hawajaisikia injili la! Au si kwa sababu hawakuielewa injili la! Bali walisikia,wakaelewa kwa maamuzi yao wenyewe wakakataa kutii..

Yohana 3:19
“Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.”

Unaona hapo? Anasema Nuru imekuja ulimwengu(Yesu Kristo) anasema na watu wakapenda giza kuliko nuru.. unaona hapo? Hawa watu hawakupenda tu giza pasipo kuiona nuru la! Waliiona nuru lakini baada ya kuiona nuru wao wakafanya uamuzi(wakalinganisha Nuru na giza kipi bora kwao wakaona giza kwao ni bora).

Hivyo ulimwengu unahukumiwa kila siku unaposikia injili na siku ya mwisho imekaribia sana sana.  Usidhani bado Muda mwingi ndugu yangu hata watu wa kipindi cha Nuhu walijia bado sana.

Lakini siku moja isiyojulikana kwao na wakiona ni yakawaida tu wakawa wana endelea na kazi zao uangamivu ukawafikia na ndivyo ilivyo..

1 Wathesalonike 5

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

Je! Umemwamini Yesu Kristo? Una uhakika unao uzima wa milele? Kama bado haujamwamini Yesu Kristo unasubiri nini? Na kama umeamini hauna uhakika ndani yako tengeneza njia zako unayo nafasi Mungu anakupenda na ndio maana ujumbe huu unausoma sasa si kwa Bahati mbaya usicheze pata potea na maisha yako yanathamani sana.

Mungu akubariki sana.

Maranatha.

Mawasiliano 0613079530.

@ Nuru ya upendo.

 

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *